Mimi ni mpenzi mkubwa wa Lampard na nitaendelea kuwa hivyo ila penye ukweli tuseme. Labda Lampard abadilike mbele ya safari ila kwa msimu uliopita na huu unaoendelea sioni kama Lampard ana mbinu za kufanya vizuri. Tuna wachezaji bora kuliko timu nyingi za EPL including Aston Villa na Everton to mention few. Sioni mbinu za kikocha hapa, ninachoona wachezaji wamekaririshwa namna ya kucheza na ndio maana hawachezi vizuri. Nakuambia hii timu angerudi MOU tungechukua ubingwa mwaka huu ukichukulia kuwa consistency ya timu zilizotegemewa kushindania hili kombe kama Liverpool na Man City sio nzuri. Ila kwa kuendelea kucheza mchezo wa kukaririshwa sioni kama tutabeba hata kombe la mbuzi achilia mbali top 4. Kama mmeshagundua upepo wa ushindani mwaka huu umebadilika. Kuna dalili za sura mpya kuwepo top 4 na 6.
Ligi ya England huwezi kuchukua kwa sababu tu eti una wachezaji wa ghali na world class kama Mendy, Silva, Werner, Pulisic, Havertz, Kante nk. Kombe la England linabebwa kwa mbinu na tacktics na tricks za hapa na pale. Sioni kama haya madoido Lampard anayo.
Kwa takwimu tu kwa wale wasiojua madhara ya matokeo tunayopata, katika mechi 6 tumefungwa moja, tume droo 2 na kushinda mbili. Maana ya takwimu hizi ni nini? Katika point 18 tumepata 9 na kupoteza 9 au kwa maneno mengine katika mechi 6 tumeshinda 3 tukafungwa 3. Mtizamo mwingine wa takwimu ni huuu, katika mechi 5 za hivi karibuni tumeshinda 1 tumefungwa 1 na kudroo 3 maana yake katika point 15 tumepata 6 na kupoteza 9. Hii ni trend mbaya kabisa. Maana yake katika mechi 5 za mwisho tumeshinda 2 na kufungwa 3. Huko mbele wachezaji watazoea kufungwa na kudroo na mwisho wa msimu tutaishia kugombea Europa na akina Westham
Hizi timu mwaka huu ziko moto na ndio basis ya maoni yangu kuwa Chelsea na Kocha hafanyi vizuri. Leeds, Aston Villa, Everton, ukiachilia mbali zile za top 6 ambao tayari wao ni washindani wetu. Kwa kusema haya Chelsea ina competitors 8 wa top 4 na Europa. Siwaoni Arsenal wakuboronga kama mwaka jana, siwaoni Liverpool wakiboronga kiasi cha kukosa top 4, siwaoni Man city wakiboronga kiasi cha kukosa top 4, siwaoni Spurs wakiboronga kiasi cha kukosa top 4, sizioni hizo timu ngeni nilizozitaja zikiboronga kiasi cha kukosa top 4. Sasa kama. Sasa kama timu 8 zote zina sifa za kuingia top 4, Chelsea inawekwa wapi kwenye top 4 au Europa?. Unless Lampard anakuja na techniques, tactics, tricks za kupora point 3 kila mechi kama Conte na MOU ndipo Chelsea itakuwa na uhakika wa top 4 kama sio ubingwa