Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Kuna baadhi ya matatizo aliyonayo Lampard hasa ya kuwaamini kupita kiasi baadhi ya academy kama Abraham dhidi ya Giroud na nyingine kupanga wachezaji out of position lakini haimuondolei kuwa kocha mzuri
After all kila kocha ana madhaifu yake na mashabiki husika wa hizo timu wanazijua madhaifu ya makocha wao
Hata Klopp na uzoefu wake alishawahi kukiri kuwa huwezi kusajili wachezaji wazuri wengi kwenye timu na wakaleta mafanikio ya haraka. Wachezaji wanahitaji kujuana, kumjua kocha na falsafa yake ndipo waanze kuleta matokeo. Msimu huu ni msimu wa timu kujuana na kumsoma kocha. Akiboronga msimu ujao no way lazima tumbadilishe kocha ila msimu huu, tumuache kwanza aisuke na kutengeneza culture ya timu ili iweze kuleta makombe.

Shime tumpe Lampard muda na tuache kusodoa au kukashifu hata mafanikio aliyoyapata akiwa na wachezaji wa kawaida tu
Wee ulitegemea baada ya Hazard kuondoka akina Luiz, Willian, Kepa, Tammy Abraham, Christensen, Tomori watuletee makombe??, Top 4 yenyewe ilikuwa ni miracle na nadhani Lampard alipewa bonus kwa kupata hayo mafanikio. Management walimtaka tu timu isishuke daraja. Maana yake hata kama Chelsea ingeshika nafasi ya 17 bado Lampard angekuwa na mafanikio

Tumpe Lampard muda aijenge timu na timu izoeane ili waanze kutupa raha
Mimi sitetei Giroud eti acheze. Wakati Gaucho Ronaldinho anapigwa benchi ili Messi apate nafasi hakuna aliyemwelewa vzr Guadiola. Kilichotekea baadae ni stori
 
ID ya October 2020 ndo unakuja kuitumia kusema Lampard uwezo mdogo!? Au wewe ndo mwenye uwezo mdogo?
Sasa mambo ya ID yanaingiaje hapa?, kocha kiufupi uwezo wake mdogo, mimi uwezo mdogo ila kocha uwezo mdogo zaidi.

Akina Kova Giroud wanaprove kabisa kocha akili kisoda.
 
Sijasema benzema ni mbovu, nilimquote alichokisema kua kane ni top striker ndio mana anaanza mbele y Abraham, ndio mana nikamuuliza hilo swali.
We ndio hujui chochote, home work yako fanya mwenyewe.
Umeshaijua sababu ya Benzema kutoitwa nationa team?
 

Attachments

  • Screenshot_20201114-123944_1605376254461.jpg
    Screenshot_20201114-123944_1605376254461.jpg
    29 KB · Views: 15

Similar Discussions

Back
Top Bottom