Mchezaji kuondoka kwenye timu kwenda nyingine kuna factor kama sita hivi
- Mtafutaji na mhamaji na tamaa tu, hana professionalism ndani yake mfano Sanchez kwenda Man U
- Haridhiki kuwepo kwenye timu yake ya sasa, mfano kutopewa play-time ya kutosha, posho, mkataba, usajili mbovu, sera mbovu nk
- Kutafuta changamoto kubwa zaidi mahali pengine
- Kwenda kwenye dream team mfano Hazard kwenda RM
- Kuwafuata jamaa na marafiki
- Mkataba kufikia mwisho wake - kuondoka kama mchezaji huru
Kante hayuko kwenye hizo sifa 5/6 hapo juu labda factor na. 5
Factor kubwa inayoipa au kuzipa timu nyingine nguvu ya kumfukuzia mchezaji ambaye wanamuona atawafaa ni factor na. 2, kulikuwepo na timu zilibip mwaka jana, nafikiri ni PSG lakini ndani ya no where walitulia tuli kwa sababu Kante ameridhika 99% kuwa Chelsea. Hii ya akina Hazard ni maoni yao tu
Kama Hazard ataweza kumuinfluence Kante na nguvu ya Hazard ikazidi marafiki zake walioko Chelsea na pia Maisha ya London kama inamboa yeye na familia yake anaweza kweli kwenda, ila sioni hilo kwa sababu Kante kajijenga na karidhika kuwa Chelsea na London.