Kitambo kidogo kuna jamaa nilifahamiana naye alikuwa na demu mzuri ila alikuwa hamjali. Siku moja nikajikuta tu nimekaa na yule dada nikaongea naye kwa dakika kama kumi hivi kawaida tu na ku flirt kidogo demu akawa amefurahi sana. Vicheko meno yote nje na pozi za kunipiga vikofi vya kimahaba kwenye bega na kifuani. Nilikuwa na haraka kwa hiyo nilimaliza maongezi nae nikaendelea na shughuli zangu. Tulivyomaliza maongezi yule dada akaenda moja kwa moja kwa bwana wake na kumwambia rasmi kuwa anamuacha na baada ya kumuacha akaja kwangu. Basi tangu siku hiyo yule jamaa na marafiki zake walikuwa wakiwa na mimi watamsema vibaya sana yule demu, mpaka story za mabaya aliyofanya kipindi cha nyuma. Mimi sikuwa mtu wa kuhukumu mtu kwa mambo yaliyopita so nikwapotezea tu na nikaenjoy life.
Sasa wao wameshindwa kumjali Willian kwa mkataba mzuri, amekuja kwetu, na wao wanashinda kumsema vibaya. Mara wamuite mstaafu, mara waseme hajui mpira...Sisi hatujali.
COYG