Kuelekea msimu ujao kwa maono yangu hawa ndio wachezaji tunaopaswa kusajili, ili kutetea ubingwa wa UEFA na kufukuzia ubingwa wa elp.
Tukianza na Straika, Ivan Toney (25) kutoka Brentford, Pedro Goncalves (22) kutoka Sporting na Andre Silva (25) kutoka Frankfurt. Hao Straika ni hatari sana na wanabalaa sana, kama ww ni mpenzi na mfuatiliaji wa mpira wa miguu basi utakuwa unakubaliana na mm ama kufahamu moto wao. Sasa katika hao watatu tuchukue mmoja ama wawili. Hapo sijamtaja Haaland maana usajili wake ni wa pesa ndefu sana.
Upande wa beki, Robert Atkinson (22) kutoka Oxford United, huyu dogo ata asipo pata nafasi ya kucheza lakin anafaa sana kusajiliwa ata kwa matumizi ya baadae. Dogo ni beki mzuri sana, tukimsajili huyu tunampelekea academy ili akapate uzoefu zaidi kisha atakuwa anapata nafasi moja moja kwenye timu kubwa. Jules Kounde (22) kutoka Sevilla, Achraf Hakimi (22) kutoka Inter na Alessandro Bastoni (22) kutoka Inter. Hizo beki ndio zinatufaa kabisa.
Kiungo mkabaji, Joshua Kimmich (26) kutoka Bayern Munchen, hapa bila kupepesa macho inabidi huyu mwamba tujilipue na tumsajili kama kweli tunataka ubingwa wa EPL na kutetea ubingwa wa UEFA. Uzuri wa Kimmich anacheza nafasi zaidi ya moja hivyo atatufaa sana hapa inabidi tujilipue kweli bila masikhara.
Hayo ndio maono yangu kuelekea msimu ujao, uchaguzi nilio ufanya kwanza nimelenga ubora kisha umri wa mchezaji.
NYUMBU na Ase8 ruksa kupeleka mapendekezo yangu kwenye bodi yenu maana nimewafanyia usikauti murua kabisa.
Papaa Gx.