Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Ntuzu nashukuru kwa taarifa,
arsenal leo wametoa suluhu, sasa tupo kwenye nafasi nzuri ya kuendelea kupanda juu, maana naona arsenal ameamua kutuachia njia kabla hajakutana na man u anayoiogopa kwa kuuziwa matta


tunahitaji kushinda leo vs WEST HAM ili ARSENAL ikamate #3.

 
Huyo jamaa alizaliwa Accra Ghana, akaitwa Odenke Abbey; lakini mama yake alipoolewa na Mwanamume Mfaransa; basi kijana akapewa jina la Kifaransa; MARCEL DASAILLY. Huyo alikuwa kapteni kabla ya ukapteni hajapewa kijana wetu JOHN TERRY. Ikumbukwe kwamba John Terry amekuwa Chelsesa tangu akiwa na umri wa miaka 14. Alianza kuchezea timu wa "wakubwa" mwaka 2000, wakati huo alikuwa na umri wa miaka 19. Kwa sasa JT ana umri wa miaka 33(hakuna kufoji cheti hapo). Ingawa Chelsea imewahi kuwa na mabeki wazuri kama vile Alex, Ben Haim, Gallas, Frank Lebouf, etc, hakujawahi kuwepo beki bora wa kati kumzidi John Terry; Tulipocheza na Manchester United; John Terry alitimiza mechi 600 akiwa mchezaji wa Chelsea.
Hakujawahi kuwa na kapteni mwenye mafanikio kuzidi John Terry; anayemfuata ni Dennis Wise.
article-2547611-007AF4FB00000258-835_634x529.jpg


Remember this guy???
 
agosti 8 na nkwela Ntuzu, asanteni kwa maelezo yenu yakinifu...!!!

KTBFFH leo ushindi ni given, ninalia tu na idadi ya magoli..naona kama itatucost mwisho wa msimu yani!!!!
 
Last edited by a moderator:
agosti 8 na nkwela Ntuzu, asanteni kwa maelezo yenu yakinifu...!!!

KTBFFH leo ushindi ni given, ninalia tu na idadi ya magoli..naona kama itatucost mwisho wa msimu yani!!!!

Mkuu Mentor tunachukua ubingwa kwa wingi Wa point sio magoli! Ondoa Shaka kabisa kwa Hilo!

Ata wakifunga dazeni za magoli sisi tunataka point tu!


Na Leo kushinda ni Lazima!
 
Last edited by a moderator:
agosti 8 na nkwela Ntuzu, asanteni kwa maelezo yenu yakinifu...!!!

KTBFFH leo ushindi ni given, ninalia tu na idadi ya magoli..naona kama itatucost mwisho wa msimu yani!!!!


Ni kweli, lakini Arsenal wametuzidi goli 1 tu. Cha maana siyo magoli ambayo timu inafunga; ila pia magoli ambayo timu inaruhusu yaingie golini kwake; Sisi tumeimarika sana kwenye ulinzi kwa sasa.
Leo tukishinda 3-0 itakuwa poa sana;
 
Kwenye fainali ya Word Cup vs Brazil 1998. Marcel alipewa kadi nyekundu kipindi cha pili. Bebeto alikuwa anaelekea kwenye goli la Ufaransa kwa kasi ya ajabu(mtakumbuka Bebeto alikuwa na umbo dogo kama Oscar vile) lakini Marcel alienda akaweka miwili; Bebeto chali. Huyu alikuwa mtu wa kazi.
hii mutu hatare sana,moja kati ya mabeki shupavu!hv yuko wapi huyu?
 
Naona hapo mkuu wa kazi Claude Makelele anamfundisha mpira kijana Babel #19 wa Liverpool(mholanzi mwenye kipaji huyo, ila majirani walishindwa kumtumia ipasavyo) Makelele kiboko; mmesahau mjadala wa wiki iliyopita kuhusu viungo wa ukabaji?
article-2547512-01013C9000000578-334_634x435.jpg


Nimemfuma wakimuongelea mahali huyu jamaa...!!!

Cc: miss chagga
 
LEGENDS
3. CLAUDE MAKELELE:
Huyu mchezaji hajatokea kama yeye kabla na baada yake. Alikuwa anacheza mbele kidogo ya mabeki wa kati kama kiungo mkabaji.
Alisajiliwa kutoka Real Madrid msimu wa 2004.
Alikuwa anavaa #4.
Website ya Chelsea inasema hivi kuhusu Makelele; "The only Chelsea player to have had a position named after him."
Yaani jukumu alilokuwa nalo uwanjani hakuna mtu amewahi kuwa nalo kabla yake. Huyu jamaa alikuwa anakaba; Kushoto kwake Thiago #30, na Frank Lampard #8. Nyuma yake John Terry, Calvaho,Gallas na Paulo Ferreira.
Msimu huo tulicheza mechi zote za ligi (mechi 38) na kupata clean sheets 25.
Tulifungwa magoli 15 tu msimu mzima na tukawa mabingwa wa kihistoria kwa kufikisha points 95.
Tulifungwa magoli 6 tu msimu mzima kwenye uwanja wetu wa Stanford Bridge. Yote hayo kwa sababu huyo Jamaa Claude Makelele. Aliondoka mwaka 2008, akiwa mchezaji huru. Chelsea walimwacha aende huru kwa sababu ya heshimu aliyokuwa nayo kwenye timu.


Sitaki kusema mengi kumhusu Claude Makelele; maana nilishasema tayari; cheki hapo.
 
Claude Makelele "holding midfielder" = "The only Chelsea player to have had a position named after him."
 
Sitaki kusema mengi kumhusu Claude Makelele; maana nilishasema tayari; cheki hapo.

When it comes to Makelele, I wish I could turn back the time. Matic anaweza kukua na kusaidia sana Midfield yetu, nilicheck game na Stoke City alifanya vizuri sana, anaweza kuwa Makelele mdogo. Matic plays the ball before it gets to him, he is really cool
 
When it comes to Makelele, I wish I could turn back the time. Matic anaweza kukua na kusaidia sana Midfield yetu, nilicheck game na Stoke City alifanya vizuri sana, anaweza kuwa Makelele mdogo. Matic plays the ball before it gets to him, he is really cool


Zinedine Zidane alimwambia hivi tajiri wa Real Madrid alipomwondoa Makelele na kumleta David Beckham kwenye timu ya Madrid; "'Why put another layer of gold paint on the Bentley when you are losing the entire engine?''
 
Kwa hivyo Zidane alimaanisha kwamba Claude Makelele ndo "the entire engine" ya timu ya Real Madrid. Zidane alisikitika kumkosa Makelele kwenye timu.

Claude alisajiliwa Real Madrid akiwa na miaka 27. Alipokuwa anacheza Chelsea alikuwa na miaka 30 na kitu.
Huwezi kuzungumzia wachezaji wazuri kwa miaka 20 iliyopita ukose kutaja jina la Makelele; labda uwe mgeni na mpira wa miguu.
 
Zinedine Zidane alimwambia hivi tajiri wa Real Madrid alipomwondoa Makelele na kumleta David Beckham kwenye timu ya Madrid; "’Why put another layer of gold paint on the Bentley when you are losing the entire engine?’’

They really lost an engine, they actually never recovered the loss. They tried with Diarra and so many more but no one got to that level, even Khedira is far from Makelele's midfield performance
 
They really lost an engine, they actually never recovered the loss. They tried with Diarra and so many more but no one got to that level, even Khedira is far from Makelele's midfield performance


Ni kweli Mkuu!

Ata timu ya taifa ya France bado hawajapata mtu Km Huyu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom