CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic amekiandikia barua chama cha Chadema na kukipa saa mbili kuondoa bendera zake zilizowekwa barabara ya Sam Nujoma karibu na ukumbi wa Mlimani City unakofanyika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.

Screenshot_20191217-155149.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic amekiandikia barua chama cha Chadema na kukipa saa mbili kuondoa bendera zake zilizowekwa barabara ya Sam Nujoma karibu na ukumbi wa Mlimani City unakofanyika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.View attachment 1295069

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwahiyo zikikaa hapo mapato ya halmashauri yanapungua? Tutaona na kusikia mengi
 
Hilo ni eneo la kibiashara lisigeuzwe la kisiasa

Watu kutoka mataifa mbali mbali wanafika pale

Je itajenga picha gani kwa Nchi yetu?

Tuache siasa
 
Ifike mahala watanzania tuache kupinga pinga kila kitu.
Mkurugenzi yupo sahihi kabisa, hizo bendera za CHADEMA ndiyo zimesababisha hizi mvua na mafuriko haya Dar.
Ni mvua hizo zilizosababishwa na hizo Bendera zimesababisha Mkurugenzi aache kutembelea maeneo na wahanga na kuongelea uharibifu uliosababishwa, badala yake wamesababisha aende maeneo zilipowekwa hizo bendera na kurudi kukaa ofisini kuwaandikia barua za maelekezo CHADEMA kwa tabia zao.
 
Ni hofu tu kuwa ataulizwa kwa nini. Pengine katahadharishwa. But hii ni ajabu sana tena saa mvili na mvua juu.
Mkurugenzi ukiona hizo bedera mapepo yanakupanda nini? Mbona za kawaida tu! Je ingepandishwa ile ya Yesu mwenyewe kiboko ya wachawi na mapepo,majini nk ungekuwa kwenye hali gani? Punguza jazba hazisaidi Nchi

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom