Uchaguzi 2020 CHADEMA: Tunamuunga mkono Maalim Seif kwa Urais Zanzibar. Lissu hataendelea na kampeni, atapangiwa majukumu mengine

Usihusianishe mambo ya dini na siasa, tabia ya kubaguana kidini ni tabia mbovu kabisa, siungani na wewe katika hiyo dhambi.
Lisu kapata alichostahili kukipata kufanya kampeni hadi saa1 usiku unadhani ni sahihi kwa mujibu wa sheria?
Asalaam alaykum
Hapa sijahusisha dini na siasa, nilikuwa naku challenge katika morals na principles zako hususan ukiwa Mwislam(basing on your name).
Simamia HAKI...hilo la saa moja lifuatilie vizuri ikiwepo sababu ya kucheleweshwa kwa msafara kulikosababishwa na mamlaka za dola.
 
Tuliwaambia Chadema usaliti ni laana, poleni kwa usaliti laana inawakabili
A[iyekuwa mwimbaji kwenye tungo yuko hoi, hata akiwa Njombe anahitaji kiyoyozi. Umebaki nayo pekeyako. Hata superliar Polepole kaiacha, hoinogi.
 
Chadema naona akili zinaanza kuwakaa sawa sasa !
hapo sasa tuko pamoja...

baba kasema hakuna namna
 
Mbowe ameongea kwa busara inaonekana amekomaa badala ya kuhamasisha fujo ameagiza mawakili wa chama wafungue kesi kwa hati ya dharula hizi ndio siasa tunazotaka hata kama demokrasia inaminywa tutajua nani ni tatizo sio kudanganya watu kuingia barabarani na kuganya fujo wakati umekimbizq familia yako nje
 
Kwa mujibu wa Tumaini Makene:

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman A. Mbowe leo Jumapili, Septemba 4, 2020, saa 7 mchana atatoa tamko, kupitia Mkutano wa Waandishi wa Habari, kuhusu maazimio ya Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Chama kilichoketi jana na kumalizika usiku jijini Dar es Salaam.

Asanteni.
========

7:45 mchana: Mambo yanawekwa sawa tayari kwa mkutano wa waandishi wa habari

7:53 mchana: Viongozi wakuu wa CHADEMA wamefika na mkutano kuanza


Mbowe: Ninapenda kuwaeleza watanzania kupitia ninyi waandishi wa habari mambo kadha wa kadha yaliyojiri katika kikao chetu cha kamati kuu ya chama kilifanyika katika ukumbi wa Bahari beach hotel siku ya jana kuanzia asubuhi hadi usiku wa manane.

Kikao kilikuwa na agenda mahsusi moja ambayo ni kujadili mwenendo wa uchaguzi mkuu Urais, wabunge, Rais wa Zanzibar, wawakilishi pamoja na madiwani wote kwa upande wa Tanzania Bara na visiwani.

Kamati kuu imeridhika na mwenendo wa misafara ya kampeni ya mgombea wetu wa Urais na mgombea mwenza ukiondoa matukio machache ya kidhalimu yaliyofanyika katika maeneo ya Nyamongo kwa upande wa mgombea wetu wa Rais na tukio la msafara wa mgombea mwenza kupigwa mabomu katika mji wa Ifakara.

Pili kamati kuu imeitafsiri sana na kuitathmini tume ya Taifa ya uchaguzi na baadhi ya maamuzi yake na mwenendo wake. Kamati kuu imesikitishwa na kitendo cha tume ya Taifa ya uchaguzi kuengua wagombea 36 wa ubunge, 35 wakitoka Tanzania Bara na mmoja kutoka visiwani na kuengua wagombea udiwani wetu 577.

Tunatambua kwamba uchaguzi wote husimamiwa na sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa, vilevile tunatambua sababu mbalimbali zilizotolewa na tame hazina mashiko ya kisheria, hazina mashiko ya kimantiki, zinavunja mfumo wote wa kidemokrasia katika nchi.

Kwamba wagombea wote wa CCM hakuna hata mmoja aliweza kuenguliwa hata wale ambao sisi tulikata rufaa dhidi yao kwa makosa ya msingi na wazi.

Kamati kuu imejiridhisha tume hii ya uchaguzi ni chombo na kinacholindwa makusudi kulinda chama cha Mapinduzi na serikali yake.

Tume imetoa adhabu mbalimbali zisizo za msingi, zisizo za kidemokrasia bila kutia maanani kipindi cha uchaguzi ni kipindi kifupi sana.

Kipindi cha kampeni, kwa mfano mgombea wa CHADEMA wa kiti cha ubunge cha Ubungo, baada ya mchakato kuanza alikatiwa rufaa kwa hiyo hakuruhusiwa kufanya kampeni kwa wiki mbili na nusu kwa sababu ilikuwa haijatoa rufaa yake, baada ya wiki moja, chama cha mapinduzi kikakata rufaa na tume tena ikamsimamisha kwa wiki nyingine moja, unamchelewasha kwa wiki tatu.

Mgombea wetu wa ubunge Same Magharibi alifungiwa kwa wiki mbili, hatujasikia mgombea wa chama cha mapinduzi akisimamishwa pamoja na uharamia mwingi.

Tume imeendelea kuchelewesha majibu katika majimbo kadhaa, jimbo la Iramba Magharibi lenye mgombea Jesca Kishoa, dada makini kabisa, madiwani wake wote wameenguliwa katika uchaguzi kwa sababu ambazo hazina msingi kabisa.

Tume hii inachochea misingi ya kuleta machafuko katika Taifa kwa sababu siku zote tunasema, uvumilivu una mwisho. Kwa hiyo kuna wagombea wetu hawajapata majibu wakati asilimia 50 ya muda wa kampeni umeshapita.

Tumepeleka malalamiko kadhaa ya makosa ya msingi yanayofanywa na wagombea wa chama cha mapinduzi kwa tume tukilalamikia masuala ambayo yanakatazwa kisheria.

Kwa mfano, katika kampeni watumishi wa serikali ikiwemo Rais, waziri mkuu, mawaziri au watendaji wowote hawaruhusiwi kutumia ushawishi wa miradi au kutoa maelekezo ya ujenzi wa miradi mbalimbali katika kampeni.

Tunaona Rais anaagiza bila woga, waziri mkuu anaagiza bila woga. Tumelalamika tume ya Taifa ya uchaguzi lakini Tume haichukui hatua yeyote.

Tumemuona Rais mali za serikali, magari ya serikali yaliyobadilishwa rangi na kuwa rangi ya kijani na kuwekwa namba za chama cha mapinduzi, yale yote ni magari ya Ikulu. CCM hawajaagiza gari hata moja, yale ni magari ya Ikulu na kama CCM wanapinga watoke hadharani na document hizi hapa.

Tumeona msafara wa Rais una magari zaidi ya 80, magari zaidi ya 50 ni ya serikali au watendaji wa serikali. Hii ni unfairness kwa sababu unampa Rais msuli wa serikali inayoendeshwa kwa kodi za wananchi wote.

Walimu wanalazimishwa kwenda kwenye mikutano ya chama cha mapinduzi, hatuna tatizo CCM wakiwaalika wasanii, ile ni initiative yao lakini waalimu wa nchi yetu ni watumishi wa Umma, wanafunzi ni watoto wa watanzania mbalimbali wakiwemo wa chama cha mapinduzi, vyama vya upinzani.

Tumeona vyombo vya habari vya umma kama TBC vinamtangaza Magufuli asubuhi mpaka asubuhi, magazeti ya umma. Mamlaka nnyingi za kiserikali, TCRA ikifanya kazi kubwa ya kujaribu kudhibiti matumizi ya mitandao na kunyima uhuru wa watu kupokea habari.

USHIRIKIANO WA VYAMA
Tumesikia viongozi kadhaa wakizungumza dhana ya ushirikiano wa vyama na tumemsikia msajili wa vyama vya siasa akitokeza hadharani akisema nyinyi hamruhusiwi kuunga mkono chama kingine, muda umeshapita, haya ni mambo ya kusikitisha sana.

Hauwezi ukanitungia mimi sheria ya kujenga mahusiano na rafiki ama kujenga uadui na mtu, hayo ni mahusiano ya watu na watu.

Wamekuwa wakipinga kauli zozote zinazoashiria ushirikiano wa njia yoyote kati ya CHADEMA na ACT lakini wakati huo huo akifumbia macho viongozi wa hivi vyama pandikizi vya upinzani kama TLP au UDP vikitoka na kumuunga mkono Magufuli.

Msajili anatamani kuona nchi hii inatawanyika vipande 40, sisi tunatamani kuona watanzania wanajumuika pamoja kutengeneza force za kisiasa aidha za upinzani au za chama tawala zenye nguvu ya kupingana kwa hoja.

Kamati kuu baada ya kushauriana kwa kina na mgombea wetu Urais wa Zanzibar, tumeona ni sahihi kabisa kwa chama chetu kumuunga mkono Seif Sharif Hamad, mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha ACT kwa hio mgombea wetu ameridhia kujitoa yeye mwenyewe kwa mapenzi yake, taratibu zake za kujitoa zitafata.

Kamati kuu imeridhia kuendelea na mazungumzo kuungana mkono kwa baadhi ya kata hata majimbo ambayo tunafikiri tukiweza kumuunga mkono wa chama kingine mwenye nafasi zaidi tunaweza tukapata muwakilishi alie bora zaidi wa eneo hilo.

KUZUIWA MIKUTANO KWA MGOMBEA URAIS
Tume ya taifa ya uchaguzi kumzuia mgombea wetu, nimeshazungumza kuhusu tume kuwa mchezaji na refarii. Awali mheshimiwa Lissu alisema ataendelea na mikutano yake ya kampeni ambayo kimsingi ni haki yake lakini akasema uamuzi wa mwisho anaiachia kamati kuu ya chama chetu. Tumekubaliana tufanye yafuatayo

Kwa sababu tunatambua nia na dhamira mbaya ya tume ya uchaguzi, kwa sababu tunatambua sababu mbalimbali zisizo na maniki sana zinazotafutwa kujaribu kumkwara zaidi mgombea Urais, tumeamua kutowapa fursa hawa tume ya Taifa ya uchaguzi.

Hata kabla sijaeleza maamuzi yetu, naomba nieleze ni nini kilifanyika, tumepokea hukumu kutoka tume ya Taifa ya uchaguzi, katika kujitetea kwake, tume ya Taifa ya uchaguzi pamoja na mambo mengine kadhaa ijaribu kujenga dhana kwamba adhabu iliyotolewa haikutolewa na tume, imetolewa na vyama vingine vilivyoshiriki uchaguzi huu.

Fair enough lakini mwenyekiti wa kikao na katibu wake ni watendaji wakuu wa tume kwa maana hiyo wanarusha lawama kwamba hawakuamua wao, waliopiga kura ni vyama vyenyewe vya siasa.

Tuna vyama 15 vilivyoshiriki kikao hicho(Anavitaja) na katika kura 15 zilizopigwa, kura tatu zilikataa kumfungia mheshimiwa Lissu mikutano yake lakini kura 12 ya hivi vyama vilivyopiga kura eti ya kumuengua mheshimiwa Lissu asiendelee na kampeni.

Huu tunajua ni uamuzi wa chama cha Mapinduzi kwa kuvitumia hivi vyama, sisi kama CHADEMA tunapinga hukumu hii.

Tumemshauri mgombea wetu asiendelee na mikutano kwa hiyo mheshimiwa Lissu hataendelea na mikutano ya kampeni kwa kipindi hiki ambacho tume imezuia mikutano yake.

Tundu Lissu sio tu ni mgombea Urais wa chama chetu, huyu ni makamu mwenyekiti wa chama na chama hiki kina kazi kubwa za kufanya, za kisiasa na za kijamii kwa hiyo Tundu Lissu hatakosa kazi ya kufanyakwa kipindi cha siku saba.

Chama kitampangia program mahsusi kama makamu mwenyekiti wa chama kufanya majukumu ya kijamii na kisiasa katika maeneo ambayo chama kitapanga.
Chadema ilikataliwa kutumia helikopita lakini imekuwa nafuu ya helikopita sasa wamezuia asifanye mikutano bado itakuwa nafuu ya kumwacha afanye mikutano.
Kila mbinu chafu kwa Lissu ni kete ya kusonga mbele.


Ni yeye Lissu 2020- 2025.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini tundu anamuheshimu Lowasa na kuthamini mchango wake ndani ya chadema na hawezi kumtusi na kumdharau hata siku moja, ...
Tundu Lissu yuleyule uliedai hatainuka, hatarudi ndie unaejaribu kumlisha 'utunzi' wako.
 
Kwa yeyote mwenye akili ameelewa mantiki ya kikao hiki Ila Kuna wapuuzi waliozama kwenye ujinga wanaelewa nini Cha kufanya
 
...tunajua mpo mnachochea kuni ili likiharibika au akienguliwa mrudi na gia ya kulaumu kuwa tulishindwa kujizuia kumzuia lissu asifanye kampeni ...mitego mingine inahitaji umakini ..usiwadharau viongozi wetu kwa matakwa yako ya kipumbavu ..
Wabunge 50 na madiwani wasio na idadi wameenguliwa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Anpigwa ban mgombea urais chama kinatii.

Sasa ccm itaondoa mawakala zaidi ya nusu na hmtafanya chochote. Na wabunge kibao hawatatangazwa na hakutakiwa na chochote.

Huyo Lisu ndo kabisaa. Yeye ndiye atapata less than 10% halafu mtatoka vichwa chini.

Mbowe ana-target ruzuku tu.
 
Kwa muktadha huu CDM wataendelea na kampeni kwa sura ya makamu mwenyekiti anafanya kazi za chama
Ndicho nilichokiona
Hawa CDM wana akili fulani hv
 
Maamuzi ya akili nyingi sana haya.. "majukumu mengine ya kijamii na kisiasa" mf. Kuhuisha chadema ni msingi jimbo la kibamba... Kwa kutumia mifano kuntu tofautisha kuhuisha chadema ni msingi na kampeni!
 
Hapana hiki ni chama makini sana na kinajua kwa hakika kifanye nini kwenye nini na wakati gani...

Naungana nawe Mkuu Mshana Jr kuwa hicho ni chama makini. Bila woga au kumung'unya maneno, leo M/Kiti hadharani:
√ kafutilia mbali uwezekano mdogo uliikuwepo wa kushirikiana na ACT Wazalendo kwa kumtosa rasmi mgombea wao wa Urais wa JMT na hapo hapo kujiondoa kwenye uchaguzi wa Serikali ya Mapinduzii Zanzibar, bila kujali athari za kufanya hivyo kwa wagombea wengine wa CHADEMA na wa ACT wazalendo;
√ kuita vyama vya siasa vingine vinavyoshiriki ni vyama mamluki vya CCM;
√ pamoja na mgombea wao kuzuiwa kufanya kampeni kwa siku 7, nyuma ya pazia, kubariki aendelee na kampeni;
√ kuagiza wanachama kuingia barabarani wasipotangazwa washindi.

Pamoja na umakini huo niwakumbushe yafuatayo:
√ Mbowe huyo huyo alitangaza kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kushinikiza urudiwe la hawatashiriki Uchaguzi Mkuu;
√ Mbowe aliagiza wabunge wake kususia Bunge la Bajeti kwa sababu ya korona akishinikiza bunge lisiendelee.

Yajayo yanafurahisha na kila la kheri tukisubiri mrejesho wa maumuzi hayo 29/10/2020
 
Hapana hiki ni chama makini sana na kinajua kwa hakika kifanye nini kwenye nini na wakati gani...
Lissu angekaidi maamuzi ya tume ya maadili iliyopo kwa mujibu wa sheria, angekuwa amefanya kosa la kihaini. Angefunguliwa kesi ya uhaini ambayo haina dhamana. Kwahiyo, nakubaliana na wewe kuwa Mbowe amekuwa makini kulinda ruzuku, maana Lissu angeswekwa remanded Chadema ingekosa ruzuku.
 
Lisu amemtega Mbowe. Ni ama aheshikike ama adhauraulike. Maamuzi ya mgombea tunayajua, maamuzi ya kamati yakiwa kinyume na yale ya mgombea Mbowe utapwaya sana
Mbowe ndio gateway ya mafanikio ndani ya Chadema. Hakuna mtu anayeweza kufanya lolote ndani ya Chadema bila indini ya Mbowe. Kwahiyo Lissu lolote analoongea utekelezaji wake unategemea na kuridhia kwa Mbowe. Katika mambo makubwa usimuamini Lissu kabisa, hana mamlaka ya kuamua lolote.
 
Majukumu ya kichama!kama kuwaona wagonjwa,kuwatembelea wafanya biashara wadogo wadogo,warsha na matamasha !!!hiyo ni kampeni tosha kabisa!!!Wamekwepa risasi za CCM!!!walitaka wapate sababu ya kutumia mabomu ya machozi!!
 
Back
Top Bottom