Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Ww ulie na nafasi kubwa mbona huendi? We nguruwe acha kuwa unaropoka ropoka tu
OK chukuen CL sasa ...


Chukueni FA ..

Team imejaa vilaza tuu ,hayajui mpira ..


Ni kulopoka tuuu , ..

Nishasema bado tunanafasi kubwa tu CL kama mnaona nyie mnastahili kuchukua CL nenden mkachukue hata saizi kenge nyie
 
Rudiger wakati wa Sarri na Lampard alikuwa hawezi wala hajui kupasi long balls au penetration pass. Alikuwa akipewa mpira na Luiz anamrudishia Luiz yeye ndie apige long ball au penetration pass
Ila baada ya TT kuja jamaa sasa anamzidi au amefikia kiwango cha Luiz kwenye pasi zile za hatari kama long ball na penantration pass
Congratulation Tony
 
Huko nyuma nilisha wahi kulalamikia kuwa Chelsea chini ya Lampard haitumii njia rahisi za kupata magoli kama City na Liverpool na timu zingine kubwa zinavyofanya
Hata kama unaposses mpira kwa asilimia 80% timu isipojua kucheza counter attack na au mara chache long balls timu haiwezi pata matokeo

Lampard yeye kama Sarri alisisitiza short passes tu hadi golini na ndio maana hata kitimu kidogo kikamua kuweka ukuta mzito Chelsea ilikuwa ngumu kufunga

Sas tangu TT aje, Chelsea imekuwa ni mwiba kwa timu zingine kwa counter attack. nimefuatilia hata Chelsea ikimiliki mpira 80%, ikipata mwanya wa kufanya counter inafanya na ndio maana akina ZIyech, Pulisic, Werner hata Havertz wamerudi kwenye ubora wao

Hata Kante anakuwa mzuri sana kwenda mbele kama timu inafanya counter attack
Magoli yote dhidi ya city tumepata kwa counter attack hata zile dhidi ya Real Madrid
Goli la first leg lilikuwa la long ball kutoka kwa Rudiger
Magoli ya second leg ni ya counter attack

Tukiendelea hivi, mwakani sisi mabingwa wa makombe mengi na tunae kocha mwenye kiu ya ushindi na makombe

Kila laheri The Blue darajani tarehe 12, Arsenal tutawaua kifo cha mwizi mpaka mashabiki wao wao wanasema shikamoo hata wakiona rangi ya bluu tu!
 
OK chukuen CL sasa ...


Chukueni FA ..

Team imejaa vilaza tuu ,hayajui mpira ..


Ni kulopoka tuuu , ..

Nishasema bado tunanafasi kubwa tu CL kama mnaona nyie mnastahili kuchukua CL nenden mkachukue hata saizi kenge nyie
Mkuu ushabiki haupo ivo. Ushabiki ni pale unapokubaliana na hali pamoja matokeo. Timu yako ikizidiwa tactic kubali then jiandae na mechi inayofata[emoji23].

Ushabiki siyo kupanic na kutoa matusi pale unapotaniwa na shabiki mwenzako.

Kubali kuwa Tuchel kawaibisha Mara mbili and get prepared for another game. Nani hayaogopi Chelsea sasa?
 
Huyu hawezi matani ya mpira Bora akae zake chini tu atulie[emoji3][emoji3]
Hakukaa miaka 30 kama Mashabiki wa Liverpool, kwa hiyo hana ukomavu wowote, Kaanza kuishabikia Man City juzi tu kipindi cha PEP
 
Ndio maana timu kubwa kama Chelsea inatakiwa kuwa na timu A na B zenye uwezo unaofanana, timu C ndio iwe ya Karabao cup NK
Kumbuka pia sio wachezaji wote wanaochoka, mimi naona kuanzia mabeki wa pembeni, viungo na washambuliaji ndio wanaochoka kwa sababu wanakuwa busy sana kila saa, Kipa na CB wanaweza wakawa walewale. Kwa hiyo TT anaweza kuwarotate wachezaji wanaoonekana wamechoka au kufululiza kucheza sana kama jana alivyofanya kwa Mount, Benchilwell, Havertz na Silva hata benchi hawakuwekwa
Kwa rotation hii timu inakuwa fresh kila mechi
Zimebaki za ligi tatu tu, hiyo ya Leicester city ni mechi ndogo kwa sababu LCFC hawana timu pana na wataingiza wacheza wamechoka na kuwa na confusion kubwa kwa sababu ya kutolewa top 4 na hivyo tutajipigia kirahisi tu. Mechi na City UCL wataingia wakiwa na hofu ya kufungwa mechi mbili mfululizo na sisi tutaingia tukiwa na confidence na uchu wa kunyanyua Ndoo kubwa yenye heshima Ulaya ambayo akina Bayern, Real Madrid, PSG na wao City wanaimezea mate
Mkuu huoni madhara ya over confidence? Over confidence husababisha ku-underrate opponent wako.
 
Naomba nitoe angalizo hapa kuhusu ile penalti ya Aguero
Aguero hakupiga ile penalti vibaya au kwa bahati mbaya, alipanga tena sio chini ya wiki kuwa akipata fursa ya kupiga penalti atatumia mtindo huo ili kuiaga Man City kwa mbwembwe za staili ile.
Wachambuzi wengi wa mpira akiwemo Michael Owen amesisitiza kuwa ile penalti ilipigwa vizuri japo yeye Owen hakuipenda ile penalti na angekuwa yeye ndie mpigaji asingepiga penalti kama ile

Kuna staili kama tatu za za kupiga penalti

  1. Kuna penalti ya kumhadaa kipa na kupiga upande tofauti, hizi huwa haitumii nguvu nyingi - mfano zile penalti za Jorginho
  2. Kuna penalti za kupipiga shuti la nguvu ili hata kipa akiifuata asiweze kudaka - Kane anatumiaga sana hii
  3. Kuna penalti za kutumia staili namba 1 na 2 kwa pamoja
Sasa jana Aguero yeyealiamua kutumia staili ile ya kwanza kwa kuuchupa mpira kwa kitaalamu inaitwa "Panenka Penalty" inaitwa pia Spoon style yaani penalti ya kijiko akitegemea Mendy angedive ila Mendy alisita kudive na ndio maana akaudaka kwa urahisi tena kwa mkono mmoja wa kushoto ili kuonyesha madharau kwa sababu mtindo kama huu huwa ni mtindo wenye lengo la kumzalilisha kipa. Makipa wanaujua huo mtindo na Mendy alihisi Aguero angeutumia huo mfumo ambao kihistoria umetumiwa na Legend wa Man City aitwaye Billy Meredith miaka 70 kabla ya Antonio Panenka kuutumia katika mashindano ya UEFA ya mwaka 1976.

Maelezo zaidi nimeweka hapo chini

Tafsiri ya hiyo Penalti


Panenka is a technique used while taking a penalty kick in which the taker, instead of kicking the ball to the left or right of the goalkeeper, gives a light touch underneath the ball, causing it to rise and fall within the centre of the goal, deceiving the goalkeeper who is counted on by the taker to have guessed a side and committed a dive away from the centre. It was first believed to have been used by Czech player Antonín Panenka, who introduced this technique to the world in the 1976 UEFA European Championship final, when he beat West German goalkeeper Sepp Maier to claim the title for the Czechoslovakian national team.

Kwa amneno ahya hata ile Twitter ya Aguero ya kuomba msamaha isingestahili ndio maana hata PEP alipoulizwa kuhusu hiyo penalti ya Aguero alisema ni maamuzi yake hakuseme kwa maneno mengi. Akijua kuwa Aguero alifanyia hadi mazoezi ya kupiga penalti kama ile
Kwa ufupi au kuhitimisha, mfumo wa kumhadaa kipa yaani mtindo ule namba moja una riski nyingi na sio mtindo mzuri wa kupiga penalty na ni mfumo wenye lawama nyingi kama penalti imekataa
Kwa hiyo kiufupi ni kwamba Mendy ana akili sana kwenye nafasi yake!
 
Mkuu huoni madhara ya over confidence? Over confidence husababisha ku-underrate opponent wako.
Hakuna mtu aliyetaja over confidence ila wewe pekee yako, Confidence inatakiwa ili ushinde ila sio over-confidence hiyo ni yako ndugu
 
Hakuna mtu aliyetaja over confidence ila wewe pekee yako, Confidence inatakiwa ili ushinde ila sio over-confidence hiyo ni yako ndugu
Sasa mtu anaposema makombe ya FA na UCL yanakuja darajani ni aina gani ya confidence hiyo? Jambo la msingi ni kwamba kocha na wachezaji wa ze bluz wanajitambua na wanaelewa bado kuna kazi kubwa mbele.
 
BREAKING NEWS
Timu ya Wanawake yawa mabingwa kwa mara ya nne
Timu hiyo kwa sasa inashikilia makombe 9 ya ndani katika miak 10 iliyopita, ikishinda FA ya wanawake ambayo bado inaendelea itakuwa na makombe 10

HONGERENI THE BLUES
WANAWAKE TUMENYANYUA NDOO TAYARI HUKO KWENYE WOMEN SUPPER LEAGUE BAADA YA KUWACHABANGA READING BAO 5-0
BADO UEFA NA BARCELONA
1620583568900.png

1620585599975.png
 
BREAKING NEWS

UEFA final inaweza kuhamishiwa katika mji wa London
Hii ni kutokana na kwamba Uturuki imeingizwa na serikali ya Uingereza kwenye red list na kwa hiyo itaadhiri mapato ya uwanjani
Serikali ya Uingereza imeiruhusu UEFA kufanyia fainali hizo katika mji wa London.
SkySports wanaripoti kuwa Serikali ya Uingereza na Uongozi wa UEFA watakuwa na mazungumzo jtatu ili kuona kama hayo mashindano yanaweza kuhamishiwa ktk mji wa London
1620585765448.png


WAWALETE TUWACHINJE KABISA NYUMBANI

Mashabiki wa city wameanza kulalamika sana, wanadai kwa nini isiwe Villa Park ambayo iko katikati ya London na Manchester
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom