CHELSEA 2-0 CRYSTAL PALACE, Premier League: Post-match reaction
By Mlanzi
Kuna mambo mengi sana ya kuburudisha ndani ya hiki kikosi chetu Chelsea, mpaka unashindwa uzungumzie ile attacking intercity ama uzungumzie zile young talents zinazozidi kutakata kila kukicha

. Hebu check kiwango cha Willian

; ukimaliza mcheck Christian Mate Pulisic anavyo sumbuwa

! Then mtazame Mason Mount alivyo threat

katika ngome za wapinzani; bila kumsahau Tammy9 Abraham anavyochana nyavu kila kuitwapo leo

. Ha haaaa kuna kitu nataka kusahau kuhusu Reece James

! Huwezi amini Zaha alitaka kuomba sub

;
Njoo kwenye Wizara ya ulinzi utazame ule msoto kati ya Kurt Zouma- na Tomori


! Vijana wapo dynamic wakaba kama siafu Zaha alipigwa tackle moja na Kurt Zouma akataka kulia

. Nimesema yapo mengi hata pale katika midfield chini ya mnyama N'goloKanté sambamba na Mateo Kovačić. Bench letu limekuwa na strength yani unatoa Tammy unaweka Mitchy Batshuayi, Unatoa Pulisic unaweka Cullum Hudson-Odoi unatoa Mason unaweka Gilmour

! Eti? Tupewe nini majamaa

!?
Okay ngoja tuwe serious kidogo. Pattern ya mchezo ilianza kuonekana sekunde ya kwanza kabisa baada ya Crystal Palace kuanzisha mchezo, na Chelsea ikaanza kuwin mpira, team ilikuwa inapeleka mipira mbele huku iki create chances japo ilibidi tusubiri mpaka second half kupata bao.
Chelsea tulipiga mashuti 11 katika first half, huku mawili pekee yakiwa on target, Crystal Palace walitumia muda wote langoni kwao na situation hii iliendelea hata second half, but crucially, Chelsea iliweza kupata breakthrough, kupitia kwa Tammy Abraham aliyefunga bao kutokana na flick iliyopigwa na Willian kutokana na kazi nzuri aliyoifanya Mateo Kovačić baada ya kuwagonga vyenga Crystal Palace alipopokea mpira wa kurusha.
Zikiwa zimebakia dakika 10 mchezo kukamilika, Chelsea tulipata bao la pili kutoka kwa Christian Mate Pulisic aliyefunga kwa kichwa.
Kwa matokeo haya Chelsea inapanda mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa League temporarily huku tukisubiri matokeo kati ya Leicester City dhidi ya Arsenal na hapo kesho Manchester City dhidi ya Liverpool pale Anfield.
Mpaka tunasema Job done.
Starting lineup ilikuwa (4-2-3-1)
Arrizabalaga | Emerson, Tomori, Zouma, James | Kovačić, Kanté | Pulisic, Mount, Willian (c) | Abraham
Kikosi kikiwa na changes mbili tuka katika game ya last weekend ambapo N’Golo Kanté alirejea kutoka katika injury na kuchukuwa mikoba ya Jorginho, huku Reece James akianza mbele ya César Azpilicueta.
Willian ilikuwa captain katika mchezo huu kutokana na kukosekana kwa Captain pamoja na Vice-captain
Kikosi chetu cha leo niyo youngest Chelsea starting lineup ever katika Premier League, na ni youngest for any team msimu huu.
Cesar Azpilicueta hakuwa katika lineup leo ikiwa ni mara ya pili katika 149 Premier League matches
Tammy Abraham amefikisha mabao 10 msimu huu na Christian Mate Pulisic amefikisha mabao matano katika matches 3 alizocheza katika Premier League games. Na huu ni ushindi wa 6 straight katika Premier League huku tukipata cleab sheet ya tatu straight katika Premier League
Next up: tunakwenda international break. Then Manchester City away!
KTBFFH