Nani aliyakumbuka haya maandishi yangu kadri mchezo ulivyo kuwa ukiendelea mpaka ulipo malizika?
Waungwana mfahamu kuwa Mchezo wa leo ni fainali sio ligi na mchezo unachezwa mara moja tu kwa dakika tisini. Timu zote mbili Chelsea na Man City, wachezaji wote wa timu mbili yaani wachezaji wa Chelsea na Man City na makocha wote wawili Pep na TT wote hili kombe wanalihitaji sana. Niwambie tu timu zote mbili leo zitacheza kwa nidhamu kubwa mno, pia tusitalajie mchezo mzuri bali tutalajie mchezo mgumu sana. Timu zote mbili naona zikiingia kwa mfumo wa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza. Pep tayari ana onyo kutoka kwa TT hivyo hawezi kuja kijinga jinga tu, akija kijinga jinga tena atapokea za uso. TT nae anaelewa uzuri wa Man City na madhaifu ya safu yake ya ushambuliaji hivyo lazima leo atabadilika tu.

Mshindi wa leo atatokana na mbinu tu, na si ubora wa wachezaji. Mchezo wa leo ndio mtajua umuhimu wa kocha ama mwalimu katika mpira. Leo msitishwe na majina ya wachezaji kama KDB, Mahrez, Foden, Gundogan, Dias, Rudiger, Kante, Mount, Pulisic na wengineo wote. Hao wote na wengineo leo mtawakataa na kusema ndio hawa kweli, naam watakuwa wao na wala si wengine. Leo ni vita ya mbinu tu, leo ni ugomvi baina ya TT na Pep hao wachezaji wataingia uwanjani wakiwa kama wajumbe wa kufikisha hizo mbinu za walimu wao.

Msitarajie mechi kuanza kwa kasi, mechi itaanza kwa kila kocha kumsoma mwenzake yuko vipi ama amekuja vipi. Na kipindi cha kwanza kinaweza malizika kwa suluhu ya bila kufungana, kipindi cha pili kitabadilika kidogo tofauti na kipindi cha kwanza. Kama nilivyo sema huko juu leo timu zote mbili zitacheza kwa kujilinda sana, mchezo utabadilika baada ya timu moja kupata angalau goli moja.

Kwa uchache hayo ndio naona leo yakienda kutokea, karibu kwa masahihisho.
 
Ngolo Kante man of the match
Huenda akachukua Ballon d'or mwaka huu

championsleague-20210530-0001.jpg


chelseafc-20210530-0001.jpg
 
Back
Top Bottom