Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Baada ya kelele za baadhi ya washabiki humu kuomba kukutana na Bayern nilianza kujiuliza ni game gani kubwa Chelsea amecheza akashinda!

Maana ana draw ya United na Tottenham, kafungwa na Liverpool, bado hajacheza na Leicester, Man City na Arsenal (huyu nimemweka kiheshima tu).
Taratibu mzee baba maana washabiki wengine hatukupiga kelele Liverpool ilipofungwa 7-0 na Aston Villa na hata mkifungwa huwa hatuna vihere here vya kuja kwenye uzi wenu.

Kila timu ipambane na hali yake.

Sent from my ONEPLUS A3010 using JamiiForums mobile app
 
Conor Gallagher

Huyu dogo ni mali ya Chelsea yupo kwa mkopo West Brom anakiwasha kweli. Anaonekana kuja kuwa moja ya midfield wazuri duniani. Nacheki game yao hapa dhidi ya Newcastle anacheza vizuri sana lakini kocha kiazi kamfanyia sub haijapita hata dakika wamewekwa goli.

Walikua nyuma kwa goli moja wamepambana wakasawazisha na walikua wanashambulia sana lakini toka atoke wamepigwa goli na Newcastle wameshikilia mchezo

Newcastle 2-1 WBA. View attachment 1648171
Gallagher is currently West Brom's best player, bright spot in all the trainwreck. #CFC

Conor Gallagher vs Newcastle:

88% pass accuracy
4 shots
2 crosses
100% dribble success
4/6 ground duels won
2 tackles

Impressive once again.
 
Yes!!! Yes!!
Nimemuona huyo Dogo mechi yao na Newcastle Bonge la Midfielder.
 
Taratibu mzee baba maana washabiki wengine hatukupiga kelele Liverpool ilipofungwa 7-0 na Aston Villa na hata mkifungwa huwa hatuna vihere here vya kuja kwenye uzi wenu.

Kila timu ipambane na hali yake.

Sent from my ONEPLUS A3010 using JamiiForums mobile app

Hamkuzuiwa kuja, hii ni open forum.

Mkitaka tusije tengenezeni group la WhatsApp au Telegram.
 
Taratibu mzee baba maana washabiki wengine hatukupiga kelele Liverpool ilipofungwa 7-0 na Aston Villa na hata mkifungwa huwa hatuna vihere here vya kuja kwenye uzi wenu.

Kila timu ipambane na hali yake.

Sent from my ONEPLUS A3010 using JamiiForums mobile app
Wewe hukuja wenzako walikuja

Ni vizuri kufariji wafiwa
 
Memba wa hili jukwaa wengi wanapendelea sana kutukana sijui shida ni nini.

Matokeo vipi uko jana tunazika au tunasafirisha? Kamati ya chakula tumeshaanza maandalizi tayari
tapatalk_1576584101047.jpg
 
Nyie fisi maji kiburi cha kulala hadi muda huu mnatoa wapi???
 
Kuna fans ni wanafiki kwel timu ikishinda wata sifu sana ila tukifungwa lawama kibao mara tunabahatisha kisa match moja
Alafu unkut mtu mwenyw kaangalia highlights tu ankuja kutema nyongo uku
 
Liverpool aliwakosa wachezaji kibao kwa injuries still alikuwa anashinda kibingwa tena mechi ngumu kwa kuwatumia madogo + mfumo bora + mbinu bora za Klop

Chelsea bado sana mfumo wa uchezaji, bado sana mbinu za mwalimu, bado sana quality players TUNABAHATISHA
Ila we jamaa bwana.

Juzi unadai wapinzani wako ni Barcelona, Bayern na Madrid.

Leo unasema mnabahatisha.

Fuata ushauri wangu. Fungua akaunti ya komedi Youtube upige pesa.
 
Leo kuwakosa Pulisic na Ziyech kwa pamoja imetucost
mkuu Pulisic alikua moto sana msimu uliopita ikn msimu huu hajaufaidi sababu ya majeraha na nafasi yake anacheza Timo,hata kama unazungumzia angereplace nafasi ya Ziyech bado sio jambo la kutegemea sana kwa sababu mbili (1)anamudu zaidi LW kuliko RW (2)hajarudisha form yake
 
Mimi niliwahi kusema Chelsea ina plastic kibao. Kuna mmoja alikua uzi wa liva anatukana watu walipopigwa goli moja akayeyuka juu kwa juu na huku wote wamepotea.

Wametususia maiti.

Chelsea ina plastic fans tu. Mwingine juzi anasema eti level yao kubwa wapinzani wa chelsea ni Madrid, Barcelona na Bayern. Leo anasema hua wanashinda kwa kubahatisha.

Hii timu ina mashabiki wanaoamini utatuzi ni usajili tu. Wiki nyuma mtu anakuambia wana kikosi kipana (na no kweli) leo anasema inabidi wasajili winger. Unabaki unashangaa "Huyu anaelewa nini juu ya kikosi kipana?" Hapo hapo anasema mfumo (yaani 4 3 3) imewaangusha wakati huu mfumo wametumia mara nyingi na wameshinda.
 
Hii timu imemiliki mpira kwa 70%+ lakini imeshindwa kucreate big chance hata moja. Timu nyingine ambayo jana haijacreate big chance hata moja ni man u. Unadhani ni coincidence?

Mimi nasema hapana.

Zote zinafundishwa na former players ambao hawana uzoefu na ukocha. Muda mwingine unakua hauchezi na timu unakua unacheza na kocha.

Ukikutana na Everton au Tottenham ya sasa wewe uko kwenye mapambano na kocha. So msinune wala msiteseke ndiyo sababu walivyokutana ole na frank ikawa sare (tena ya bila kufungana) wakati ukiangalia kikosi unaona magoli yangetiririka plus ile namba 3 ya mdhamini ingekua ni bandika bandua.

Kumbe wanabahatisha.
 
Mimi niliwahi kusema Chelsea ina plastic kibao. Kuna mmoja alikua uzi wa liva anatukana watu walipopigwa goli moja akayeyuka juu kwa juu na huku wote wamepotea.

Wametususia maiti.

Chelsea ina plastic fans tu. Mwingine juzi anasema eti level yao kubwa wapinzani wa chelsea ni Madrid, Barcelona na Bayern. Leo anasema hua wanashinda kwa kubahatisha.

Hii timu ina mashabiki wanaoamini utatuzi ni usajili tu. Wiki nyuma mtu anakuambia wana kikosi kipana (na no kweli) leo anasema inabidi wasajili winger. Unabaki unashangaa "Huyu anaelewa nini juu ya kikosi kipana?" Hapo hapo anasema mfumo (yaani 4 3 3) imewaangusha wakati huu mfumo wametumia mara nyingi na wameshinda.
Hao unakuta wanafurahia mikeka na siyo timu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom