LATRA: Mabasi yasiyotumia tiketi mtandao mwisho Septemba 1

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra), imesema kuanzia Septemba 1, 2022, mabasi yanayofanya safari za mikoani na nchi za nje yasiyotumia tiketi za mtandao hayaturusiwa kufanya shughuli za usafirishaji wa abiria.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Agosti 18, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maendeleo ya mchakato wa matumizi ya tiketi mtandao kwa mabasi yanayoendea katika mikoa mbalimbali na nchi za jirani.

Amesema kipindi cha majaribio ya matumizi ya tiketi mtandao kilikuwa kuanzia Aprili Mosi mwaka huu hadi Juni, lakini Latra ikishirikiana na wadau wakiwamo Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) walikubaliana kuongeza muda.

"Mamlaka iliongeza muda wa miezi miwili hadi Agosti 31 unaombatana na utoaji wa elimu kuhusu suala hili. Changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika mchakato huu zimeshafanyiwa kazi," amesema Suluo.

Kwa mujibu wa Suluo, hadi Agosti 17, 2022 jumla ya mabasi 2,033 kati ya 3,916 yanayomilikiwa na kampuni za usafirishaji wa abiria yaliunganishwa na tiketi mtandao na kubaki 1, 883 sawa asilimia 52.

"Kwa hatua hii hatua mamlaka imepanga kuchukua hatua stahiki ikiwamo kutoa adhabu ya faini au kusitisha huduma ya mabasi yote yatakayoshindwa kutimiza takwa hili ifikapo Septemba Mosi," amesema Suluo.

Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara, Johansen Kahatano amesema suala la tiketi mtandao ni la kila mtu na lina faida kwa wananchi na Serikali. Amewataka abiria kuwa mstari wa kukata na kudai tiketi mtandao badala ya tiketi za karatasi.

Chanzo: Mwananchi
 
Sasa na sisi abiria tunao pandia njiani, hizo tiketi tutakutana nazo humo humo kwenye basi, au!!
 
Hawana lolote la kusema kuhusiana na nauli ambazo kimsingi bila:
1. Uwepo wa wapiga debe
2. Uwepo wa wenye kudai za kubrashia viatu
3. Uwepo tozo za stendi utitiri zisizokuwa moderated.
4. Nk
zingaliweza kuwa chini zaidi pamoja na changamoto zisizoepukika kama za vita vya Putin?
 
Hawana lolote la kusema kuhusiana na nauli ambazo kimsingi bila:

1. Uwepo wa wapiga debe
2. Uwepo wa wenye kudai za kubrashia viatu....
Hizo wapiga Debe nazani ni kampuni inajitakia mbona kuna kampuni hazina hao wapiga debe?
 
Hso wapiga Debe nazani ni kampuni inajitakia mbona kuna kampuni hazina hao wapiga debe?
Wapiga debe wakijiita pia maajenti hauwezi kuwa mradi wa wenye mabasi ambao madhara yao ni nauli kuwa juu zaidi.

Wapiga debe wanajulikana kuwa ni wafuasi na wapiga kura wa chama fulani kinacho jinadi hadharani nao kuwa ni wanyonge. Wapiga debe hawa wanakula na kuvimbiwa pamoja na wale wabrashi viatu.

Kama Dar Mwanza mpiga debe analamba si chini ya 5,000/- kwa kila abiria, unadhani mradi huu ni mdogo au wewe hukuwahi kuwasikia Mungiki?
 
Baada ya zoezi hilo tunataka wapigadebe wote watafutiwe shughuli mbadala, haiwezekani mtu anatoka Mbagala akifika Mbezi mjinga mmoja anakunadi kwa muuza tiketi bila wewe kujijua
 
Baada ya zoezi hilo tunataka wapigadebe wote watafutiwe shughuli mbadala, haiwezekani mtu anatoka Mbagala akifika Mbezi mjinga mmoja anakunadi kwa muuza tiketi bila wewe kujijua
Wapiga debe ni mradi wa wabrashi viatu. Kumbuka si chini ya 10% ya mauzo ya basi kwa wakati. Huu si mradi mdogo ndiyo maana bila wananchi kusimama imara mbona tutaendelea kuisoma namba?
 
Wapiga debe wakijiita pia maajenti hauwezi kuwa mradi wa wenye mabasi ambao madhara yao ni nauli kuwa juu zaidi...
Naomba ukubaliane na mimi kwamba mfumo uuh utaokoa ma billioni yalikuwa yanapotea kwenye unknown market ya wapiga debe ambao hata kodi hawalipi.
 
LATRA imepiga marufuku matumizi ya tiketi za kuandikwa kwa mkono kuanzia 01/09/2022

Mabasi yote ya mikoani ni lazima watoe tiketi Mtandao vinginevyo watapigwa faini ya tsh 250,000

Source ITV
 
Hilo zoezi litasitishwa...

Ukiniuliza kwanini, jibu ni kwamba hatujawahi kuwa serious...
 
Back
Top Bottom