Ngoja niwaambie kitu wanachelisii kuhusu usajili wenu japokuwa mimi sio shabiki wenu.
Chelsea tatizo lenu kubwa lipo kwenye beki na mshambuliaji.
Sasa nawashangaa mnavyohangaika kusajili viungo washambuliaji wakati miviungo mnayo ya kutosha!
Huyu Havert sio namba 9 kama hamjui, ni natural 10!
Ona mmesajili Timo Werner (LWF), Ziyech (AMF/RWF) bado mnataka kumsajili Kai Havert (SS) wakati mlitakiwa msajili mtambo wa kupachika mabao, nazungumzia Natural Striker (9, CF) ili tatizo lenu lipate utatuzi.
Na sitoshangaa msimu ujao tukaendelea kuwaona akina Zouma, Rüdiger na Azpilicueta kule nyuma maana huwa mnajenga katikati halafu nyuma mnaziba nyufa tu, mwisho wa siku ukuta unaachia tena.