Basi bwana mwaka 2009 chelsea ilikutana na Barcelona kwenye nusu fainali. First leg ilipigwa Camp Nou na kutoka bila bila hii second leg ikaenda kupigwa darajani.
Refa wa hii game alikua Ovrebo.
Game ikaanza chelsea wakapata chuma cha kwanza. Mambo yakaenda vizuri kisha hali ya hewa ikaanza kubadilika.
Alves akamkata Malouda ndani ya box. Ovrebo akasema kosa limetokea nje ya box.
Wakina Drogba wakamuwakia ila yule bwana akaweka pamba sikioni akaendelea na maisha mengine.
Replays zikaonyedha ni kweli kosa limetokea nje ya box.
Game ikaendelea.
Drogba akapata chansi ya kwenda kuscore akawa yupo mbele ya Abidal, Abidal amekazana kumtoa Drogba kwenye reli ila Drogba kakaza huko Valdes anawaza shuti litakalotoka hapo. Kufika kwenye boksi Abidal akaona isiwe kesi akamlamba rafu janja Drogba, Drogba chini.
Ovrebo akageuka zake huyooooo.
Drogba kawaka bwana Ovrebo katia pamba masikioni hata hajali.
Replay inaonyesha Drogba alianza kuchezewa rafu tangu nje ya box, body language inamuonyesha akiwa anajiandaa kupiga shuti kabla hajalazwa chini.
Kisha Chelsea ikiwa inaendelea kushambulia wapo langoni kwa Barca Anelka anapiga shuti linazuiwa na mkono wa Baba Shakira.
Anelka hata hajisumbui kumuonyesha refa kwakua ni kosa lililoonwa na kila mtu lakini Ovrebo wala hata hakujigusa akaamuru mchezo uendelee.
Kisha Abidal akagewa red kwa kumchezea rafu Anelka, marudio yanaonyesha Anelka alijikwaa mwenyewe, hata hivyo haina maana kwakua Abidal alitakiwa awe ametoka tangu muda hata hivyo.
Game ikiwa inaelekea ukingoni Iniesta akatia chuma kusawazisha.
Ikawa 1 kwa 1. Wastani kwa hapo ni Barca anasonga mbele.
Chelsea ikapata kona. Ikapigwa kona mchezaji wa chelsea akaachia shuti, Samuel Etoo akalikinga lile shuti likamgonga mkononi. Pembeni yake Etoo alikuepo Ovrebo.
Ila akawa kama hajaona kitu akajigeuza zake na kuondoka. Ballack akaona huu ni upuuzi akamkimbilia Ovrebo na kumkaripia na kuomba na kila kitu ila Ovrebo hajali, muda huo mpira unaendelea.
Game ikaisha. Chelsea ikatolewa.
Ovrebo alikua ameikatalia Chelsea penati nne za wazi.
Pale pale Drogba akamkimbilia Ovrebo, maafisa wakafika kumzuia ila mashabiki wa chelsea wakamuahidi kifo Ovrebo palepale uwanjani.
Drogba akaigeukia kamera akasema "Are you watching this? Its a disgrace. Its a fvcking disgrace"
Maafisa wakamsindikiza nje Ovrebo kwa kuhofia kuuawa usiku huo huo wakambadilishia hoteli na kumtoa nje ya Uingereza kisirisiri.
Akiwa anahojiwa na jarida la Marca, Ovrebo akasema "Chelsea imeanzishwa 2003, ni timu ndogo ilikua inapambana na timu kubwa. Hata wangepata penati 100 bado ningekataa tu"
Anyway, natania. Alisema "Makocha na wachezaji hua na siku ya hovyo na marefa pia hua na siku hatupo sawa. Siwezi kujivunia kilichotokea siku ile"
Baada ya pale Ovrebo alikatwa kwenye orodha ya marefa wa waliotakiwa kwenye tournaments. Baadaye akaja kutangaza amestaafu.