Mashuti ya ukuta hakuna kipa anayeona, wote wanabahatisha
Tofautisha shuti la open space na hilo uliloliweka linalozuiwa na Ukuta. Unaonyesha jinsi hujui mpira
Lete hapa reference ya kipa aliyewahi kudaka shuti ambalo aliyepiga alionyesha bado yuko kwenye move kudrift kushoto kisha akapiga shuti la kulia.
Mimi nakutajia magoli ya siku mbili nyuma yanayofanana na yenu.
1- Santi Mina anapokea pasi kutoka kushoto akiwa kwenye final third, Mina ni right footer, anatokea mchezaji anajaribu kuclose in kutokea kulia kwa Mina na mbele yupo Pique kumzuia asisogee mbele.
Na kwakua ni right footer anaonekana akijiandaa kushuti. Ter Stegen kwa kujua Mina ni right footer anajiandaa kuruka kushoto.
Pique kwa kujua Mina ni right footer anafanya body block ya kuelekea kushoto.
Mina shuti anapiga kushoto kwake (yaani kulia kwa Ter Stegen na kulia kwa Pique)
Ter Stegen hata hakuruka alibaki kasimama tu.
2- Gunter anapokea mpira wing ya kushoto anaambaa nao anaingia ndani ya ya box kutokea kwenye box huko huko kushoto. Neuer kwa kujua Gunter ni left footer anazidi kubana upande wake wa kulia.
Gunter anaachia shuti, na analipigia kushoto kwa Neuer ambaye alishajaa kulia.
Goli.
Xhaka kamfungaje Mendy? Xhaka ni left footer hivyo anaweza zaidi kucurve mpira na kuushuti comfortably kushoto (ambapo ni kulia kwa kipa) ndiyo maana Mendy akajaa upande ule in advance.
Xhaka alivyopiga kulia (Kushoto kwa Mendy) lazima iwe ngumu kuuzuia huo mpira.
Ili uelewe zaidi kama uliangalia ile nusu fainali first leg ya Barca na Liva, goli la faulo la Messi. Ukiachilia Liva kua hawajajiandaa ila uliona Messi alipopiga mpira? Sasa ule ndiyo upande ambao left footer anakua comfortable kupeleka mpira.
Cha mwisho kabisa: hili ni somo basic kwenye mpira, right footer atakua comfortable kumfunga kipa kwa kucurve mpira kwenda kushoto kwa kipa wazia mawinga au striker wa mguu wa kulia wanapocut in na kuscore kama Connolly wa Brighton, Pullisic nishamuona akifanya hivi, James wa United, Neymar au Auba wa Arsenal.
Left footer atakua comfortable kumfunga kipa kwa kucurve mpira kwenda kulia kwa kipa. Hapa unakutana na Sturridge, Salah, Pepe, Ziyech, Mahrez, Di Maria, Pogba alivyotumia left foot kufunga siku wanacheza na Fulham.
Kwahiyo Tielemans, right footer, yupo kwenye move anadrift kushoto Kepa anaenda na move na hata beki anajua huyu atakua comfortable kuleta mpira kushoto kwangu. Tielemans kapiga kulia beki kauzwa na Kepa kauzwa Mendy angefanya nini?
Mashabiki wa chelsea hua nawaita plastic kwa ishu ndogo kama hizi. Hizo ni basics za mpira.
Haya lete reference ya kipa aliyewahi kuzuia shuti kama hilo.