Ukiondoa mechi za Mancity dhidi ya Aston villa na Watford ambazo Mancity ilishinda 8-0 na 6-1, Chelsea ndio timu inayoongoza EPL kwa kuwa na magoli mengi ya kufunga kwa mechi moja ikiwa na average ya 3.16 per match na ukiweka hizo mechi mbili nilizozitaja ndipo Mancity inakuja ya kwanza, Chelsea ya pili. Kilichotuangusha ni kufungwa magoli. Tunazo clean sheet chache sana
Chelsea ni ya 15 kwa clean sheet (7)- too bad
Chelsea ni ya 3 kwa kushinda mechi (17) mbele ni Man city (21) na Liverpool (29) tu
Chelsea ni ya 4 kwa kufunga magoli 60, walio mbele ni Leicester city (63), Liverpool (72) na Man city (81)
Unaona kinachotuangusha ni kufungwa tu, hata mechi nyingi tulizoshinda tulifungwa magoli kadhaa
Katika mechi 17 tulizoshinda 10 tumefungwa hata kama tulitoka na point 3 zote
Kwa maelezo haya mafupi, uwezo wa kufunga tunao, wakiongezeka akina Ziyech na Werner ndio itakuwa hatari
Tatizo kubwa ni kujilinda na nashangaa mpaka sasa hivi hatujalishughulikia hilo tatizo. Ndio maana naungana na wanaosema dili la Havertz liwekwe kando kwanza, tuwalete akina LB kama Ben Chilwell au Álex Grimaldo, au CB kama akina Upamecano, Konate, Alex Telles ana miaka 27, kuwa na senious wengi kwenye timu sio afya, Azpi anatosha kuwapa uzoefu akina James na watakaokuja. Hata Alonso akibaki atasaidia.