hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,438
- 27,011
Baada ya kichapo cha 2-0 tulichopata jana chelsea kutoka kwa Everton ni rasmi sasa toka mwaka 2023 uanze hadi leo chelsea tumecheza jumla mechi 39 Epl lakini aibu ni kuwa katika mechi hizo 39 tumepata point 39 tu sawa na wastani wa point 1 kila mechi Average hii maana yake ni sawa na kusema toka mwaka 2023 uanze chelsea hatujashinda mechi yoyote Epl.
Baada ya chelsea kutapeliwa na Brighton kwa kuuziwa Moises Caicedo kwa €116 million sawa na Tsh 312,797,746,800.00/= Bilion mia tatu kumi na mbili, milion mia saba tisini na saba, laki saba na elfu arobaini na sita na mia nane bila senti, ni rasmi sasa Caicedo Kacheza jumla ya mechi 14 Epl lakini aibu ni kuwa katika mechi hizo chelsea tumeshinda mechi 3 tu na katika mashindano yote kacheza mechi 17 kinachosikitisha ni kuwa katika mechi zote mashindano yote tangu aje chelsea hajawahi kuhusika katika mchango wa goli lolote hana goli wala hajawahi kutoa assist hata moja alichofanikiwa ni kupata kadi za njano 3 hadi sasa.
Si mnakumbuka Everton walikatwa point 10 Epl na mkacheka sana? sasa nasikitika kuwakumbusha zile point walizokatwa hazijasaidia kitu wamebakiza point 6 tu wafikie point tulizo nazo chelsea na aibu ni kuwa chelsea hatujakatwa point hata moja.When push comes to shove naendelea kuomba radhi kwa uchambuzi huu ulio chini ya kiwango nitaendelea kujitahidi ili siku moja na mimi niwe mchambuzi mzuri kama nyie
Nasema uongo ndugu zangu? Basi mniombee.


Hapa inawezekana kuna mitazamo 2 ya kufanyia maamuzi.