CHELSEA 3-1 LEEDS UNITED, Premier League: Post-match reaction
By Mlanzi
Olivier Jonathan Giroud, Kurt Happy Zouma Pamoja na Christian Mate Pulisic kwa pamoja wamekamilisha comeback na kuipa Chelsea ushindi Mbele ya Mashabiki wapatao 2,000 katika Dimba hatari kuliko Madimba yote duniani, nalizingumzia Dimba la Stamford Bridge.
Makosa madogo kutokea dimba la kati yalimpa nafasi Patrick Bamford kuipatia Leeds United bao la kwanza kabla ya ile clinical finish kutoka kwa Olivier Jonathan Giroud dakika ya 27 akipokea assist kutoka kwa Reece James.
Kabla nisahau! Kina kitu sijakipenda kutoka kwa Mashabiki walipokuwa wakisema "TAKE A STAND AND BOO THE KNEE. WE ENGLISH DON'T KNEEL FOR CRIMINALS" haya maneno ni ya kibaguzi na hayana nafasi katika soccer

!
Ukiachana na performance ya team, kuna ukomavu unazidi kujengeka unaoifanya team yetu iwe tushio...!! Ile Character ya team pindi inaporuhusu bao la mapema. Team inapambana kupata come back na ushindi Juu. Kwa mfano, hii game dhidi ya Leeds, Game dhidi ya WBA nk. Hii ndiyo proper energy itakayotupeleka mbali.
Katika hii game Manager Frank Lampard alikuwa amepanga kikosi bora kabisa kwa upande wangu

! Kikosi kilichokuwa na veteran Olivier Jonathan Giroud kuanza mbele ya Tammy Abraham. Nina uhakika Jibu litapatikana hivi karibuni la nani aanze mbele ya nanini na wakati gani sub zifanyike.
Timo Werner asipokufunga basi atafanya assist..!! Hebu check ile pace na assist yake dakika ya 93!!

!! Mabepari wanaita brilliant. Baada ya kurejea kutoka half time, turning point ilikuja kupitia corner kick, ambapo Mason Mount alim-assist Kurt Happy Zouma dakika ya 62.
Pongenzi kwa goalkeeper wa Leeds Meslier kwa kuokoa rundo la mashambulizi kutoka kwa Timo Werner Pamoja na Mason Mount. Bao la tatu lilikuja Kutoka kwa Christian Mate Pulisic dakika ya 90+3 Akipokea assist kutoka kwa Timo Werner.
Subs zetu ZIlikuwa Christian Pulisic akimtoa Hakim Ziyech, Huku Mateo Kovacic akiingia upande wa Kai Havertz na Tammy Abraham upande wa Olivier Jonathan Giroud.
Next up: Tutawakaribisha Krasnodar pale pale Stamford Bridge katika Champions League group stage.
KTBFFH!