Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Shabiki usiyekuwa na team maalum naona una sherehe kubwa mno! Kumbe ulikuwa unamuhofia sama Mourinho eeeh!? Weka akiba ya maneno huenda Mou akatua kwenye moja ya team zako.
Akija Mou kwenye moja ya team zangu nahama siku iyo hiyo. Mou hafundishi mpira anafundisha wachezaji kuwa wahuni uwanjani na boring football. Mimi ni mpenzi wa total football, sipendi kabisa aina ya mtindo wa Mourinho.

Mou anapoenda popote anaharibu mpira. anashinda vikombe at the expense of utamu, chenga twawala na flamboyance. Je ni kosa kushabikia a cluster of teams? Usiweke mayai yote kwenye kikapu kimoja. Hiyo nayo ni falsafa ya upenzi wa soka, usilazimishe unazi. Haya mfuate Mou huko aendako.

Mfalme... sio mimi niliyemfukuza Mou ni Abrahamovich yule mafiaso wa kirusi..mimi sicheki wala sifurahi, nakenua tu kwa mshangao.
 
mi naona hapa kama tunatofautiana, mi naona ufundishaji wake, mana mi alianza kuniboa tokea game la stoke city game la Capital one, stoke city walikua pungufu kwa red card eti badala ya kucheza mpira wa kushambulia eti ndio kwanza wanaforce game liishe droo wakati penalt hainaga mwenyewe, uwe pungufu dhidi ya man city au baca utajutaa .........
kwanza timu ilikua inacheza haishambulii, wachezaji hawawezi kupiga penetration pass, wao ni V pass, wanapasiana mabeki kwa mabeki theni wanamrudshia kipa abutue mbele. sasa vile walivyokua wanacheza si ndio kocha kawafundisha hivyo.
Angalia kocha kama Gudiola anavyofundisha, mchezaji anapewa mpira, halafu anakua na option kama ya wachezaji watano hivi ya kuwapasia mipira, kwa wachezaji wa chelsea option ni kumrudishia kipa!, aondoke tuuu!
It is too late. Sisi wengine tulipokuwa tunasema haya, ulikuwa unakuja na vijineno vya utoto wako. Leo domokaya ametemwa unakiri kuwa jamaa alikuwa bogus. Tukueleweje dogo?

sasa unabaki Ze blauz au unamfuata Mou huko aendako kama Ntuzu?

Heshima kwa Root. Alipotoa maoni yake kwa ukweli na uwazi kama che nkapa mlikuwa mnamwita shabiki maandazi. Root ukuje huku uone hawa walikuwa wanakupiga madongo wamebadilika rangi sasa.

Mentor lete katuni za Moureen sasa.
 
Mou ni best kocha kasoro moja tu ya kuongea sana ndo ilifanya asipendwe na timu pinzani ila ukweli utabaki ni best kocha, poleni sana na bandugu wapenzi wa Mou Ntuzu na Mentor..... Root toka mafichoni umeshinda kesi.

Nimepokea hizi taarifa kwa uchungu mkubwa sn hasa ukinzingatia hii wiki tumempoteza mwenzetu Dotto Mnzava......

Kila mmoja najua atasema lake kadri awezavyo..... Lkn ukweli utabaki kua Mourinho ni kocha bora na kwa Chelsea hakuna kocha atakaekuja kufikia record yake.

Sababu iliyomfanya Jos? kufukuzwa ni kuinusuru timu kwani ata km angebaki kua pale bado wachezaji wangemuangusha tu hasa kutokana wao kuamua kwa makusudi kumuangusha kocha wao. Sasa timu inapofika ktk wakati huu ni bora kumpumzisha kocha ili kuleta kocha mwingine ili kuleta maelewano kati ya wachezaji na kocha na kupelekea timu kufanya vzr. Ni mshukuru sn Mourinho na kumpongeza ktk hilo alikua akijaribu kujenga mahusiano mazuri pamoja na hujuma za wazi zilizokuwa zikiendelea.

Mourinho kafukuzwa sio km yeye ni kocha mbaya.... Kafukuzwa kwasababu mahusiano yake na wachezaji yamekua mabaya na kamwe yasingeweza kua mazuri hasa kutokana na hujuma kupenyeza kutoka FA, Media. Waamuzi na wadau wa mpira wa wa England kuhakikisha kua hafanikiwi ktk wakati huu.

Kocha yoyote atakaekuja hatoweza kuinusuru hii timu kwa wakati huu..... Ila Jos? km angepewa nafasi hadi January basi angeinusuru hii timu.
Aleyn na Kituko nimeona michango yenu.....nyie mnatambua mpira na hali halisi ya makocha na wachezaji na soka kwa ujumla. Hoja zenu zina mashiko sn.
ENZO sijaona point yoyote nzito ktk hoja yako. Nachoweza kusema ni kwamba umetoa dukuduku lako.

Mwisho nakushukuru sn everlenk kwa kuniita. Mimi nipo na daima nitabaki kua Chelsea fans mpk kufa. Na Mourinho popote pale alipo nami nipo. Mourinho will simply remain the best.....

Jingine EPL inakwenda kupoteza mvuto, ushindani na mashabiki hasa kutokana na hamasa za Mourinho kukosekana ktk hiyo ligi. Sioni hamasa na mvuto na ushindani kwa Wenger, Pellegrine, LvG au Klopp.

#KTBFFH.......

#holler.
 
Last edited by a moderator:
Cesc Fabregas
 
Attachments

  • 1450399870987.jpg
    1450399870987.jpg
    47.8 KB · Views: 221
Hujajiuliza kwanini klabu kubwa kama madrid wanamtaka, watu wa mpira huwa wanaelewa fitna za kwenye mpira

Kutakiwa na Madrid sio issue kwani ataenda kufundisha misimu 2 then atafukuzwa,Kwa sasa Jose hakuwa kocha sahihi kufundisha Chelsea
 
Ajiuzuru akose ?40mil??

Huenda akalipwa less than ?40 mil kwani
1.Ameshindwa kuiongoza timu kufikia viwango vya Chelsea,sio level yao kupambana kutoshuka daraja

2.Ugomvi wake na Dr Eva Carneiro umesababisha klabu ishtakiwe na hii imeharibu image ya klabu na huenda klabu ikaadhibiwa
 
Katika kipindi ambacho nimeumia sana basi ni Jana kusikia Mou kafukuzwa kwa kweli nahisi some betrayal inside the cabinet. Hii siyo haki kabisa

cc Ntuzu kalou
 
Mara nyingi hua nakuona unotoa hoja za mashiko lkn ktk hili naona unaongea tu km wewe binafsi una chuki tu na Mourinho.

Km Chelsea wasinge muhitaji Mourinho basi asingeondoka Madrid kwasababu aliondoka Madrid si kwa kufukuzwa.
 
Katika kipindi ambacho nimeumia sana basi ni Jana kusikia Mou kafukuzwa kwa kweli nahisi some betrayal inside the cabinet. Hii siyo haki kabisa

cc Ntuzu kalou

Mkuu ni shida.....

Baada ya Mourinho kufukuzwa baadhi ya wachezaji wamesema wazi kutaka kuondoka na kuachana na Chelsea na soccer la Uingereza kwa ujumla..... Hii hali itaighalimu sn timu.
 
Last edited by a moderator:
Ifikie sehemu makocha waikatae hii timu ili wachezaji wajicoach wenyewe, toka Mou ameondoka mara ya kwanza kuna makocha wazito sana wenye uwezo wamefukuzwa kwa sababu za kutoelewana na wachezaji.

Kuna wachezaji kama Terry na kundi lake nadhani ifikie muda wapumzike, kwa sababu nadhani ndo wanaoleta influence.

Kama timu haitakaa iwaondoe wachezaji hao hakuna kocha atakaye kaa Chelsea na tajiri ataendelea kupoteza hela.
 
Dah!!!! Kwa kweli inaumiza sana kocha bora kama mou kufukuzwa kisa upumbavu wa wachezaji.... Halafu hatutapata kocha mwenye mapenzi na club kama mou, wakati anaondoka Cobham baada ya kutimuliwa alikuwa akimwaga machozi masikini... Halafu kuonesha kuwa anaipenda club zile hela alizotakiwa kulipwa amesema zitumike kurebuild club, for sure mou was the best man for the job, gone but never forgotten!!!!!!!😿
 
Terry anapaswa kuondoka......

Hii ndio michango bora kabisa yenye mashiko sio watu wanakuja kubwabwaja yao hovyo tu km wamevurugwa.

Salutes kwenu wakuu.
 
Terry anapaswa kuondoka......

Hii ndio michango bora kabisa yenye mashiko sio watu wanakuja kubwabwaja yao hovyo tu km wamevurugwa.

Salutes kwenu wakuu.

Wote kina Scolari, Ancheloti, AVB na sasa Mou wamekutana na huu ujinga wa kina JT.

Bila JT kuondoka, tena na baadhi ya wachezaji wanaomtii, Chelsea haitakaa ipate kocha wa kudumu.
 
Wote kina Scolari, Ancheloti, AVB na sasa Mou wamekutana na huu ujinga wa kina JT.

Bila JT kuondoka, tena na baadhi ya wachezaji wanaomtii, Chelsea haitakaa ipate kocha wa kudumu.

Atarudi hapo akiwa na timu ingine na kuifunga Chelsea km alivyokuja na inter Milan na kuitupa Chelsea nje ya UEFA.
 
Watu walikuwa wakimsema sana Mourinho kuwa hafai na kumbeza! Sasa kama Mou mliona hafai na ni kocha wa kufungwa tu hasa msimu huu iweje leo mfurahie kufukuzwa kwake? Si mgependa aendelee kuwepo ili mumfunge tuu kama mnavyojiaminisha?

Kitendo cha baadhi ya HATERS kufurahia kufukuzwa kwa mou kinaonesha wazi kabisa ni kwa kiasi gani Mou alikuwa akihofiwa kimafanikio,

Tatizo la Chelsea halikuwa Kocha bali "hujuma" ya wachezaji wasio na mapenzi ya dhati na team,jaribu kufuatilia ili kujua Matokeo mabovu kwa Chelsea yalianza kipindi gani?

Nenda Kocha wangu Mourinho baadhi ya watu hawakupenda mafanikio yako,

Kwa staili hii team za Uingereza zitaendelea kuburuzwa sana tu na team za ligi zingine Ulaya na hasa Spain mpaka mwisho wa Dunia,

EPL imejaa majungu na fitina zaidi na hiyo ni sumu kali sana katika maendeleo ya soka kwa ujumla.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom