Doria ya Mabasi ya Abiria kufanyika kwa saa 24 Barabarani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Jeshi la Polisi limetoa maagizo kwa makamanda wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanafanya doria katika barabara zote zitakazotumiwa na mabasi yatakayokuwa yanafanya safari zake saa 24 katika kudhibiti aina zozote za kihalifu.

Huo ni utekelezaji wa agizo lilotolewa, Juni 28, mwaka huu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa akitoa hoja ya kuahirisha Bunge la Bajeti jijini Dodoma.

Alisema mabasi sasa yameruhusiwa kuanza safari zake usiku kwa sharti la wamiliki kuomba vibali.

Itakumbukwa mwaka 1992, aliyekuwa Waziri Mkuu, John Malecela alisisitisha rasmi safari hizo kwa mabasi yote nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam kwenye mkutano na vyombo vya habari, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadhi Juma Haji alisema makamanda hao watapaswa kushughulika zaidi na madereva wote watakao kuwa vinara wa uvunjaji wa sheria.

“Makosa hayo ni mwendokasi na kuyapita magari yaliyo mbele yao katika maeneo yasiyoruhusiwake. Watakabainika wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali ikiwemo kufungiwa leseni, tunataka madereva wenye nidhamu barabarani,”alisema.

Alisema kwa kuwa mabasi hayo yatakuwa yanasafiri usiku, madereva wanapaswa kuwa makini hasa kwa baadhi ya maeneo yenye barabara finyu, maeneo ya misitu minene, kona na giza kali.

Kamanda huyo alisema maeneo hatarishi yote yaliyobainishwa ikiwemo mlima Kitonga na yale yenye misitu mikubwa, polisi watakuwa wanafanya doria na operesheni za mwendelezo.

“Maeneo ambayo mara nyingi madereva huvunja sheria za usalama barabarani kama yenye miteremko inayosababisha ajali hasa usiku, yatakuwa kwenye uangalizi mkali na askari watakuwepo muda wote,”alisema Awadhi.

Ujumbe kwa abiria na wasafirishaji

Alisema ni wajibu wa watakaosafiri na mabasi hayo, kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kutoa taarifa watakapobaini kuna uvunjifu wa sheria utakao fanywa na madereva.

“Abiria wana nafasi kubwa ya kuona mwenendo wa madereva, wakiona mwendo ni hatarishi kwao, wasisite kutoa taarifa haraka ili hatua zichukuliwe kwa dereva husika,”alisisitiza.

Kuhusu wamiliki wa mabasi na wasafirishaji wengine, Kamishna Awadhi alisema wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia vyombo vyao vya usafiri pamoja na madereva watakaokuwa wanaendesha huku akieleza kuwa wanao huo wajibu wa kuona sheria za usalama barabarani zikizingatiwa.

“Mmiliki au msafirishaji asije akabweteka akifikiri ni jukumu la Jeshi la Polisi peke yake, kwani anao wajibu wa kuona chombo chake kinachotoa huduma ya usafiri na dereva aliyepewa chombo, anasimamia sheria,”alisema.

Alisema wamiliki wanalojukumu la kuhakikisha wanawasimamia madereva wao wanakuwa na utimamu wa afya zao na kuwa na leseni zilizotolewa na mamlaka husika.

Wito kwa madereva

Alisema madereva watakaokuwa safarini hasa kwa wale wa masafa marefu, watapaswa kuwa na siha njema na utimamu wa mwili.

“Tunataka wawe na wajibu wa kufuata sheria za usalama barabarani kama walivyofundishwa darasani kwa maana anapokuwa barabarani takiwa na usukani, aongozwe na sheria,”alisema.

Latra kutoa ratiba

Awali, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra), Habibu Suluo alisema wataanza kutoa ratiba ya safari za mabasi hayo , baada ya kufanyika kwa kikao baina ya Wizara ya Mambo ya Ndani na ile ya Uchukuzi.

Wizara hizo zimeagizwa kukaa na kuweka mkakati unaokwenda kutekelezwa pindi safari hizo zitakapoanza hivi karibuni.

"Hatuna kipingamizi, tunachosubiri ni hicho kikao kifanyike, tutaanza kutoa ratiba inayoonyesha utaratibu mzima utakavyokuwa," alisema Suluo.

Mabasi ya Newforce kusitishiwa ratiba za usiku

Katika hatua nyingine, Saluo alisema Latra imesitisha ratiba za mabasi 38 ya Kampuni ya New force yaliyokuwa yanafanya safari zake kuanzia saa 9:00 na saa 11 alfajiri na kurejeshwa saa 12:00 asubuhi.

Alisema kuanzia kesho, mabasi hayo yataanza safari zake saa 12:00 asubuhi na kuendelea.

Alisema hiyo ni baada ya mabasi matano ya kumpuni hiyo kupata ajali mfululizo ndani ya wiki nne.

Hata hivyo, alisema hiyo si adhabu, bali ni utaratibu wa kutaka kudhibiti hali hiyo na kuhakikisha usalama wa abiria.

"Kutokana na wimbi la ajali kwa mabasi haya, tulifanya uchunguzi na kubaini uvunjaji wa sheria kwa makusudi unaofanywa na madereva wake ndiyo umechangia kutokea kwa ajali hizi, hivyo tumesitisha ratiba zao za usiku na kuzirudisha zianzie Saa 12:00 asubuhi,” alisema.

Akizungumzia hilo, Meneja wa Kampuni ya New Force, Masumbuko Masuke alisema kabla ya mamlaka kusitisha ratiba yao, nao pia walipanga kupunguza magari ili wafanye tathimini.

"Hizi ajali zilizotokea zimetupa hasara kubwa, tulipanga kuanzia Jumamosi ijayo tupunguze mabasi tubakiwe na machache tutakayo mudu kuyasimamia," alisema Masuke.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri (Latracc) Ngowi Leo alisema hatua iliyochukuliwa na Latra inatia matumaini kwa usalama wa abiria.

MWANANCHI
 
Rwanda na Kenya nishawai kusafiri usiku napishana na magari mengi akuna shida.

Kwa Rwanda jambazi anapigwa risasi chap ndio dawa kuu.
 
kuhakikisha wanafanya doria katika barabara zote zitakazotumiwa na mabasi yatakayokuwa yanafanya safari zake saa 24 katika kudhibiti

Jeshi la Polisi Waanzishe kikosi cha kukagua mwendokasi wa madereva, kuondoa magari yaliyoharibika barabarani, na mtu gari likiharibika atakiwe kisheria mbali ya kuweka triangle au majani barabarani basi mwenye chombo atakiwe kupiga simu kwa polisi patrol kuliondoa haraka barabarani au kikosi cha patrol wafike haraka kuliondoa na kumtoza gharama ya kulivuta / kukiondoa chombo kilichoharibika barabarani.

Hata kama polisi wakifanya patrol lakini hawawezi kuwa kila sehemu gari ilipoharibika kwa wakati. Gari inapoharibika, dakika tano tu ni muhimu sana.

Tujiulize nchi zilizoendelea kama za Marekani ya Kaskazini, Ulaya, Japan, Australia na China kwa kuzitaja kwa uchache wana vikosi vya doria vya usalama wa njia kuu / highway patrol iwe vipi nchi ya Tanzania ishindwe na kukosa kuona umuhimu wa kikosi cha doria cha usalama wa barabara kuu ?

Bonus Scene : Always On Patrol I Heavy Rescue : 401

Law enforcement on the 400 series highways is a massive task. The Ontario Provincial Police responds to calls big and small - all of them vital to making the highways safer.
Source : Discovery Canada
 
LAANA ya Mwalimu Nyerere inatutafuna.

Miaka 40 KUSHINDWA kuendekeza Reli.

Wenzetu Wana Underground Railway na treni za MWENDO Kasi.

CCM MBUMBUMBU MASIKINI WA FIKRA.
 
Jeshi la Polisi limetoa maagizo kwa makamanda wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanafanya doria katika barabara zote zitakazotumiwa na mabasi yatakayokuwa yanafanya safari zake saa 24 katika kudhibiti aina zozote za kihalifu.

MWANANCHI
Wakawaongezee magari na Waajiri askari wa kutosha ili kutimiza hilo lengo nje ya hapo itakuwa stori tu.
 
“Maeneo ambayo mara nyingi madereva huvunja sheria za usalama barabarani kama yenye miteremko inayosababisha ajali hasa usiku, yatakuwa kwenye uangalizi mkali na askari watakuwepo muda wote,”alisema Awadhi.
Sheria ni msumeno hukata uendapo mbele na urudipo nyuma, je madereva wakisababisha ajali vipi hao police wa patrol
 
Jeshi la Polisi Waanzishe kikosi cha kukagua mwendokasi wa madereva, kuondoa magari yaliyoharibika barabarani, na mtu gari likiharibika atakiwe kisheria mbali ya kuweka triangle au majani barabarani basi mwenye chombo atakiwe kupiga simu kwa polisi patrol kuliondoa haraka barabarani au kikosi cha patrol wafike haraka kuliondoa na kumtoza gharama ya kulivuta / kukiondoa chombo kilichoharibika barabarani.
Sambamba na hilo wafungue ukurasa wa mtandao ili iwasaidie kupokea taarifa kutoka kwa wadau wengine watakaoyaona magari hayo mabovu yaliyoziba njia
 
Sambamba na hilo wafungue ukurasa wa mtandao ili iwasaidie kupokea taarifa kutoka kwa wadau wengine watakaoyaona magari hayo mabovu yaliyoziba njia

Muhimu sana maana tumeona ajali nyingi kwa chombo kimoja kugonga gari bovu lililoacha barabarani kwa masaa kibao
 
Jeshi la Polisi Waanzishe kikosi cha kukagua mwendokasi wa madereva, kuondoa magari yaliyoharibika barabarani, na mtu gari likiharibika atakiwe kisheria mbali ya kuweka triangle au majani barabarani basi mwenye chombo atakiwe kupiga simu kwa polisi patrol kuliondoa haraka barabarani au kikosi cha patrol wafike haraka kuliondoa na kumtoza gharama ya kulivuta / kukiondoa chombo kilichoharibika barabarani.

10 April 2024
#BREAKING: AJALI MBAYA! BASI LA LUJIGA LAGONGA LORI KWA NYUMA – MASHUHUDA – “VIFO WATU 7 MAJERUHI WENGI

View: https://m.youtube.com/watch?v=-0lYhFwvv00

Madereva wa magari yaliyoharibika barabarani watungiwe sheria kuita polisi mara pale gari bovu linaposhindwa kutolewa barabarani mara moja ili kuepusha ajali za madereva wasiokuwa waangalifu.
 
Back
Top Bottom