Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Vip mzee si ulitaka kante auzwe kwasababu aendani na mfumo wa Lampard umeona leo Lampard kaamua yaishe kamchezesha kwenye eneo lake halisi Hili umeshindwa kabisa kuligusiwa Kama Lampard angekuwa anampanga kante kwenye eneo lake tusingekuwa tunapoteza game kirahisi jorginho alitukosti Sana kwenye nafasi yake.Tukija kwenye issue ya Gilmour yah Ni mchezaji mzuri lakini Kama atachezeshwa basi kante hatachezeshwa kwenye natural position yake labda tu Lampard ampe Gilmour role nyingine ya number 10. lembu
Ndugu yangu mechi sikuangalia, jana usiku nilijitahidi kuangalia replay nikashindwa kwa sababu ya usingizi. Pamoaj na hayo comments nyingi za humu ndani na za kwenye mitandao mingine inaonyesha Kante alitawala katikati kisawasawa na ndio maana possession ya Chelsea ilikuwa 74% kwa mechi yote. Sisi washabiki tunachotaka ni hilo, matokeo sio mchezaji. Kante akifit kwenye mfumo tunakuwa pamoja, asipofit auzwe ndio lengo. Alichofanya Lampard ni sawa kabisa ila tu amtafutie pa kumuweka kinda Bill Gilmour kwa sababu anatufaa pengine kuliko hata hao akina Havertz wa mil 90.
Maoni yangu Kochga aendelee kumuweka hapo asibadilishe tena mfumo wala wachezaji kama alivyofanya Conte msimu wa 2016/17 alivyoswitch kwenye mfumo wa 3-4-3 hadi kubeba kombe baada ya kufungwa na Arsenal 3-0. Hiki kipindi sio ya kubadilibadili mifumo na wachezaji
 
Kante akiendelea kuchezeshwa 6 Jognho hana chake atafute timu ya kwenda. Kuliko kumchezesha Kante wrong position bora akae bechi kuliko kumuharibia Cv yake

Sent using Fly in any Weather.
Auzwe chap chap kabla hajashuka bei kwa sababu Gilmour yupo Kante akiumia
 
Sure Lampard akiamua kumchezesha Kante namba 6 hakuna wa kumweka benchi Kante. Hivyo hivyo kwa Pulisic akiwa hana majeruhi hakuna wa kumweka benchi.

Jognho namba 6 hapana tulishasema sana kwamba jamaa ni mzito hana kasi, hawezi kupora mipira, anacheza rafu sana.

Jognho jana angecheza pale katikati ingekuwa uchochoro wa villa kupita. Na beki yetu ya ovyo ingelemewa

Glimour bado mdogo jamani aendelee kupata experience mdogo mdogo. Muda wake ukifika hatakosa namba.

Sent using Fly in any Weather.
Cash Money Forever jorginho Ni bonge la mchezaji na Ni mchezaji muhimu Sana SEMA Ni kwamba Lampard ndio mwenye shida la kujua eneo lipi jorginho atafit zaidi ukiachia weakness yake ya ukabaji lakini ana quality kubwa anajua kucontrol game nzima, ana pass accurancy kubwa na ajua kupiga pass za mwisho na key pass so Lampard anatakiwa amchezeshe advance role sio DM hapa ndio ubora wake utaonekana.Me sipendekezi jorginho auzwe kabisa @lembu
 
Vip mzee si ulitaka kante auzwe kwasababu aendani na mfumo wa Lampard umeona leo Lampard kaamua yaishe kamchezesha kwenye eneo lake halisi Hili umeshindwa kabisa kuligusiwa Kama Lampard angekuwa anampanga kante kwenye eneo lake tusingekuwa tunapoteza game kirahisi jorginho alitukosti Sana kwenye nafasi yake.Tukija kwenye issue ya Gilmour yah Ni mchezaji mzuri lakini Kama atachezeshwa basi kante hatachezeshwa kwenye natural position yake labda tu Lampard ampe Gilmour role nyingine ya number 10. lembu
Hujawahi ona timu ina defensive midfielders wawili? Yaan upo uwezekano wa Gilmour na Kante kucheza pamoja na game hizo huwa ni zile ambazo tumeelemewa sana yaan mashambulizi hayakauki. Ila ubaya wake inadhoofisha madhambulizi kwa sababu umelimit midfielder kutawala mchezo so inawapa nafasi wingers so kama hakuna mawinga wazuri kazi inakua kubwa.

So inawezekana kante/Jorginho/Gilmour wawili kati yao kuanza pamoja.
 
Hatuwezi kuuza wazeshaji chap chap kwa kuangalia swala la pesa tuu, tunaangalia mchezaji ana mchango gani kwenye timu.

Hatuwezi kumuuza mchezaji timu ikashake, ingekuwa swala la pesa Madrid ingewauza modric, kroos, Ramos, Benzema wakiwa na age ya 20's

Kwa kazi ambayo Kante ameifanyia Chelsea mpaka sasa hata akiondoka bure tumeshapata faida kubwa sana kwake (Kimakombe), kuliko hiyo faida ya kwenda kumuuza sokoni.

Glimour bado mdogo usimwesabie kwa sasa anatakiwa aendelee kukua chini ya Kante.

Sent using Fly in any Weather.
Sisi mashabiki hatutaki mchezaji auzwe ila klabu ya mpira inafanya business. Na business ni kufanya shughuli yeyote yenye tija. Gilmour akienda klabu nyingine tutamtaka kwa Mil 70 hadi 90 kwa umri huo huo
Kama tunawahitaji wachezaji wazuri kuuza mchezaji asiyekuwa na matumizi ni jambo lisilokwepeka.
Tunamhitaji Chilwell mil 80
Tunamhitaji Havertz mil 80
Na bosi kasema policy yake ni kuuza mchezaji ili kumnunua mchezaji
 
Chelsea kudadek zenu laana ya kutuuzia mzoga Luiz itawatafuna, malipo ni hapahapa duniani na hao wanaokuja hao mkae mkao wa kulia kilio cha mbwa koko maana itakuwa ni mizigo ya mavi hapo darajani,haiwezekani sisi tuwape mtu anayewapa points 3 muhimu OG alafu nyie mtubambikie kinyesi katika mfuko wa rambo mkitudanganyia kuwa ni dhahabu......
 
Chelsea kudadek zenu laana ya kutuuzia mzoga Luiz itawatafuna, malipo ni hapahapa duniani na hao wanaokuja hao mkae mkao wa kulia kilio cha mbwa koko maana itakuwa ni mizigo ya mavi hapo darajani,haiwezekani sisi tuwape mtu anayewapa points 3 muhimu OG alafu nyie mtubambikie kinyesi katika mfuko wa rambo mkitudanganyia kuwa ni dhahabu......
tunawapa na batshuay
 
Jana nilibadilika rangi na kuwa mwekundu pale James alipokuwa anagawa mipira kwa adui kidogo tu team ya mwisho ipate sare ,Lampard simuelewi kabisa haswa sub na upangaji wa team
 
Kwa jana timu imecheza vizuri..

Kante kwenye nafasi yake halisi alicheza vizuri sana, lakini haimaanishi kua giorginho ndo hatumuhitaji tena hiyo itakua uongo.
1) mechi ya jana ni chelsea vs timu ndogo villa, hata angeaza nani obvious tungetawala mchezo, Jo kwenye big match hua anasaidia sana kubalance mchezo. Hua hatuelemewi sana. Kante pekee hawezi,kipindi kile alikua na mnyama matic ndo maana combo yako ilikua nzuri sana.

RLC , James na Tammy, jana wameonyesha bado wanasafari ndefu sana kua top players,
Cheek alikua mzito sana kwa jana, sidhani kama anafaa kucheza winga, ni bora winga angecheza mount maana ni mshapu sana.
James, alikua anapoteza mipira kizembe mno, alikua anacheza utani utadhani yuko kwenye mazoezi. Hata loose ya mpira ya mwisho kidogo itupe athari chelsea (foul ya mwisho waliyotukosa villa).

Tammy bado ana utoto ,, hakui kabisa. Jana niliona tatizo lile, hawezi kucheza mipira ya juu japo ni mrefu. Na pia ana mambo mengi sana, muda wa kutoa pasi na yeye anajiona willian au pulisic anataka apige chenga, unakuta anapoteza mipira kirahisi sana

Yote na yote. Muhimu ni kua tumepata point 3 muhimu sana.
Ni muda wa kujikaza sana ili kufikia Lengo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom