Chama cha Wamiliki Mabasi (TABOA) kusitisha kutoa huduma kuanzia Jumatano wiki ijayo kwa kugomea mfumo wa ukataji tiketi kupitia mtandao

Huo mfumo kwa wapigaji aka vishoka ndo imekula kwao hakuna kupiga hela sahv,
Mnaboa mno watu wa kariba yako roho mbaya hivyo inakusaidia nini mzee baba?watu wakikosa hela wewe furaha yako ni nini hapo unaweza kuta hata v8 la serikali hujawahi kupanda acheni unafiki ndugu zanguuuu
 
Inabidi mbinu za medani zitumike kudhibiti viongozi wa hii kitu maana ni kama wanaona wana haki ya kupata pesa bila kulipa kodi.

Agent pekee ana uwezo wa kupata hadi elfu 60 kwa siku kwa mwezi 1.8M ila hawalipi PAYE hata senti tano.Mtumishi ana mshahara wa laki 5 analipa sio chini ya laki 6 kwa mwaka.Imefika wakati wa kuhakikisha hawa watu wanadhibitiwa kabla ya kuumiza wananchi
 
CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), kimetoa siku tatu kwa mamlaka zinazohusika na mfumo wa mashine za kukatia tiketi kwa njia ya mtandao (POS), kutatua changamoto zinazoukabili “lasivyo hatuteweza tena kutoa huduma.”

Taboa wanalalamikia mfumo huo wakidai si rafiki na kuitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra), kuachana na mfumo huo kwani unawasababishia hasara.

Uamuzi huo, wameutoa leo Jumamosi tarehe 6 Machi 2021, katika kikao cha dharura cha wamiliki wa mabasi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

“Leo tarehe 6 Machi 2021, Taboa tumefanya mkutano mkuu wa dharura juu ya changamoto zinazotokana na mfumo huu ambao si rafiki wa POS, kumekuwa na faini za kila leo kutoka Latra bila kujali changamoto za mfumo.”

“Latra imekuwa ikifungia magari ya wamiliki wanaoshindwa kutumia mfumo bila kutatua changamoto za mfumo husika,” amesema mwakili wa wamiliki hao, Max Komba

“Hivyo basi, kwa kauli moja wanachama wameazimia kuwa, kwa kuwa mfumo wa kielekoniki si rafiki ni kandamizi, wasafirisgaji watashindwa kutoa huduma na tunatoa siku tatu kwa mamlaka kutatua changamoto,” amesema.


Mwanahalisionline
 
Hawa wa mabasi huwa wanaishia kutishia nyau tu kisha wanaufayata.

Inabidi wakaze maana dona kantri inawafyonza Sana na kuharibu kabisa biashara ya mabasi.
 
Razima turipe kodi hii ni vita ya kiuchumi ...

Mabeberu wanatouone wivu....

Nasema uongo ndugu zangu?
 
Wakigoma futa leseni na mabasi yasimame!! Kodi lazima ilipwe na kila mwenye kustahili, wafanyakazi wamekuwa wakilipa kodi kwa kiwango kikubwa kuliko wafanyabiashara wakubwa!!

Wakati huo huo kama kweli mfumo haufanyi kazi, urekebishwe!!
 
Mabus ndio sehemu ya kupigia Pesa kina eddo walizipiga kupitia speed governor sijui zilipotelea wapi.Wabongo wakaja na ubunifu wa kuongeza urefu wa accelerator yaani unakanyaga ikizama inagusa speed governor kwa mwendo huo huo.
 
Wakigoma futa leseni na mabasi yasimame!! Kodi lazima ilipwe na kila mwenye kustahili, wafanyakazi wamekuwa wakilipa kodi kwa kiwango kikubwa kuliko wafanyabiashara wakubwa!!

Wakati huo huo kama kweli mfumo haufanyi kazi, urekebishwe!!
Unachanganya desa wewe...

Hawajasema tatizo ni kulipa kodi. Hawesemi kuwa hawatalipa kodi...

Tatizo lao liko katika mfumo wa POS kutofanya kazi inavyopaswa...

AMA

Mfumo kuwa na kasoro za makusudi ili mradi tu wapate makosa ya kumtoza faini mmiliki wa gari/bus ili tu serikali ipate fedha haramu ya mapato ili kufanya ifanyayo...

Hiki ndicho kilio cha kila mtu toka kwa serikali hii inayoongozwa na CCM ya Magufuli...yaani kodi kandamizi, faini kandamizi na zisizo halali kwa vipimo vyote...!!
 
Alafu na nyie TABOA mambo ya kusimama sehemu ambazo chakula ni ghali muache kenge nyie yaaani chips na upaja wakuku na Pepsi unaambiwa jumla 18k aisee endeleni kuringa siku SGR ikienea mikoa yote mtakula jeuri yenu
 
Wakigoma futa leseni na mabasi yasimame!! Kodi lazima ilipwe na kila mwenye kustahili, wafanyakazi wamekuwa wakilipa kodi kwa kiwango kikubwa kuliko wafanyabiashara wakubwa!!

Wakati huo huo kama kweli mfumo haufanyi kazi, urekebishwe!!
Hao wakigoma hakuna rangi wataacha kuona KAMATA/UDA itafufuliwa upya wakati mabasi Yao yanaota kutu yard. Zama za kutishia zilikwisha kitambo. Wajifunze kusoma nyakati. Kiroho Safi nawashauri wasijaribu. Hakuna aliyewahi kugoma akafanikiwa miaka ya karibuni. Narudia, hayupo
 
Labda wana point za msingi kwenye lalamiko lao wasikilizwe na ubabe usitumike...
 
Back
Top Bottom