Kaka Chelsea wanacheza mfumo wa 3-4-3, huo mchezo unabadirika kulingana na mazingira, kama tunashambuliwa kwa shabulizi la kawaida na la mpito, basi mfumo unakuwa 4-3-3, beki zinakuwa nne, Alonso Kushoto, kati Luis na Cahil na kulia ni Azip, na katikati kunakuwa na Matic, Kante na Victor moses na mbele kunakuwa na Willian, Hazard na Costa
Tukiwa tunashambuliwa kwa muda mrefu na timu inazidiwa basi mfumo unabadirika na kiwa 5-4-1, nyuma kunakuwa na beki tano, Luis, Azip, Cahil, Alonso na Victor moses, katikati tunakuwa na Matic, Hazard, Kante na Willian na mbele anabaki Costa kusubiri counter attack.
Tukiwa tunashambulia kwa kujihami, yaani mechi iko 50:50, mfumo unakuwa 3-4-3, na tukiwa tunatawala mechi basi mfumo unageuka na kuwa 2-3-5 yaani hapo lazima ufungwe, nyumba anabaki Azip na Cahil, kati anasogea Luis, Matic na Konte mbele kunakuwa na Victor, William, Hazard, Costa na Alonso
Huo ni mfumo mzuri sana, sema unahitaji wachezaji wepesi, inahitaji wachezaji wenye uwezo wa kuhold Mipira na wachezaji wenye skill zakufunga