Tuwachambue wachezaji wetu ili tuone wachezaji ndio wenye shida au kocha
1: Reece James
Iwapo James ataendelea kuwa fiti, yeye ni mchezaji wa kiwango cha kimataifa ambaye huingia katika timu yoyote duniani. Ni mshindi wa Ligi ya Mabingwa pia

Ana uzoefu.
2. Enzo Fernandez
Huenda alicheza Ulaya mwaka mmoja kabla hatujamnunua, lakini karibu vilabu vyote vya juu vilimfuata. Ameshinda Kombe la Dunia na kushinda mchezaji mdogo wa mashindano. Ana uzoefu pia, bila shaka. Yeye ni Bingwa.
3. Moises Caicedo
Liverpool, Arsenal, City na Chelsea zisingepigania kumsajili kutokana na kwamba alikuwa mbabe. Kila mtu anajua ubora wake. Mtumie vizuri na tuna mchezaji ndani yake. Yeye ni daraja la dunia.
4. Levi Colwill
Anaweza kuwa mdogo lakini amejaa ubora. Arsenal, Brighton na Liverpool hawangemtazama kama si mzuri. Mcheze katika nafasi yake na utapata mchezaji wa mfano. Kocha hapa ni wa muhimu.
5. Cole Palmer
Pasi zake, pressing na maono yake yako waziwazi hapa. Wengine wanasema yeye ni Kevin De Bruyne Regen, wengine wanasema Mata. Hii inaonyesha ubora alionao. Akitumiwa vizuri ni msaada mkubwa kwa Chelsea
6. Conor Gallagher
Penda au usipende, Gallagher ni mchezaji wa ajabu ambaye yuko uwanja mzima hasa katika safu ya kiungo. Alikosa katika mechi iliyopita an Man United na tuliona pengo lake
7. Mykhailo Mudryk
Kuna mchezaji hapa mkubwa sana. Kwa ufundishaji sahihi na kumfanya ajiamini, anaweza kufanya mengi na ya maajabu kwa timu. Ni mchezaji ambaye ana madhara kwa timu pinzani hata kwa uchezaji wake mdogo tu. Ana nguvu, ana mwendo mkali na bado mdogo.
8. Raheem Sterling
Anaweza asiwe na uchezaji ule ule mzurio kwenye kila mechi lakini ameonyesha ubora wake msimu huu na kwamba chini ya kocha mahiri angeifaa sana Chelsea kuleta madhara kwenye eneo la wapinzani wetu.
9. Wengine
Sikuwasema wachezaji kama Silva, Badiashile, Disasi, Nkunku, Lavia, Ben Chilwell, Wesley Fofana hata Cucurella. Kuna ubora katika timu hii ambao unaweza kupigania mataji kwa urahisi wakati wote wako fiti na wakiwa na kukiwa na ufundishaji mzuri na sahihi kitu ambacho kinakosekana kwa sasa kwa Pochettino
Ingawa bado tunahitaji Mshambuliaji wa kiwango cha Dunia.