Anaongea shit alijua sisi tunatania
Nakumbuka nilipoanza kutoa taarifa za Caicedo kuikataa Liverpool, walinijia juu na matusi kwa maana walishajua kwa 100% walikuwa wanamchukua. Haya yatakuwa ni maumivi makubwa sana
Hakuna shabiki hata mmoja wa Liverpool anayemjua Caicedo anakataa uwezo wake
Wengi wenye negativity wanasema Caicedo wewe ni mchezaji mzuri sana ila huko unakokwenda unakwenda kuua kipaji chako (sehemu ya maumivu ya kumkosa hayo) ila hakuna anayesema kuwa huyo anakuwa overrated kama hapa jamii forums.
Kwa hiyo kuna baadhi ya mashabiki wa Liverpool wanaumia kweli kweli
Mimi niliposikia dau la mil 111 ya liverpool siku hiypo ya alhamisi usiku na kwamba Brighton wameikubali na kwamba deadline ilikuwa imeisha saa nane usiku saa za Uingerea yaani niliumia nilianza kuugua ugonjwa wa ajabu ajabu hadi taarifa zilipoanza kujitokeza asubuhi kuwa Chelsea wamekataa kushindwa, baadaye taarifa za SkySports na vyanzo vingine vinajitokeza na habari ziliosema Caicedo ana maoni tofauti na hilo dau la Liverpool na baadaye baada ya mchana ijumaa hiyo hiyo anajitokeza kijana wetu, mweusi mwenzetu Moises mwana wa Caicedo kupitia Fabrizio Romano anasema Caicedo ameiambia Liverpool kuwa yeye anataka kwenda kuichezea klabu ya Chelsea tu. Hapo ndipo ugonjwa wangu wa ajabu ajabu uliokuwa unaninyemelea kwa kumkosa Caicedo ukaanza kutulia na furaha ikaipoteza huo ugonjwa kabisa.
Sasa mimi nilivyojisikia maumivu kihivyo kwa kumkosa tu Caicedo nawaza na hao Liverpool ambao kweli DMs zao zote hakuna ni uozo mtupu, Caicedo alikuwa aende akatatue huo uozo halafu wameweka dau kubwa la kihistoria halafu tena anajitokeza mhusika mwenye anasema haitaki Liverpool. inauma sana. Mbaya zaidi anajitokeza tena tumaini pekee lililobaki kwa Lavia naye anasema anataka kwenda Chelsea tu, ni kama ameshindilia msumari penye kidonda cha Caicedo. Wewe ungekuwa wewe maumivu ni kiasigani
Tumsamehe tu atukane hadi nyongo yake mbaya iishe ili apone. Akipona naamini atakuja kuomba msmaha