Chama cha Wamiliki Mabasi (TABOA) kusitisha kutoa huduma kuanzia Jumatano wiki ijayo kwa kugomea mfumo wa ukataji tiketi kupitia mtandao

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,938
25,281
Chama cha wamiliki wa mabasi nchini(TABOA) kwa kauli moja kimetangaza kusitisha kutoa huduma kuanzia jumatano wiki ijayo kwa kugomea mfumo wa ukataji tiketi wa mtandao wakidai mfumo huo ni kandamizi na unawaumiza wamiliki na kufIkia hatua ya kutaka kuwafilisi.

====
Dar es Salaam. Wamiliki wa mabasi wameeleza kusudio lao la kusimamisha huduma ya kusafirisha abiria endapo suala la kutumia mashine za kukatia tike kwa njia ya mtandao (POS) halitapatiwa ufumbuzi.

Mashine za POS zinamtaka mmiliki wa fedha kuweka kiasi cha fedha katika laini ya simu au wakala wa huduma za fedha kwa makadirio ya abiria wa basi husika. Mfano kama basi linabeba abiria 50 kwa nauli ya Sh30,000, mmiliki analazimika kuweka Sh1.5 milioni katika laini ya mashine hiyo.

Hata hivyo, kwa nyakati tofauti baadhi wa wamiliki wamekuwa wakiulalamikia mfumo wakisema siyo rafiki kwa matumizi ya mabasi hayo wakidai una mapungufu makubwa yanayosababisha wao kupata hasara.

Kutokana na hali hiyo, leo Jumamosi Machi 8, 2021 Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), kimeitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kujadili mfumo huo ambapo asimilia kubwa wa wajumbe wa mkutano huo waliazimia kuegesha mabasi yao endapo suala hilo halitashughulikiwa.

Wengine wameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra), kuachana na mfumo huo badala watoe muongozo kwa wamiliki kutumia mashine za kieletroniki za EFD zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Ingawa hakuwasema muda wa utekelezaji wa mchakato huo wa kuegesha mabasi yao, lakini walitaka Latra kulishughulikia suala hilo, wakisema tangu kuanza kutumika wamekuwa wakipata hasara hali inayosababisha kutojiendesha kwa ufanisi.

“Hili suala ni janga inabidi tupate mashine nyingine kama wanazotumia wafanyabishara. Endapo mfumo huu utaendelea nitawalipa wafanyakazi wangu madai yao kisha mabasi yangu nitayaegesha maana sitoweza,” amesema Max Komba mwakilishi wa mabasi ya Tavavili.

Mwaka 2017 Taboa mkutano mkuu maalumu wa Taboa uliazimia kugoma kutofanyika kwa shughuli za usafirishaji , wakipinga sheria inayolenga kupitishwa ambayo walidai haikuwashirikisha wadau na haitenganishi makosa ya dereva na mmiliki, hali inayosababisha kosa lililofanywa na dereva kusababisha mmiliki kufungwa jela.
 
Jumatano ijayo TABOA wanaanza mgomo wakigomea mfumo wa tiketi za kielektroniki ambao wamesema unaelekea kuwafilisi. Wameamua kwa kauli moja kuanza rasmi mgomo.

Tumekuwa tukishuhudia huko nyuma serikali ya awamu ya tano ikitumia ubabe na vitisho kuzima sauti za madai na matokeo yake kupelekea msiba mkubwa sehemu husika. Kwa hili watakuwaje? Tusubiri tuone.
 
Kivipi unaumiza tafadhali nitaongea na Ngewe mkurugenzi mkuu wa Latra ni msikivu. Tafadhali fafanua kivipi haraka mleta mada changamoto ni zipi?
 
Please elezeni tatizo ni nini kiufasaha mpewe msaada. Tulieni andikeni mkiwa mumetulia. Haraka andikeni kwa ufumbuzi. Mleta mada simamia zoezi
 
Jumatano ijayo TABOA wanaanza mgomo wakigomea mfumo wa tiketi za kielektroniki ambao wamesema unaelekea kuwafilisi. Wameamua kwa kauli moja kuanza rasmi mgomo.

Tumekuwa tukishuhudia huko nyuma serikali ya awamu ya tano ikitumia ubabe na vitisho kuzima sauti za madai na matokeo yake kupelekea msiba mkubwa sehemu husika. Kwa hili watakuwaje? Tusubiri tuone.
tiketi za ndege hukatawa kwa mfumo wa ki ekectronic na kuna mabasi kibao nao huo mfumo toka zamani kabla ya sasa ikiwemo scandinavia mwanzilishi wa huo mfumo sasa hivi yako mabasi kibao unakata online tiketi na meli pia unakata online .Hawa Taboa siwaelewi mbona kuna mabasi unakata online tiketi na ni wanachama wa Taboa waneanza siku nyingi na hawajafilisika kwa ajili ya mfumo?
 
Kumbe Wewe uelewa wako mdogo,kwenye ndege TCAA ndo wameweka mfumo wa kukata ticketi?au kwenye meli SUMATRA ndo wameweka mfumo wakukata ticket?
 
tiketi za ndege hukatawa kwa mfumo wa ki ekectronic na kuna mabasi kibao nao huo mfumo toka zamani kabla ya sasa ikiwemo scandinavia mwanzilishi wa huo mfumo sasa hivi yako mabasi kibao unakata online tiketi na meli pia unakata online .Hawa Taboa siwaelewi mbona kuna mabasi unakata online tiketi na ni wanachama wa Taboa waneanza siku nyingi na hawajafilisika kwa ajili ya mfumo?
Hawa sio machizi lazima kuna cost ya uendeshaji imeongezeka..., Kama Serikali inataka database moja itumike na sio kila mtu na database yake, apart from TRA, utakuta hapo wanamlipa LATRA, na mdau atakayepewa Tender ya kusimamia hizo tickets...
 
CCM ina mhujumu Rais wamiliki wamabasi 100 % ni makada wa tifuu wa chama akiwemo mwigulu .co
 
Taboa wanatumiwa na chadema hawa
NI KWELI ,😃😃.

HATA "shida ya upumuaji" imeletwa na CHADEMA.

Ila ni siri yako usimwambie mtu. 🤣🤣🤣🤣

TATIZO LA "ajira" nalo limesababishwa na CHADEMA na hii pia ni "SIRI " kubwa sana...😃🤣🤣🤣 usimwambie mtu 🤣🤣🤣🤣

AMA kweli" UJINGA NI MZIGO MKUBWA"😃😃😃🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom