SoC03 Mfumo mmoja wa ukataji tiketi mtandao kwa mabasi ya mikoani

Stories of Change - 2023 Competition

IFAC

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
3,626
9,146
Hakuna kitu kinachotesa na kuumiza kichwa kama unapohitaji kukataa Tiketi ya basi ili usafiri kutoka mkoa mmoja mpaka mwingine.

Unapotaka kufanya hivyo unakuta mifumo yao sio rafiki na kila kampuni imeanzisha tovuti (website) yake.

Tovuti zao sio rafiki kwa watumiaji na nyingine huwezi kuzitumia kabisa mpaka uende kwa wakala wa hayo mabasi.

Wakati lengo la uanzishwaji wa ukataji tiketi mtandao ilikuwa kumuwezesha mteja( Abiria) kuweza kupata huduma akiwa eneo lolote na kuchagua siti yake bila kulazimika kukutana na wakala au vishoka.

Sasa inabidi serikari ione umuhimu wa kuanzishwa kwa website Moja ya ukataji tiketi kwa mabasi yote nchi nzima.

Hiyo website iwe na mfumo rahisi wa malipo.

Huo mfumo wa malipo uwe integrated na mitandao ya simu iliyopo nchini.

Iwe rafiki na rahisi kuzitumia hata kwa maamuma.

Kila kampuni ya basi itakuwa na nyuzi yake (Section)

Kila route itaonyesha kiasi Cha Nauli hadi anaposhuka Abiria.

Kila basi watakuwa washaliweka kwenye hadhi yake na gharama halisi ya nauli yake
Mfano:
1)Anasa (Luxury)
2)Nusu Anasa(Semi Luxury)
3) Kawaida(Ordinary)

Tofauti na Sasa ambapo gari lenye hadhi ya Ordinary unakuta mteja analipishwa hadhi ya Luxury.

Gari zenye hadhi ya Semi Luxury nalo linalipisha wateja Luxury.

Itasaidia kuondoa ama kuwapunguza wapiga debe kwenye vituo vikuu vya mabasi na kero zao.

Hakuna mtu asiyejua kero ambazo abiria mbalimbali hupata wakiwa Nyamngholo, Nane Nane au Stendi ya Magufuli.

Hivyo mfumo huu unaweza kuondoa ama kuwapunguza maana Sasa Abiria wanaweza kukataa Tiketi wakiwa mbali kabisa na eneo la Stendi,

Hivyo kufanya uwepo wao kutokuwa na maana.

Usimamizi, uboreshaji na miongozo yote ya mfumo huu itasimamiwa na mamlaka za kiserikari hivyo kuwa salama mbali kabisa na hujuma.

Serikari kupata Kodi stahiki maana itajua kiasi Cha pesa kilichokusanywa na kila gari na kila kampuni.

Serikari kujua idadi kamili ya wasafiri kwa wiki, mwezi au mwaka kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Kuboreshwa kwa huduma za Magari maana gari lisilo na viwango litafungiwa Moja kwa Moja.

Hivyo mfumo huu utasaidia kuondoa usumbufu na sintofahamu iliyopo sasa.
View attachment 2699186
Chanzo mtandao wa kitabu sura
Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom