Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Alishawahi kipindi Luis Suarez bado yupo Liverpool FC
Kuna watu ni wanafiki aisee! Hivi kigezo kipi kinatumika kusema Lampard ni kocha mbovu? Au ni hisia tu za kishabiki?

Watu wanasema Tammy haisaidii Chelsea! hii ni akili kweli? Hivi Top four legue Ulaya wachezaji wangapi wenye umri wa Tammy wana magoli 12?
Ni maajabu unamshabikia mchezaji ambaye hajaprove kitu EPL alafu mchezaji mwenye magoli 12 a half a season unamuona si kitu.

Huyo Timo Werner akija EPL msimu wa kwanza hata magoli 15 yatampa shida kuyafikisha.

Miaka miwili ijayo Tammy na Mount watakuwa lulu Ulaya. Tusirudie ya De Bruyne, Lukaku na Salah. Huu ndo muda wa kuwachezesha Tammy na Mount.

Hivi Hazard aliwahi kufikisha magoli 18 EPL katika msimu wowote alioichezea Chelsea. And still is a legend
Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diego Costa msimu wa kwanza goli 22 na majeruhi juu, msimu wa pili goli 26 epl.
Mzee tunao ujua mpira tunakuunga mkono..

Hawa wanataka kila mechi tammy awe anashinda.. kitu ambacho hakiwezekan,tammy ndio kwanza msimu wake wa kwanza

Tammy kajitahd sana, kwangu mm tammy akifikisha goli 15, ni foward mzuri ukizingatia ndio msimu wake wa kwanza na bado umri mdogo

Huyo diego costa hajawah kufikusha goli zaidi ya 21, msimu mzima

Chelsea ya sasa inahitaji central defender na left defender wa upande wa kushoto, tena hao wote wawe warefu,

Tomori ni mzuri lakin ni mfupi ndio maana, lampard ana orefer zuma aanze kwa sbbu ni mrefu

Vile vile tunahitaji goalkepeer, ina bidi caberelo tumuuze tumchukue kipa mwingine ampe changamoto kepa

Vile vile tunahitaji kiungo mmoja ambae ana uwezo kufanya assist kama alivyokuwa fab

Na tunamuhitaji sancho...


Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu ni wanafiki aisee! Hivi kigezo kipi kinatumika kusema Lampard ni kocha mbovu? Au ni hisia tu za kishabiki?

Watu wanasema Tammy haisaidii Chelsea! hii ni akili kweli? Hivi Top four legue Ulaya wachezaji wangapi wenye umri wa Tammy wana magoli 12?
Ni maajabu unamshabikia mchezaji ambaye hajaprove kitu EPL alafu mchezaji mwenye magoli 12 a half a season unamuona si kitu.

Huyo Timo Werner akija EPL msimu wa kwanza hata magoli 15 yatampa shida kuyafikisha.

Miaka miwili ijayo Tammy na Mount watakuwa lulu Ulaya. Tusirudie ya De Bruyne, Lukaku na Salah. Huu ndo muda wa kuwachezesha Tammy na Mount.

Hivi Hazard aliwahi kufikisha magoli 18 EPL katika msimu wowote alioichezea Chelsea. And still is a legend
Sent using Jamii Forums mobile app
Wee una mawazo kama yangu, Tammy na Mount ni wachezaji wa kawaida kwa sababu tunao, ngoja waende kucheza kwingine!!
 
Kumkashifu Timo Werner siyo sahihi.

Kiuchezaji Timo Werner yupo tough sana na analijua goal kuliko Tammy. Anafunga goals za mbali pia anafunga goals za Vichwa.

Huu msimu peke yake kwenye Bundesliga Timo werner amecheza match 17 tu ila ana goals 18 na assist 6. Unawezaji kumuunderrate mtu kama huyu.?

Huyo Tammy abraham akipata majeruhi. Niambie una Striker gani wa kumuweka pale mbele?

Pia Tammy ameshindwa kuonesha makali kwenye Big games.

Kuwa na Tammy kusitufanye tubweteke na tushindwe kutafuta Striker mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Timo tunamtaka na Tammy tunamtaka, wote tupo pamoja
 
ARSENAL 1-2 CHELSEA, Premier League: Post-match reaction, ratings

By Mlanzi

Tammy Abraham na Jorge Luiz Frello Filho a.k.a Jorginho wameiangamiza Arsenal pale pale Emirates Stadium dimba lililokuwa likifahamika kama Ashburton Grove enzi zile.

Ngoja nianze na hii formation ya 3-4-3. Naweza kuwa tofauti kidogo but mfumo huu bila ya Marcos Alonso kuwepo uwanjani 3-4-3 inakuwa useless. Chelsea inakuwa toothless. Sijasema Emerson Palmieri ni mbovu hapana, lakini mfumo huo hauwezi. Kulingana na kikosi chetu 3-4-3 inahitaji tireless wingbacks kama MarcosAlonso. Marcos Alonso anapanda na kushuka kumliko Emerson Palmieri, isitoshe Marcos Alonso ni strong na ana experience. Marcos Alonso ni hatari zaidi kwenye box la wapinzani.

Kuutumia mfumo huo tunahitaji mbadala sahihi ambae ni left footed player kama Marcos Alonso. Nadhani Frank Lampard analiona hilo. Na huenda wanamfuatilia Ziyech mchezaji mwenye uwezo wa ku-unlock wale stubborn defenders. Emerson Palmieri atatuchoma sana unless tumtumie katika formation nyingine.

Chelsea tuliuanza mchezo vibaya na tulicheza ovyo dakika 30 za mwanzo kiasi cha kuruhusu bao kutoka kwa Arsenal bao lililofungwa dakika ya 13 na kudumu kipindi chote cha kwanza. Frank Lampard alibadili mfumo dakika ya 34 na kuanza kutumia 4-3-3.

Ujio wa Jorge Luiz Frello Filho a.k.a Jorginho dakika hiyo ya 34 ulibadilisha kabisa appetite ya team. Jorginho ni midfielder lakini ni kama kocha awapo uwanjani, Jorginho ni vice-captain lakini ni kama full captain awapo dimbani. Anaipanga team, anapandisha team, anahamasisha team kama sote tulivyo ona mara baada ya Frank Lampard ku change formation dakika ya 34 na kuanza kutumia 4-3-3 ambapo Jorginho alimpumzisha Emerson, alafu Cesar Azpilicueta akahamia left back, na Fikayo Tomori kuhamia right back.

Dakika chache baadae Chelsea tulitakiwa kupata penalty na Arsenal walitakiwa kuwa 10 uwanjani baada ya Guendouzi kumvuta Tammy Abraham ndani ya penalty box. Cha ajabu siyo referee wala VAR walioiona hiyo.

Juhudi za Chelsea katika second half zilikuwa nzuri especially wakati team ikitafuta equalizer goal. Kazi na temper ya mchezo ilipanda na bao la kusawazisha lilipatikana kutoka kwa Jorginho dakika ya 83 mara baada ya keeper Bernd Leno kushindwa kuokoa free kick kutoka kwa Mason Mount na mpira kumkuta Jorginho aliyekuwa katika nafasi nzuri.

Yes! Kunawatu tunadhani Jorginho hakutakiwa kuwa uwanjani baada ya kumvuta mkono Guendouzi, but Guendouzi hakupaswa kuwa uwanjani pia kabla ya hilo tukio. So perhaps tuliozoea jiji tunasema ngoma draw!.

Chelsea tulifanikiwa kujenga momentum na counter iliyochezwa na Tammy Abraham wakiwa na Willian ilitosha sana kuwaangamiza Arsenal katika dakika ya 87 bao likifungwa na Tammy Abraham. Na mpaka dakika 90+7 zinakamilika Chelsea ilikuwa mbele kwa mabao mawili kwa moja na kuondoka ikiwa kifua mbele katika London derby

Na kwa maana hiyo Arsenal watauanza mwaka 2020 wakiwa umbali wa points 11 nyuma ya top four.

Kulikuwa na changes kadhaa kutoka katika kikosi kilichocheza Alhamisi ambapo Mateo Kovačić alirejea kutoka katika suspension na kuchukuwa mikoba ya Jorginho, huku Mason Mount akichukuwa nafasi ya Callum Hudson-Odoi katika ile front three.

Nafasi ya Fikayo Tomori ilichukuliwa na kinda Lamptey ikiwa ni debut kwa kijana huyo fresh kutoka Academy dakika 20 za lala unono. Callum Hudson-Odoi alimpumzisha Mateo Kovačić na team ikaanza kutumia formation ya 4-2-3-1.

Katika mchezo huu tumeshuhudia yellow cards tisa ikiwa ni cards nyingi zaidi katika Premier League msimu huu. Kutokana na Spurs kudondosha points mbili, Chelsea inajikita katika nafasi ya nne ikiwa mbele ya Manchester United kwa tofauti ya points nne huku Spurs ikiwa nyuma kwa tofauti ya points tano.

Next up: tutawatembelea Brighton siku ya Juma tano katika Premier League

KTBFFH

Sent using Jamii Forums mobile app
Emerson hakuwahi kuwa clinical kwenye krosi au pasi. Wakatri wa Sarri Emerson alikuwa mzuri kwenye kukaba na kupanda, ila Lampard alipokuja, Emerson amegeuka kuwa kama Alonso hasa kwenye kukaba. Mfano jana goli la Arsenal alitakiwa kumuwahi AUBA ila alikuwa slow na tukafungwa kwa namna hiyo. Magoli mengi Chelsea ina concede inatokmea kwake au pia timu kuzidiwa, kushambuliwa , counter attack inasabbishwa kwa sehemu kubwa na yeye.
Emerson ameprove hafai kwenye falsafa ya Lampard na kwa hiyo January auzwe, bora abaki Alonso atatufaa kwenye 3-4-3 na tukufanikiwa kumsajili LB mzuri Alonso atakuwa backup
 
Chelsea VS Arsenal 6-0 March 22 2014
  1. Goli la kwanza alifunga Samuel Etoo dk ya 5 tu
  2. Goli la 2 alifunga Schurrle dk ya 7
  3. Goli la 3 alifunga Hazard kwa penalti dk ya 17 baada ya mkwaju wake uliokuwa unatinga wavuni kulia mwa goli kudakwa na Alex Oxlade-Chamberlain
  4. Goli la 4 alifunga Oscar dk ya 42
  5. Goli la 5 alifunga tena Oscar dk ya 66
  6. Goli la 6 na la mwisho lilifungwa na Mo Salah dk ya 71 Goli la Salah ndio ilikuwa goli lake la kwanza kwenye jezi ya blue
  7. Mechi ilipoisha Asene Wenga hakumsalimia Jose Mourinho
LINE UP ILIKUWA HIVI
View attachment 1303640
Kabla ya kufunga decade ni vyema tukajikumbusha historia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom