Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Nadhan umesahau msimu ule wa Mourinho, 2015/16
December mourinho anafukuzwa.
Tulimaliza wa 10 na Yeye alifukuzwa nadhani tukiwa wa point moja nyuma ya relagation zone. Mechi tisa tulifungwa kati ya 16 tulizocheza.
"Mourinho had been under increasing pressure as their worst start to a season since 1978 began to form, with defeats to Manchester City and Crystal Palace in August, Everton in September, Southampton, West Ham and Liverpool in October, Stoke in November, and Bournemouth and Leicester in December 2015"

Maneno ya Emenalo akihijiwa na TV ya Chelsea kuhusu kufukuzwa kazi MOU
“There obviously seemed to be a palpable discord between manager and players and we feel it was time to act.
The owner is forced to make what was a very tough decision for the good of the club. We are one point above relegation and that’s not good enough. Any fan can understand this club is in trouble and something needed to be done.”

Emenalo alitofautiana na laumu ya MOU kuhusu wachezaji kumtosa majini kwa kudai hawa hawa wachezaji ndio walioleta ubingwa msimu uliopita kwa kusota na kutokwa na jasho na machozi juu kwa kufuata kila agizo walilopewa na kocha. Kwa hiyo alidai huu sio muda wa kuwalaumu wachezaji.

"Emenalo appeared to absolve Mourinho’s players of blame and laid it squarely at the feet of the manager. “This is the same group of players who won the league and the League Cup last season, they did it by sweating tears and blood. They played to instruction, they adhered to everything the manager asked them to do. It’s very easy to make that kind of inference [about the players] but it’s not one that club accepts."

Na nadhani ujumbe mkuu wa MOU ilikuwa "Betrayal"
Wachezaji watatu walimuuza kwa kuwasema vibaya kwenye media
  1. Hazard (msimu uliopita 14 goals and 9 assists)
  2. Diego Costa (20+ goals msimu uliopita)
  3. Fabregas (18 assists msimu uliopita
Hao wote walikuwa ni wachezaji muhimu wakagoma kutoa matokeo waliyoonyesha msimu uliopita
Hazard kipekee alisikika akisema waziwazi hawezi kumfungia magoli huyo bwege. Tatizo kubwa ni kwamba MOU alimuita mtoto na hajitumi.
Ndio maana naogoma sana anachokifanya TT kuwasema wachezaji kwenye media italeta mgomo baridi kama walivyofanya hiyo 2015

Dalili ya kwanza ya MOU kufukuzwa ilikuwa ni kushindwa mechi zote za Pre season kitu ambacho naye TT kafeli!! na nina wasiwasi hiki kitu kinaweza kujirudia msimu huu labda kitakachomuokoa ni uhamisho wa mwaka huu kuleta sura nyingi na sura nyingi pia kuondoka, inaweza ikapooza vuguvugu la kumgomea kocha kwa kucheza mchezo uliopooza kama wakati wa MOU
 
Mbona kama Bakayoko hivi?
Tunabet kwenye mfumo wa TT labda atafit in, hatukuwa na option
Alicheza vizuri sana akiwa Bundesliga, mambo yake hayakwenda vizuri alipohamia Juventus dirisha dogo la January 2022
 
1662097701507.png
 
Line up 2022/23
343
A
----Sterling ------------- Auba ------------- Ziyech----

Cucurella --------- Denis ----------Kante ----------James

----- Koulibally --------- Silva ----------- Fofana --------

------------------------ Mendy -------------------------

B

----Sterling ------------- Auba ------------- Mount----

Chilwell ---------Kovacic----------Denis ----------James

----- Cucurella --------- Silva ----------- Fofana --------

Tutaanzia hapo, timu imepanuka kidogo ila kwa ajili ya top 4 sio ubingwa don't misquote me
 
Nichukue nafasi hii kumpongeza Tajiri wetu Boehly kiukweli amefanya kazi kubwa Sana kwenye Hili dirisha ametuprove wrong wapenzi wengi wa chelseafc dirisha la kwanza tu ametumia kiasi kikubwa Cha fedha kwenye usajili nadhani kuliko Tajiri wowote wa Teams za Ulaya na kikubwa zaidi amezingatia mahitaji ya kocha hata pale ambapo kuna wachezaji alikuwa anawataka binafsi kama Ronaldo lakini kwazingatia Mapendezo ya TT ameamua asimsajili tu kwasababu TT amemkataa.

Kutokana na usajili Huu uliofanyika TT ana deni kubwa kwa mashabiki kwasababu kapewa kila kitu na Wamiliki hana excuses zozote zaidi ya kuona tunapata matokeo yenye kutupa makombe.Kazi imebaki kwake tuone nini atafanya na hamu kubwa leo nini ataongea kwenye press conference atakayoifanya jioni ya leo baada ya dirisha kufungwa.
 
Usisahau zile silaha za academy, viungo wale watatu, beki, golkipa na ule wa dinamo ambaye nadhani atakuja januari. Usisahau akina Levi Colwill. asipoweka plan ya kuwaingiza kwenye first team kama anavyofanya Xavi kwa Gavi na Ansupati wa Barcelona, nakuapia atafukuzwa kweupe. Nasema hivi kwa sababu naona maono waziwazi ya Boehly ni kuunda kikosi imara ya sasa na ya baadaye. Na hii inaonyesha waziwazi Todd Boehly anahitaji kocha wa kufit kwenye maono hayo
ningekuwa ni mimi hao watoto kwa rotation wangetumika sana kwenye mechi za mwanzoni mwa karabao na FA sio wote kwa pamoja ila mmoja mmoja ili kuwajengea confidence na baadaye waweze kucheza first team

Gavi an miaka 18 tu na Ansupati miaka 19 na wote wameshakuwa regular starters wa Barca. Wamekuwa hivyo baada ya kuaminiwa na kocha na kuingizwa kidogo kidogo hadi with short period wakawa regular starter
Chukwuemeka anafikisha 19 October 2022 na ana composure sawa na Gavi ila unaweza kusota development team hadi anakosa hamu ya kubaki Chelsea
Casadei ana miak 19 naye ni mzuri ila uzuri wake utadumu akicheza mechi kubwa, sio development team tu
Omari Hutchinson anye miaka 19 October, kiungo mshambuliaji mzuri
Levi Colwill miaka 19 na ameonyesha kuwa anaweza japo ni kwenye ligi ndogo ila angepewa hata minutes chache tu
Hawa wachezaji wote wanne wakipewa muda mdogo mdogo hadi 2023/24 hata kama sio wote unaweza shangaa watatu kati yao wakawa wachezaji muhimu sana Chelsea na kuokoa mamilioni ya dola ya kusajili wazoefu kutoka nje
 
Mbona kama Bakayoko hivi?
Alikuwa mzuri sana wakat yupo Borussia Monchengladbach,
Juve amehamia + majeruhi yakawa yanamuandama,

Form ya juve isiwachanganye sana maana usajili ni 50/50, kuna player wakat wako juve walionekana wabovu Bentaccur n Kulivesky ila sahiv spurs wako vizur

Ngoja tuone hali itakavyokuwa.
 
Line up 2022/23
343
A
----Sterling ------------- Auba ------------- Ziyech----

Cucurella --------- Denis ----------Kante ----------James

----- Koulibally --------- Silva ----------- Fofana --------

------------------------ Mendy -------------------------

B

----Sterling ------------- Auba ------------- Mount----

Chilwell ---------Kovacic----------Denis ----------James

----- Cucurella --------- Silva ----------- Fofana --------

------------------------ Mendy -------------------------

Tutaanzia hapo, timu imepanuka kidogo ila kwa ajili ya top 4 sio ubingwa don't misquote me
Ningependelea
Sterling Auba Ziyech
au
Pulisic Auba Sterling

in case Sterling akipumzishwa
Pulisic Auba Ziyech
 
Alikuwa mzuri sana wakat yupo Borussia Monchengladbach,
Juve amehamia + majeruhi yakawa yanamuandama,

Form ya juve isiwachanganye sana maana usajili ni 50/50, kuna player wakat wako juve walionekana wabovu Bentaccur n Kulivesky ila sahiv spurs wako vizur

Ngoja tuone hali itakavyokuwa.
Kuna game hapo hapo juve walicheza dhidi ya Real Madrid UEFA jamaa alikiwasha sana alikaba mno hii game
 
Nichukue nafasi hii kumpongeza Tajiri wetu Boehly kiukweli amefanya kazi kubwa Sana kwenye Hili dirisha ametuprove wrong wapenzi wengi wa chelseafc dirisha la kwanza tu ametumia kiasi kikubwa Cha fedha kwenye usajili nadhani kuliko Tajiri wowote wa Teams za Ulaya na kikubwa zaidi amezingatia mahitaji ya kocha hata pale ambapo kuna wachezaji alikuwa anawataka binafsi kama Ronaldo lakini kwazingatia Mapendezo ya TT ameamua asimsajili tu kwasababu TT amemkataa.

Kutokana na usajili Huu uliofanyika TT ana deni kubwa kwa mashabiki kwasababu kapewa kila kitu na Wamiliki hana excuses zozote zaidi ya kuona tunapata matokeo yenye kutupa makombe.Kazi imebaki kwake tuone nini atafanya na hamu kubwa leo nini ataongea kwenye press conference atakayoifanya jioni ya leo baada ya dirisha kufungwa.
Now Pressure iko kwa Tuchel,
6 new signing ambao wote or 5 wanaingia kwenye kikos moja kwa moja.

Now Boehly-Clearlake wafocus kwenye kutafuta new DOF,
 
Wote wanaingia first team
Koulibally
Sterling
Cucurella
Fofana
Aubameyang
Denis Zacharia

Wengi permanent, wengine rotation labda form Yao ikiacha kutick hasa ya Denis
 
Nichukue nafasi hii kumpongeza Tajiri wetu Boehly kiukweli amefanya kazi kubwa Sana kwenye Hili dirisha ametuprove wrong wapenzi wengi wa chelseafc dirisha la kwanza tu ametumia kiasi kikubwa Cha fedha kwenye usajili nadhani kuliko Tajiri wowote wa Teams za Ulaya na kikubwa zaidi amezingatia mahitaji ya kocha hata pale ambapo kuna wachezaji alikuwa anawataka binafsi kama Ronaldo lakini kwazingatia Mapendezo ya TT ameamua asimsajili tu kwasababu TT amemkataa.

Kutokana na usajili Huu uliofanyika TT ana deni kubwa kwa mashabiki kwasababu kapewa kila kitu na Wamiliki hana excuses zozote zaidi ya kuona tunapata matokeo yenye kutupa makombe.Kazi imebaki kwake tuone nini atafanya na hamu kubwa leo nini ataongea kwenye press conference atakayoifanya jioni ya leo baada ya dirisha kufungwa.
Ashindwe mwenyewe kapewa yote anayotaka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom