Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Mimi nilipenda Lampard angevumiliwa hadi mwisho wa msimu na kama katupa top 4 au UEFA apewe msimu mwingine ili azoee EPL ila pia FL kufukuzwa ilikuwa ni lazima, kocha ukishaingia kwenye mgogoro na wachezaji usio na tija na timu hakuna njia nyingine ni sacking tu.
Mkuu lembu uko upande gani? Kwani ofsa lampad atapata timu nyingine we utamfata Tuchel muache nae afundishe anachoweza
 
Marina ni mnafiki, yeye ndio kamfukuzisha Lampard na pia yeye ndie anayeiua Chelsea kwa kutuletea mkorogo ndani ya timu
Akina Drinkwater, Kepa yeye ndie kawaleta bila ya kuwasikiliza makocha
Conte alikataa kukorogwa ndio akasepa, Sarri aliona hapa hakuna future akasepa
Sasa mtoto wa nyumbani Lampard kafukuzwa hata ajamaliza kunyonya maziwa
 
Mkuu ulipotea mazima ni Lampard kakupoteza nini?
Mkuu nilipata changamoto ya simu tar 28/12 na hata niliporudi nikaona ngoja nijiweke pembeni. Ila tuko pamoja nawafuatilia chini chini kwa sasa comments zitakua chache maana majukumu yanabana kwa sasa.

Lakini pia hii fukuza ya makocha inanikera sana yan hatuwezi kumpa kocha muda ajenge timu ya ushindani walau tuwe top level kwa misimu walau minne hii kitu nayo inakera sana.

All in all mimi naamini Tuchel ni mtu sahihi kwa sababu kafanikiwa PSG, Dortmund na Mainz hata Chelsea pia atafanikiwa kwa aina ya wachezaji tulionao coz ana experience ya ku manage majina makubwa. Namuona mbali sana Tuchel kama sisi fan we will hold our breath at mostly tough times.

KTBFFH
 
Of course Arizabalaga will be our first choice goal keeper and he is also the best Spanish goal keeper after De Gea.
.
kiukweli Arizabalaga atakuwa golikipa chaguo letu la kwanza pia ni golikipa bora hispania baada ya De Gea.
-
maneno ya kocha kipenzi chetu Thomas Tuchel
May be an image of 2 people and people standing

 
Of course Arizabalaga will be our first choice goal keeper and he is also the best Spanish goal keeper after De Gea.
.
kiukweli Arizabalaga atakuwa golikipa chaguo letu la kwanza pia ni golikipa bora hispania baada ya De Gea.
-
maneno ya kocha kipenzi chetu Thomas Tuchel
May be an image of 2 people and people standing

Naona umekuwa msemaji mkuu wa habar zote za porojo kuhusu Chelsea mkuu?
 
Kubali tu kuwa hapo umechemsha mkuu, timu ambayo ndio kwanza iko assembled ichalenge ubingwa?
Ukisoma article nyingi + statement ya club kuhus lampard kufukuzwa utaona kuwa msim huu ilikuwa ni kuchallange ubingwa na kupunguza gap lililopo kati yetu na city na liverpool
 
Tuchel ataanza na hii line-up leo
Formation 4-1-4-1

-----------------------------------------------------Werner -----------------------------------------------------------

-----------Pulisic -------------Havertz------------------Mount ----------------------Ziyech------------------

----------------------------------------------------Jorginho --------------------------------------------------------

------Chilwell-------------------------Silva ----------------Zouma -----------------Reece James-------

---------------------------------------------------Mendy -------------------------------------------------------------
 
Ukisoma article nyingi + statement ya club kuhus lampard kufukuzwa utaona kuwa msim huu ilikuwa ni kuchallange ubingwa na kupunguza gap lililopo kati yetu na city na liverpool
Hiyo ya pili ndio sahihi, kupunguza gap na sio kuchalenge. Sio watu wa media ndio wanaweka malengo. Ni bodi inayosimamia klabu. Huwezi kuchalenge ubingwa wakati una timu ya academy na wachezaji wengi wapya hadi wazoeane na wazoee ligi. Msimu wa 2022 ndio msimu muafaka wa kuchallenge ubingwa. Alichoboa Lampard mpaka akafukuzwa ni hayo matumaini ya top 4 yalishaanza kupotea kwa sababu ya kushindwa kubadilika na kuelewana na wachezaji. Ila angefight akapata matokeo ya kumbakiza kwenye top 4 wala asingetimuliwa.

Statement ya Chelsea baada ya kumfukuza kazi Lampard
"We are grateful to Frank for what he has achieved in his time as head coach of the club. However, recent results and performances have not met the club's expectations, leaving the club mid-table without any clear path to sustained improvement.
Chelsea's past eight Premier League results
DateScoreResult
12 DecemberEverton 1-0 ChelseaL
15 DecemberWolves 2-1 ChelseaL
21 DecemberChelsea 3-0 West HamW
26 DecemberArsenal 3-1 ChelseaL
28 DecemberChelsea 1-1 Aston VillaD
3 JanuaryChelsea 1-3 Man CityL
16 JanuaryFulham 0-1 ChelseaW
19 JanuaryLeicester 2-0 ChelseaL
 
Wachezaji watakaofaidika na ujio wa kocha mpya na watakaadhirika pia

Winners: Timo Werner, Kai Havertz, Toni Rudiger and KEPA

Kocha mpya anatoka ujerumani, anaongea kijerumani, tutegemee hao wajerumani wakipewa muda wa kutosha kwenye play minutes labda watuangushe wenyewe. Ktk mechi 15 Werner kafunga goli moja tu tena kwenye FA na kitimu cha mtaani, Havertz yeye kaanza vibaya hadi mechi zingine akawa anawekwa benchi. Rudiger yeye baada ya kurudi majeruhi amekuwa akila benchi na saa nyingine kukosa benchi kabisa

Mchezaji mwingine atakaefaidi ni KEPA, Kepa alifanya vizuri kwenye utawala wa Sarri, ghafla akaanza kufanya vibaya kwenye utawala wa Lampard. Wachambuzi wengi wa soka wadai ubovu wa Kepa unamizizi na ubovu wa Kante, Kovacic, Pulisic, Werner, Havertz, Jorginho
Haiwezekani 90% ya darasa ikafeli halafu tuseme ni wanafunzi vilaza. kule chuo kikuu enzi zangu, lecturer akifelisha darasa zima au kwa asilimia kubwa huwa yeye ndie anaadhibiwa ikiwa ni pamoja na kufukuzwa. Sasa Lampard kushusha viwangi vya wachezaji wote hao maana yake na KEPA yumo na hivyo Lampard na benchi lake la ufundi ndio walikuwa wabovu. Sasa Tuchel kaja tutegemee KEPA atarudi kwenye form yake iliyosababisha zaidi ya mil 70 zilipwe kwa jina lake. Kwa hiyo tutegemee KEPA naye akipewa mechi kubwa kubwa na sio zile zile za FA na Karabao cup tu


Loosers: Mount, Tammy Abraham and Giroud

Mount ni mchezaji mzuri na mwenye kipaji sana kwenye kiungo na ni mchezaji anayeweza kufit takriban kila mfumo. Lampard alimuamini sana kiasi cha kufikia hatua ya kumchosha kwa kumchezesha kila mechi. Tutegemee naye kuingizwa kwenye rotation, sub na saa nyingine kupumzishwa kabisa kwenye mechi zingine. Siku zake za kufanywa mtoto wa mfalme zimefikia ukomo na sasa itabidi kisaikolojia ajiandae kuzoeza benchi na saa nyingi kulala bwenini.

Tammy alishapunguziwa mizigo na FL. Sio kwamba Tuchel atamuacha kabisa ila tutaona akimpunguzia mizigo zaidi na kijitahidi kuinua viwango vya wajerumani wenzake.

Pamoja na kufunga magoli manne kwenye mechi na Sevila, OG umri wake wa miaka 34 utamfanya Tuchell awekeze zaidi kwa vijana wadogop akina Werner na Tammy Abraham. Ningekuwa mimi Giroud ningewahi tu Juve kwa wazee wenzangu


Ushauri
Ili Tuchel afanikiwe na aweze kuwatumia vizuri akina Werner, Kai na hao wengine ni lazima atumie hizi formation mbili
4-1-4-1 au 4-2-3-1
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom