Ni kwamba tu mashabiki wa chelses tushazoea kulalamikia makocha, lakini safari hii tatizo ni kwamba tuna wachezaji wasio na calibre ya kucheza chelsea.
Embu angali goli tulilofungwa, azpilicueta anaona kabisa forward yuko mbele yake baada ya thiago kufanya makosa ila akabaki anamuangalia tu mpaka alipopewa pasi ndo akajifanya anaenda kumkaba. Goli lilikua linazuilika kabisa yani lile.
Tuje kwa ziyech, kusema kweli huyu jamaa tusiwe na matumaini kwamba atakuja kuperfom ndani ya uzi wa chelsea. Amekua kila akicheza hasahas msimu huu ndiye anaongoza kwa kupoteza mipira na kukosa nafasi, hovyo kabisa.
Pulisic ndo zero kabisa, akiingia kama vile hatupo uwanjani.
Naonaga wengi mnamsema Jorginho, lakini ukweli ni kwamba Jorginho ni mchezaji bora kushinda wengi mno ndani ya kikosi cha chelsea.
Bila usajili wa maana tutakua kama Man U, kulalamikia makocha kila siku kumbe tuna wachezaji wapumbavu.