Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Vijana wamejitahidi second half, wanablues msife moyo timu itaendelea kuimprove
 
Lini Mane alikuwa na Bifu na Salah? Acha uongo! Hebu nenda kwenye Akaunti zao za Insta na Twitter ukaangalie kama wana bifu hilo unalolisema.

Washabiki wa Mane wa Afrika na Salah Waarabu ndiyo wanaoshambuliana Mitandaoni labda ndiyo bifu unalolisema.

Lakini wenyewe hawajawahi kuwa na Bifu Bali ni Best Friend.
Kwani likiwepo wataweka kwenye twitter???
 
Kwanza elewa kuwa Timu si Ndowa

Na hayo uliyoyasema yote kuwa Kante hana na ameridhika na Chelsea pamoja na London ni Maoni yako tu lakini si uhalisia kwani hujui noyoni mwake Kante anawaza nini? Ni yeye mwenyewe Kante ndiye anayewaza.

Kila Mchezaji anaposajiliwa na Timu Fulani basi husema ANAIPENDA TIMU HIYO NA YUPO PAHALA SAHIHI

Na ipo mifano wazi kwa baadhi ya wachezaji waliojisifia Timu kuwa Wameridhika nazo baadae Wakadai kuhama.

Mpira ni Biashara Ndugu! Hakuna asiyehitaji Hela!

Perezi akamuahidi Mshahara wa £350K na Mibonus ya kufa Mtu basi nayeye atasema kama alivyosema Hazard kuwa 'REAL IS MY DREAM TEAM'.

Tena wala usijidanganye kuwa karidhika na Maisha ya London! Mbele ya Pesa London inakuwa sawa na Gongolamboto.
Asiporidhika itaonekana tu kwa matendo au maneno, hiyo hakuna anayeweza kuficha
 
Nimekupiga kimyaaa
Mpige City tukuone kidume lakini wajanja wenzio wanaona gemu yetu ilikuwa nyepesi tu sababu ni kikosi B pia bado hakijazoeana sana.

Pili timu imejawa na majeruhi kibao, so weka akiba ya maneno ili uje uifunge Chelsea ikiwa haina sababu yoyote ile kujitetea lakini si sasa hivi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom