Maneno ya Shukrani ya DrinkWater kwa Washabiki wake.
Kupata mafanikio tuliyoyapata na Leicester city iikuwa ni maajabu, itakuwa kumbukumbu yangu ya milele. Haikuwa rahisi kwangu. Kulikuwa na changamoto nyingi mno kufikia mafanikio hayo, lakini watu wa karibu yangu walinisaidia na hili sintalisahau kamwe.
Ilikuwa uamuzi mgumu sana kwangu kuondoka, lakini binafsi niliona ni wakati muafaka kwangu kufanya hivyo. Ukishapata mafanikio makubwa kama tuliyoyafikia pamoja na wenzangu, inaleta chachu – unahitaji kuyapata mafanikio kama hayo sehemu nyingine pia na hii niliona ndiyo fursa pekee kwangu kutimiza ndoto hiyo.
Huwezi kujua fursa huja mara ngapi maishani kwako, kwangu mimi niliona hii ni fursa pekee na ilikuwa vigumu kuiacha ipite.
(Maneno haya yamenigusa sana - karibu darajani Jembe jipya) -
Its now chance to see our dream combination with N'Golo Kante.