Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Axel na BAdiashile walikuwa wakicheza pamoja Monaco na sasa wanakuja kuendeleza hiyo Chemistry Chelsea
1690782742862.png
 
Elye Wahi katika mechi 53 kahusika na magoli 40 (magoli 32 na assists 8)
Alikuwa apelekwe mkopo lakini sasa Pochettino anamtaka aje kushindania Ustriker na Nicolas Jackson
Hii itakuwa business nzuri sana

Kumbuka ktk historia ya Chelsea mara nyingi tumewaajiri mastriker wazoefu na wa bei mbaya ndio waliotuangusha
Nadhani hawa wa bei chee na bado wachnaga kama akina Drogba hawatatuangusha kabisa
1690782933820.png
 
Hii timu sasa ni bora tu ibadilishwe jina iitwe Chukwuchukwu Fc.
Pundamilia FC sijui kwanini hatuanzi ligi na nyinyi.

Ila mutapata salamu zetu kwa yale makuku yenye mdondo.

Tutayapiga left, right and centre.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] kuna jamaa kanifurahisha sana, anasema kwa sasa hivi mtu yoyote mwenye dreads tajiri miluzi akimuona tu fasta anampa mkataba.
We subiri siku 13 zijazo uone hao marasta wanavyopeleka moto.
 
Linda Caicedo ni binti wa Kikolombia anayeichezea Real Madrid wanawake na timu yake ya Taifa kule Sydne kwenye mashindano ya Dunia ya Wanawake
Kwa nini nimeleta taarifa yake hapa

Huyu binti siku mbili kabla ya mechi yao na Ujerumani alianguka akazimia sec 90 na kupelekwa hospitalini. Wataalamu walijua hataichezea tena timu yake ya Colombia
Huyu binti akiwa na miak 14 tu aliingizwa kuichezea timu ya wakubwa na alipofikisha miaka 15 akagunduliwa na saratani ya mfuko wa uzazi yaani Ovarian Cancer
Sasa jana aliwafunga Ujerumani goli la akili sana wakati juzi yake tu alidondoka na kuzimia na kupelekwa hospitalini. Kama Mungu akimjalia maisha mema atakuja kuwa bonge la mchezaji wa kike Duniani na ningetamani Chelsea wangeanza kumnyemelea sasa

1690788747953.png
 
Caicedo ni type ya Kante kwa uchezaji wake
  1. Anajua kufanya clean tackle hata kama ni za hatari
  2. Anajua kufanya ball recoveries ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya shambulio la haraka na kujenga mashambulizi ya kawaida
  3. Anajua kuusoma mchezo na kujua mashambulizi ya hatari yanajengwa kuelekea upande gani na kwa hiyo anakuwepo maeneo hayo kuzuia au kufanya clearance muhimu kabisa
  4. Pia anayo stamina na nguvu kama ya Kante ya kuwepo kila eneo la kati kumaliza kazi ya kukata umeme
Kwenye soko sasa mchezaji kama huyo hayupo, tutajisumbua, tutajidanganya na kupoteza muda sana
Tukimpata Caicedo atawezesha timu kupata utulivu pale katikati ya uwanja na kuwawezesha mabeki kucheza kwa utulivu. Pia atawawezesha final third ya timu pinzani kuwa busy na hivyo kuwezesha washambuliaji kutupatia mabao na ushindi kirahisi
View attachment 2701800
Tukiwaambia huyu Caicedo ni staili ya Kante (Kante v2.0) wengine hawatuamini, mkata UMEME. Ebu cheki hapa
anavyofanya tackle za maajabu. Aisee tumnunue hata kwa pauni mil 100 wanazotaka Brighton
 
Sura ya Chalobah yabadilika baada ya usajili wa Axel Disasi
Alikuwa na ujasiri na kujiaminiu kabla ila sasa kanyong'onyea na anataka kuhama kwa sababu anajua hatapewa kipaumbele kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea msimu ujao
Anafikiriwa ndani ya Chelsea kuwa anauzika na sasa wamemwekea bei ya £45m
1690811742279.png
 
Mashabiki wanawashabgilia sasa hivi akina Axel Disasi na Lesley na wakasahau kuwa Bakayoko alitokea Monaco tena baada ya kufanya vizuri akiwa na akina Mbape na kuipa Monaco Ubingwa mbele ya PSG iliyosheheni vipaji na wachezaji wenye majina makubwa.
Mungu atusaidie tusije kuwa tumeuziwa Bakayoko kwa jina lingine
 
[emoji23][emoji23][emoji23] kuna jamaa kanifurahisha sana, anasema kwa sasa hivi mtu yoyote mwenye dreads tajiri miluzi akimuona tu fasta anampa mkataba.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sura ya Chalobah yabadilika baada ya usajili wa Axel Disasi
Alikuwa na ujasiri na kujiaminiu kabla ila sasa kanyong'onyea na anataka kuhama kwa sababu anajua hatapewa kipaumbele kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea msimu ujao
Anafikiriwa ndani ya Chelsea kuwa anauzika na sasa wamemwekea bei ya £45m
View attachment 2703849
Huyu jamaa na mirasta yake michafu auzwe tu haraka.
 
Pochettino hakutaka usajili wa Lesley Ugochukwu na ndio maana anapelekwa mkopo chap chap
Huo usajili haukuwa uchaguzi wake, yeye anamtaka Caicedo au wa Calibre yake sio Ugochukwu
 
Mashabiki wanawashabgilia sasa hivi akina Axel Disasi na Lesley na wakasahau kuwa Bakayoko alitokea Monaco tena baada ya kufanya vizuri akiwa na akina Mbape na kuipa Monaco Ubingwa mbele ya PSG iliyosheheni vipaji na wachezaji wenye majina makubwa.
Mungu atusaidie tusije kuwa tumeuziwa Bakayoko kwa jina lingine
Hakuna usajili mbovu uliowahi kutokea chelsea, kama usajili wa bakayoko
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom