Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Kwa msomu uliopita Matic na Costa walikuwa nguzo ya muhimu katika ushindi wetu.
Pedro, Cahili, Luiz, Moses, na hata Hazard wameshuka viwango vyao tofauti na mwaka jana. Na hata Willian amefanya vizuri katika mechi hizi chache za Mwisho.

Kwa hiyo kosa kubwa la Chelsea lilikuwa kumuuza Matic na kushindwa kufanya replacement Nzuri ya D. Costa.

Kwa anayengalia vizuri anaweza kuona kuwa katikati Chelsea inavuja na kwa karibuni Christensen anafanya makosa yenye kutugharimu.

Let's hope kwamba bodi, na technical benchi watalifanyia kazi
Finally mwisho wa msimu mnakubali mwanzo mlikuwa mnakataa
 
Matic kauzwa na bodi. Luiz alipata injury na hata baada ya mgogoro alicheza mechi mbili. From there ameugua goti, sasa unatakaje hapo? Costa tu ndo kafukuzwa na Conte. Alafu alikuwa anajiona mkubwa kuliko timu. Mpaka siku nyingine abembelezwe ndo acheze, kesho atakwambia anataka kwenda China na utovu wa nidhamu kibao. Kama kocha alipaswa kumdeal hata kama hatua aliyochukua haikuwa nzuri.

Makocha bora wote wanadeal na nidhamu ya wachezaji. Kosa la Chelsea na si Conte peke yake ni kukosea kufanya replacement ya Matic na Costa.
Wachezaji wote wanauzwa/kununuliwa baada ya bodi kukubali msimu ulivyoisha Conte alitaka klabu imsajili DM kijana asaidiane na Matic sababu umri wa Matic ni mkubwa baada ya Bakayoko kusajiliwa Matic atajua nafasi yake kucheza itapungua akaomba kuondoka bodi ikaridhie auzwe.

Nidhamu ya Diego Costa uwanjani haijaanza msimu uliopita na haitaisha ndio alivyo hata tangu akiwa Atletico na enzi za Mourinho timu ikimtaka mchezaji huwa ina-disturb mind yake so makocha wengi huwa anamweka mchezaji benchi hadi saga liishe (LVG alifanya kwa De Gea,Klopp alifanya kwa Coutinho,Wenger alifanya kwa Sanchez) baadae saga likiisha unamrudisha mchezaji kwenye timu
 
Oyaaa inabd Leo tuue uyu soton tuingie big4 nani kasema Europa inatuhusu
This is chesi bana tunagawa dozi akuna cha MATIC wala Costa
Game zijazo zote tunaua wa2 alafu manure na toti watapoteza alafu tunaingia big4
Inabidi mjitengenezee come back yenu Leo, ama sivyo mnarisk kuikosa hata hiyo Europa.
 
Asikwambie mtu Chelsea ya mwaka huu itakuwa hatari zaidi kuliko ya mwaka jana. Sote tunakumbuka kuwa Chelsea ilikuwa na kikosi bora kuliko timu nyingine yoyote ya EPL. Hata katika PFA premier league team of the year Chelsea ilikuwa na wachezaji 4 ambao ni Luiz, Cahill, Kante na Hazard na wotehawajauzwa, wamebaki kwenye timu.

Timu pekee iliyoingiza wachezaji wengi nyuma ya Chelsea ni Tottenham iliyoingiza wachezaji 3; Kayle Walker, Dan Rose na Harry Kane.

Timu nyingine zilizobaki ziliingiza atmost mchezaji mmoja mmoja. Man U waliingiza goalkeeper De Gea, Liverpool Sedio Mane, Everton Lukaku na Arsenal hawakuweza kumwingiza mtu yoyote.

Kwa hapo juu inaonekana Tottenham ndo ina wechezaji wengi walioingia katika PFA team nyuma ya Chelsea..

Lakini ikumbukwe pia Kayle Walker tayari ashauzwa Man City na Dany Rose anawindwa sana na Chelsea. Kwa hiyo katika ile list wanapunguza idadi ya wachezaji na ikumbuke kuwa Tottenham haijanunua wachezaji wapya msimu huu.

Sasa unaweza kuanza kupata picha kwa nini nasema Chelsea itakuwa timu tishio zaidi.

Chelsea imemuuza Matic na kumnunua Bakayoko ambaye kiwango chake ni kizuri zaidi. Diego Costa naye ni surplus to requirement na Morata amekuja kuziba pengo lake na naamini muda si mrefu mashabiki wa Chelsea wataacha kum-miss Diego Costa. Lakini pia imeingeza makali ya safu ya ulinzi kwa kumnunua Antonio Ludiger.

Wengine waliouzwa walikuwa reserve ya timu ambao wengi wao ni vijana wadogo ambao wameondoka kwa mkopo kwenye club nyingine ili waive zaidi.

Chelsea haijaishia hapo ila tajiri Abramovic atatoa about £130, 000,000 (£ 130 million) kwa ajili ya kuimarisha kikosi na wachezaji walio katika rada ya Chelsea ni Van Dijk ambaye Chelsea iko tayari kutoa £50M/Dan Rose, Ox Chambalein, Dan Drinkwater na wengineo.

Hivyo waweza kuona jinsi Chelsea itakavyokuwa timu hatari zaidi katika msimu huu kuliko msimu uliopita.

Chelsea lazima ifanye maajabu msimu huu

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu sio wewe
 
Kwahyo tunaamuaje sasa wakazi wa shithole country kuhusu comparison ya morata na lukaku?
 
Tatizo si pesa wala uwanja. Angalia usijiri wa mwaka Jana.
Morata -£56M
Bakayoko -£40M
Ludiger- £30M
Zapacosta - £22M
Drinkwater- £18M
Barkley- £15M
Emerson-£17.6M
Giroud -£18M
Jumla ni £ 233,000,000

Hivi EPL nani katumia kiasi hicho cha pesa kwa msimu huu kwenye usajili?

Ni Man City pakee ndo katumia pesa nyingi kusajili kuliko Chelsea. Kwa Ulaya nzima ni Man City, PSG na AC Milan tu ndo walitumia kiasi kikubwa kuliko Chelsea.

Sasa hapo shida ya pesa iko wapi?

Tatizo Si Last season wala season Hii muliyojenga Uwanja! Uwanja Unataka Kuanza Sasa! Hapo Ndiyo Shida Yote inapoanzia Kwenye Matumizi Kwani Bajeti iliyopita Haikuathiriwa na Gharama za Ujenzi Wa Uwanja, Bali Bajeti ya Next season ndiyo itakuwa affected na Project ya ujenzi Wa Uwanja.
 
Ligi ya England na Chelsea wanavyocheza wanahitaji striker mwenye nguvu mpiganaji ndio maana (Drogba na Costa ) walifanya vizuri
Hizi projects za Chelsea ni unsustainable. Kila kocha anahitaji wachezaji wenye character Fulani kutokana na style yake ya kujenga timu.

Sasa huyu bwana conte akiwa katikati ya kutengeneza team tayari anahofu ya kuondolewa, hawezi Fanya kitu.

Msimu wa kwanza alifanikiwa sababu alilazimika kufanya kazi na timu aliyoikuta,

Hilo lundo la wachezaji alioleta inahitaji muda kuwafanya wawe team
 
Oyaaa inabd Leo tuue uyu soton tuingie big4 nani kasema Europa inatuhusu
This is chesi bana tunagawa dozi akuna cha MATIC wala Costa
Game zijazo zote tunaua wa2 alafu manure na toti watapoteza alafu tunaingia big4
Kweli mnamfanyia ukatili soton. Futui inawahusu tu msimu ujao
 
Hizi projects za Chelsea ni unsustainable. Kila kocha anahitaji wachezaji wenye character Fulani kutokana na style yake ya kujenga timu.

Sasa huyu bwana conte akiwa katikati ya kutengeneza team tayari anahofu ya kuondolewa, hawezi Fanya kitu.

Msimu wa kwanza alifanikiwa sababu alilazimika kufanya kazi na timu aliyoikuta,

Hilo lundo la wachezaji alioleta inahitaji muda kuwafanya wawe team

Conte alichukua ubingwa na foundation aliyoijenga Mourinho na walikuwa hawana michuano ya ulaya ukilinganisha na competitor wenzake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom