[emoji117] Unajua kuna mashabiki wenzangu mnafanya masihara kukosekana kwa Kante & Kovacic kikosini.
[emoji117] Hawa jamaa ni uti wa mgongo wa timu, hawa jamaa ni msingi wa ubora wa safu ya ulinzi na ushambuliaji.
[emoji117] Hawa jamaa wanatembea na mpira uwanjani sio mchezo, hakuna kiungo ya timu pinzani itapenda kukabiliana na Kante/Kovacic, kwani wameshikilia asilimia 70 ya kutoa clean sheet na asilimia 50 za kufunga magoli.
[emoji117] Kante/Kovacic wanakaba, wanaziba njia, wanapora mipira, wanashambulia kwa kasi ya hali ya juu.
[emoji117] Jog, Cheek & Saul sio Kante wala Kovacic, tutawalaumu sana, tutuwalaumu mabeki, tutawalaumu makipa lakini
[emoji117] Bila uwepo wa Kante/Kovacic, kiungo yetu inajeuka kituko, njia ya walanguzi, Jog anakuwa comfotable kumiliki mpira na kutuliza timu kama Kante anafanya kazi ya msingi ya kukaba na kupora mipira.
[emoji117] Zile clean sheet kwenye mechi 12 hazikuja bahati mbaya Kante/Kovacic walikuwa wanaulinda ule ukuta nyuma yao. Wanazima mashambulizi kabla hayajafika kwa mabeki.
[emoji117] Madirisha ya usajili yajayo kuna ulazima wa kumsajili kiungo mkata umeme wa kusaidiana na Kante na Kovacic. Usajili wa SAUL ulikuwa wa kukurupuka, hasaidii chochote kwenye hili janga la majeruhi.