Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Leo Lampard kabaatisha ktk mabadiliko aliyoyafanya kwa kurudisha formation ya 4-3-3
Kaona Emerson ni bomu la kuuza January, kasababisha goli liingie kiraisi
Jourginho ni muhimu sana Chelsea
Mimi likuwa kwenye kikao naibia kupitia live streaming wao walianza na 68% possession mara on target 2 mara goli dk ya 13 mara wanaendelea kutushambulia lakini baada ya dk ya 30 hivi nikaona mashambulizi hakuna tena kumbe kaingia mwenye timu Yaani Jorginho na Emerson OUT
Pia leo nimeshangaa kumbe Chelsea ina defender kijana kinda wa miaka 19 anaitwa Tariq Lamptey
Chelsea ina comeback ndani ya dk za hatari (Mimi huwa naona dk ikiishafika ya 80 ni hatari ambazo kurudi ni ngumu)
Goli la Tammy namfagilia Willian, speed na pass murua kwa Tammy ilisababisha goli japo naye Tammy kaonyesha kuwa bado yuko kwa kufunga goli zuri la 12 kwa EPL na 14 kwa mashindano yote
Well done Chelsea. Mmetufanya tumalize Krismasi na mwaka mpya vizuri
 
January si rahisi kuwa na usajili wa uhakika unless umsajili mchezaji aliyeisusia Timu baada ya kumfuata kwa muda mrefu kama VVD to Liverpool and Coutinho to Barcelona.
Hata bila usajili tutakwenda tu na tutamaliza top 4
Anayetuangusha ni kocha saa nyingine anwaingiza wachezaji kwa kuwajaribu akiwa na imani watacheza vizuri. Lampard akiijua 1st eleven na kuwapanga wachezaji wanaondana na formation, nafasi ya nne hata ya tatu tunaweza kamata
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom