Alichokifanya Kepa leo ni aibu kwa manager/coach Sari lakini zaidi pia ni aibu kwa club.
Nimekuwa nikisema hapa kwamba tatizo kubwa Chelsea ni club board.
Wachezaji wamepewa power kubwa mpaka wanafanya mambo ya kudhalilisha uwanjani. Na hata manager akichukua hatua utaona msukosuko unaanza kutokea kwa kocha. Huu upumbavu ni kama ule alioufanya Costa kwa Conte alafu kuna mazwazwa humu yakawa yanatetea ule upumbavu
Huo ujinga huwezi kumfanyia Guadiola, Wenger, Klopp, Pochetino, Mourinho au hata sir Fugerson ukabaki salama.
Club inapaswa kutengeneza mazingira ya kocha kuwa anaheshimiwa kama inavyostahili.
Alichofanya Keppa siyo profetional ni upumbavu mkubwa. And I guess ujinga kama huu kuna muda unafanyika huko nyuma ya camera japo hatuoni.
Bodi yenyewe ya kihuni. Kocha anaweza kubeba ubingwa ila akishindwa mechi 2/3 washaanza kuruhusu tetesi kwamba kocha atafukuzwa. Hakuna hata mtu kwenye bodi anasimama kumtetea kocha dhidi ya vyombo vya habari vya kiingereza.
Itafika mahali makocha makini kama Pep Guadiola, Pochetino, Zidane, na makocha wenye kariba kama yao watashindwa kuja kufanya kazi na Chelsea hii ya sasa. Maana haina heshima kwa makocha
Lastly mnapaswa kuelewa Chelsea ilipokuja imezifunika club pendwa za kiingereza na kuipa man U ushindani mkali. Lakini pia mmiliki Wa Chelsea ni mrusi na Urusi ina mahusiano mabaya na Uingereza. So waingereza wengi wako against Chelsea na wanaichukia sana. Kwa hiyo ni lazima media nyingi ziko against Chelsea. Guadiola alifungwa msimu wa 2016/2017 lakini sikusikia tetesi za kufukuzwa.
Sent using
Jamii Forums mobile app