Pale kwa mabingwa wa Tanzania (Simba Sports Club) wanachama na wadau wengi wa klabu hiyo kauli iliyopo midomoni mwao kwa sasa ni kwamba pengo la Luis Miquessone na Cletus Chota Chama bado halijazibika ndani ya klabu hiyo.
Hali hiyo imenifanya na mimi kuangalia kwa jicho la mbali sana kuhusu timu yetu ya Chelsea, na kugundua kuwa pengo la Cesc Fabregas na Eden Hazard pale Chelsea bado halijazibika.
Chelsea kwa sasa inakosa kiungo mshambuliaji (namba 10) halisi mwenye jicho la kupiga pasi za mwisho kwenda kwa mshambuliaji wa mwisho kama ilivyokuwa kwa Cesc Fabregas na pia inakosa mawinga wasumbufu wenye nguvu, akili na uwezo wa kufunga na kutoa pasi za mwisho kwenda kwa mshambuliaji kama ilivyokuwa kwa Eden Hazard, Pedro Rodriguez na Willian.
Romelu Lukaku kwa sasa anaonekana si lolote ndani ya Chelsea yote inatokana na kukosa watu wa kumlisha pasi za mwisho kama alivyokuwa Everton, Inter Milan na anavyokuwa kwenye timu yake ya Taifa.
Nina hakika kama sasa hivi pale Chelsea kungekuwepo Cesc Fabregas, Eden Hazard, Pedro Rodriguez na Willian bila shaka Romelu Lukaku angetupia nyavuni kila siku kama ilivyokuwa kwa Diego Costa.
Kwa pendekezo langu ningependa kwenye dirisha dogo bodi ifanye mchakato wa kumsajili kiungo namba 10 halisi mwenye jicho la kupiga pasi za mwisho,