Nafasi ngapi Abraham anakosaga? Au uangalii mwangalie game dhidi ya man city alipata nafasi mbili za wazi kakosa, Kuna game pia tulicheza na Liverpool Stamford bridge kakosa chance za wazi.Team kubwa Kama Chelsea haiwezi kumtegemea Abraham kuwa striker wao tegemezi
Kukosa ni jambo moja. Kama unafuatilia michezo yopte sio Chelsea tu, strikers wazuri wanakosa chances nyingi kuliko wanazofunga. kinachoangaliwa kwenye striker ni conversion rate
Ebu tuangalie hiyo conversion rate ya strikers
EPL
Jamie Vardy 69% - huyu ni counter attack strikers mara nyingi wanakuwa na touches chache kwa sababu ya nature ya uchezaji wao
Marcus Rashford 58% - kama Vardy hapo juu
Dany Ings 58% - kama hao wa juu
Tammy Abraham 56% - purely one touch football, touches kwenye box zinakuwa nyingi na hivyo shot golini zinakuwa nyingi likewise. Uchezaji wa nature hii strikers kuwa na accuracy percentage kubwa ni vigumu
Sergio Agüero 51% huyu nature ya uchezaji wa timu yake ni kama Chelsea
NJE YA EPL
LALIGA
Karim Benzema 51% uchezaji wao ni kama Chelsea - Box to box football
SERIE A
Ciro Immobile 62% - huyu ndie striker kwenye big legues aliyempita Abraham kwa goal acuracy
Romelu Lukaku 65% striker mwingine aliyempita kwa mbali Abraham
Budesliga
Robert Lewandowski - 58% pia huyu kampita Abraham kwa mazingira yanayofanana
Timo Werner 63% - na huyu pia kampita Tammy
Frech League One
Kylian Mbappé - 60% kamzidi pia
Mouser Dembele - 53% - huyu ni mojawapo ya target ya Chelsea kwenye ligi ndogo tu Abraham kampita mbali kwa accuracy na kwa assists
Kwa maelezo haya, Abraham anashutumiwa bure, yuko kwenye nafasi nzuri tu
Jambo lingine nilishasema huko nyuma Sio striker ndie peke yake anaamua timu kubeba makombe, ni safu nzima
Liverpool kwa mfano wako mbali sana kwa ufungaji na mechi walizoshinda lakini sio kwa sababu ya striker wao
Striker wa Liverpool mara nyingi ni Firmino ana magoli 8 na assists 7 accuracy 59%. Hii inaonyesha kuwa Liverpool hawamtegemei yeye tu kwenye kufunga
Mawinga kama akina Mane na Salah wanafunga. Viungo wanafunga
Ukija kwa Mancity ni hivyo hivyo hata kwenye misimu yote miwili waliochukua ubingwa hawakumtegemea striker pekee afunge
Chelsea tukikazania sana kusajili striker na kuondoa obligation za kufunga kwa wachezaji wengine kama viungo na wingers hatutaweza kuchukua kombe lolote.
Tunahitaji kutengeneza Chemistry ya timu nzima iwe na wachezaji wa kubeba makombe
Kipa awe ni caliber ya makombe
Mabeki wawe ni caliber ya kubeba makombe viungo hivyo hivyo
Tuache kuweka matumaini makubwa sana kwa striker kwa sababu hata Ciro Immobile akija Chelsea na kuwa na watoa huduma wavivu, wazembe na wasio kuwa wabunifu. Atashindwa kazi ile anayofanya Lazio