Kwa jana timu imecheza vizuri..
Kante kwenye nafasi yake halisi alicheza vizuri sana, lakini haimaanishi kua giorginho ndo hatumuhitaji tena hiyo itakua uongo.
1) mechi ya jana ni chelsea vs timu ndogo villa, hata angeaza nani obvious tungetawala mchezo, Jo kwenye big match hua anasaidia sana kubalance mchezo. Hua hatuelemewi sana. Kante pekee hawezi,kipindi kile alikua na mnyama matic ndo maana combo yako ilikua nzuri sana.
RLC , James na Tammy, jana wameonyesha bado wanasafari ndefu sana kua top players,
Cheek alikua mzito sana kwa jana, sidhani kama anafaa kucheza winga, ni bora winga angecheza mount maana ni mshapu sana.
James, alikua anapoteza mipira kizembe mno, alikua anacheza utani utadhani yuko kwenye mazoezi. Hata loose ya mpira ya mwisho kidogo itupe athari chelsea (foul ya mwisho waliyotukosa villa).
Tammy bado ana utoto ,, hakui kabisa. Jana niliona tatizo lile, hawezi kucheza mipira ya juu japo ni mrefu. Na pia ana mambo mengi sana, muda wa kutoa pasi na yeye anajiona willian au pulisic anataka apige chenga, unakuta anapoteza mipira kirahisi sana
Yote na yote. Muhimu ni kua tumepata point 3 muhimu sana.
Ni muda wa kujikaza sana ili kufikia Lengo.