Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Ukweli ni kwamba tupo kwenye kundi la kushindania ubingwa la EPL... Timu yoyote ukipata majeruhi Kama tulivyopata msimu uliopita lazima watumbe tu.

Hivi pale Madrid Kuna wachezaji gani wa maana ukilinganisha na Chelsea? Still walichukua makombe...ni muda wa kocha kutumia rasilimali zilizopo na kushinda makombe, tumeingia fainali mbili msimu uliopita na tukatolewa kwenye penalty na tukafika hatua nzuri zaidi UCL msimu uliopita.

Tuseme ukweli, Chelsea bado ni timu yenye kikosi kizuri miongoni kwa timu barani ulaya, hizo timu za Liverpool na Man City wakipata majeruhi kwa key players wanne Kama tulivyopata msimu uliopita mtashangaa sana.

Tunaposema tufanye usajili, je wachezaji wa maana wanaowazidi tulionao wako wapi sokoni? au tunawaleta wachezaji ili wazoee ligi kwa misimu miwili then tunaowatoa nao wanakwenda kufanya vizuri huko waendako?

Tukubali tu, kama Chelsea wanataka kufanya vizuri inabidi kumpatia Kocha muda wa kutosha lakini siyo kununua tu wachezaji kisa timu zingine wananunua.
Chelsea ndiyo timu Ulaya wanaopeleka wachezaji wengi kwa mkopo, je tumeshajiuliza ni kwanini?
Ndg timu ambayo wachezaji hawatoki wala hawaingia, kuna siku watakuwa wanacheza business as usual. Kupangua timu na kuingiza sura mpya ni one of the best strategy ya kucheza vizuri hata kama wanaoondolewa ni wazuri.

Factor nyingi zinasababisha mchezaji aondolewe apelekwe mkopo au auzwe na baadhi ya hizo factors hizi hapa
  1. Mchezaji anataka kuondoka
  2. Kukaa muda mrefu kwenye timu na hana jipya la kuipa timu
  3. Kuflop labda haendaniu na mfumo wa kocha au haendani na ligi au haja fit in kwa wenzake yaani hana chemistry nzuri
  4. Ana tabia ambazo sasa haziendaniu na kinachotakiwa kwenye dressing room au uwanjani
  5. Timu inafanya mchakato wa kubana matumizi kwa sababu za hali mbaya ya kiuchumi, kuwatoa wachezaji wenye mishahara mikubwa ili kuingiza wapya wazuri watakaoanza na mishahara midogo (Mfano mesi katoka Barca kwa sababu ya mshahara mkubwa, De Jong wanamlazimisha apunguze mshahara au auzwe ili timu iweze kubalance mahesabu yake)
Pia Kocha naye anaweza kuondolewa iwapo
  1. Yeye mwenyewe anataka kuondoka
  2. Hawezi tena kutoa matokeo mazuri na kufukia malengo ya timu
  3. Hana maelewano mazuri na key players
  4. Hana maelewano mazuri na managementi ya timu
  5. Timu ina malengo mapya na inahitaji kocha mpya nayeendana na hayo malengo mapya (mfano timu ilipouzwa kwa Abramovich 2004 Ranieri ilibidi aondolewe aletwe Mounrinho)
  6. Ziko sababu nyingi zaidi
Ukweli ni huu afya ay timu iko kwenye kila wakati wachezaji wapya waingie na wengine wasiofaa waondoke. Ligi ya EPL kwa timu kubwa zenye malengo ya kushinda makombe makubwa haina muda wa kumsubiri kocha au mchezaji azoee, kama huwezi kuleta matokeo ya haraka inabidi kupart ways
 
Sio tu billy pekee kuna huyu Lewis Hall ndio ananiuma Sana sijajua huyu dogo ni raia wa nchi ni fundi Sana technically gifted anajua kupiga pass, yupo vizuri kwenye ukabaji na anauwezo wakucheza nafasi tofauti kama CAM na Wing back na Left back lakini chakushangaa hakuna hata mechi Moja ya preseason aliyopewa TT sijui anashida na hawa makinda hivi huyu dogo akampata mtu kama klopp au Guardiola tutaanza kulia lia
TT kuna wakati mie nahis kma wa michongo hiv
 
Development squad siyo ya watoto, ni squad ambayo wachezaji wanaotarajiwa kuingizwa kwenye fisrt team wanapitia kutokea academy hadi vijana wa 23 yrs wako pale pia wachezaji wanaotokea majeruhi kama bado hawapo fit kocha anaweza kuwapeleka huko ili wainue fitness yao kwanza. Swali je Gilmour hakuwa na fitness ya kutosha hadi apelekwe huko? au ni ile sababu aliyosema TT kuwa alitaka squad ndogo ili quality ionekane ya mazoezi hata hjivyo tukaishia kufungwa mfululizo

TT akiboa huwa naboa kweli kweli, inawezekana kabisa wachezaji wanaoogopa kuja Chelsea hawana imani kwa TT jinsi anavyowatreat baadhi ya wachezaji. Mawazo yangu tu!
Uko sahihi kabisa nahis nae TT Anachangiwa nahis mie natamani nae aondoke maana kuna wakati vigumu sana kumuelewa
 
Mkuu tim nzima haiwez jaa academy,
Angalia city or Liverpool wanaaacademy wangap kwenye vikosi vyao?

Kwa nafasi anayicheza wako watu gani? Kuna age unaweza kuwa unatumika upande wa academy ikitokea game za carabao or fa against tim ndogo kama za league 1 huenda akacheza ila kupewa nafasi tusidanganyane hapa .
Mbona tuliwapa nafasi mount, Abraham, James tumemuuza Tomori kwa kwa mtazamo kama wako angalia nini kaenda kufanya AC Milan? Sasa hivi tunashida kubwa kwenye left back au left wing back ukimtoa Benchilwell akampa hiyo nafasi dogo lewis Hall mechi Moja dogo akachafua akawa man of the match baada ya hapo dogo hakupewa nafasi yoyote ile hii ndio point tunayozungumzia imekuaje kashindwa kumpa nafasi Tena alafu Cha ajabu anamganda sarr
 
Mbona tuliwapa nafasi mount, Abraham, James tumemuuza Tomori kwa kwa mtazamo kama wako angalia nini kaenda kufanya AC Milan? Sasa hivi tunashida kubwa kwenye left back au left wing back ukimtoa Benchilwell akampa hiyo nafasi dogo lewis Hall mechi Moja dogo akachafua akawa man of the match baada ya hapo dogo hakupewa nafasi yoyote ile hii ndio point tunayozungumzia imekuaje kashindwa kumpa nafasi Tena alafu Cha ajabu anamganda sarr
Hao wengi walipewa Kwa sababu hakuwa na alternative. Timu ilikuwa kwenye ban. Kuwapa academy wengi nafasi Kila msimu ni kuamua kujitoa kabisa kwenye makombe kama Arsenal. Wenga aliwapa academy nafasi wakasahau kama Kuna kushindania makombe. Tuwape nafasi mmoja au wawili Tena wanaoonyesha kustahili
 
Taarifa za wacheza kudakwa au kuondoka ni nyingi kuliko za wachezaji kusajiliwa
 
Mbona tuliwapa nafasi mount, Abraham, James tumemuuza Tomori kwa kwa mtazamo kama wako angalia nini kaenda kufanya AC Milan? Sasa hivi tunashida kubwa kwenye left back au left wing back ukimtoa Benchilwell akampa hiyo nafasi dogo lewis Hall mechi Moja dogo akachafua akawa man of the match baada ya hapo dogo hakupewa nafasi yoyote ile hii ndio point tunayozungumzia imekuaje kashindwa kumpa nafasi Tena alafu Cha ajabu anamganda sarr
Timing ya Marina ndio alipofail kwenye uuzaj wa wachezaj huku akishindwa ongeza mkataba rudiger n christensen

Je kwa uwezo alionyesha rudiger o christeansen unahis Tomori angeweza waweka bench??

Halaf Lewis Hall amecheza dhidi ya tim ya daraja la 1, sawa anaweza perform, je kunauhakika wowote anaweza waweka chilwell or Alonso njee

Still anamiaka 17, bado ananafas ya kutumika ndio maana stil yuko kwenye vikos vya vijana na hajatolewa kwa mkopo.
 
Report: Club unlikely to accept Chelsea's offer for goalscoring midfield talent

Chelsea have submitted their first offer for Inter Milan talent Cesare Casadei after an unsuccessful enquiry during talks for Romelu Lukaku’s loan deal.
 
Kumekucha. Haaland leo kakaribishwa Uingereza kwenye Community Shield. Tayari ameshafananishwa na Lukaku. Na inaonekana akipanic anapanic vizuri. Magazeti yakianza kumuandika hasi kwa kukosa magoli ya wazi, atapoteza uelekeo kama Torres alivyopoteza baada ya kujiunga Chelsea kwa £50m.
Screenshot_20220730-223755_Chrome.jpg
 
Toa batshuay hapo

Kwanza naskia anaondoka huenda wiki ijayo akasepa if taarifa nilizoziona ni za kweli.

Kuna tim 2 za premier league zinamtaka mojawapo ni Brighton
Hata Everton wanmtaka yeye na Barkley kwa mkopo
 
Kwa mechi ya leo nilivyoona, Haaland atasota sana labda PEP abadili uchezaji acheze kama klopp "Direct footbal"
Haaland anahitaji counter attack na direct football sio huu wa mabeki na viungo kupasia hadi mbele wanasinzia
Kwa falsafa hiyi hiyo Nunez ameingia muda mfupi akasababisha magoli mawili

Natamani TT naye angeweka mkazo kwenye mpira wa direct na counter, sideways na backwrads passes hazisaidii kitu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom