CHADEMA na Udikteta Makao Makuu

Mzee Kifimbo, uwe na ujasiri basi, kwanini unataka mimi nijibu swali lako?

Nimekujibu kule Chadema na Asha, unasema nakutaja nina posts kama 210 naomba ushahidi kuwa kila post nakutaja ktk hizo ngapi nimekutaja? kwani wewe ni nani hapa JF? au kuna classes?
 
Kifimbo

I read you loud and clear but I can guarantee you that; your actions won’t last long just be yourself and issues not JF members personally.

Mimi ndiye niliyeanzisha thread hii naomba kujua kwanini umelitoa jina langu? au kuna matusi kwenye yale maandiko yangu.
 
Kubwajinga

Nijibu pia jamani, nimeuliza swali kama uliwahi kufukuzwa CUF kutokana na tabia yako ya kuwabagua watu kutokana na dini na makabila yao.

Asha


Huu uzushi wa mimi na CUF umeutoa wapi wakati hunijui na wala mimi sikujui? Have you seen anything from my posting that is promoting or demoting CUF? Kama huna ushahidi wowote ingekuwa ustaarabu mzuri kama ungeomba msamaha ASAP.
 
Mimi ndiye niliyeanzisha thread hii naomba kujua kwanini umelitoa jina langu? au kuna matusi kwenye yale maandiko yangu.

jibu swali langu kwanza; kwanini ulinitaja nijibu na kuniweka kati ya Mnyika na Kitila? Kwanini kwa mfano hukutaka KubwaJinga, Mzee ES au Chinga kujibu?
 
Kitila na Mnyika ni watu wako wa karibu sana.

Once again, onesha ushahidi kuwa Kitila na Mnyika ni watu wangu wa karibu sana? Kwanini usiseme Mzee ES au Reverend Kishoka, au Invisible, au mtu mwingine yoyote ambaye yuko karibu na mimi? H

Onesha ukaribu wangu na Mnyika na Kitila na ueleze huo ukaribu (kama upo) umetokana na nini? go ahead..una ruhusa yangu.
 
Rudia tena swali lako liweke vizuri sijakuelewa.

of course, (ni mgumu kuelewa na mwepesi kusahau ulichokisema punde) nitakusaidia. Umesema Mnyika na Kitila ni watu wangu wa karibu sana. Onesha ushahidi kuwa ni watu wa karibu na ukaribu huo umetokana na nini (kama upo huo ukaribu)
 
nakumbuka december 2006 Bwana Mbowe alipeleka misaada kanisani-Kilimanjaro tu. lakini hajawahi kusaidia watu wa dini nyingine leo umetusaidia kuwa ni chama cha wakristu wachagga, ndio maana ANNA KOMU ilibidi awe mkristu ndio apewe ubunge.

Mwaka 2006 Vyombo mbalimbali vya habari viliandika michango ambayo Mbowe ameitoa misikitini na kwa waislamu ikiwemo milioni nne alizochangia chuo cha waislamu na kupewa cheti cha heshima na Mufti.

Ana Komu amechaguliwa kuwa Mgombea Mwenza akiwa Muislamu na baadaye akatueliwa kuwa mbunge wa Viti Maalum. Kama angekuwa si Mzanzibar pingamizi lililoweka na DP na Mtikila lingepita na Mbowe angeondolewa kwenye kugombea urais.

Asha
 
Asha
Umesema kuwa wewe ni Mzanzibar lakini unaonesha kukerwa na CUF na udini wao. swali ni kama wewe ni mtu wahuko na majority ni Cuf,usingeweza kuusema Udini kwa ile wewe ni dini moja na hao Cuf wa Zanzibar.
ni sawa na Mbowe alalamikie uchaga ndani ya TLP, jambo lisilowezekana. kwa hili unataka kutuambia kuwa unadai uZnz ili kutuhadaa nakubaliana na Chinga kuwa wewe ni Kitila mkuombo.

Hivi we jamani unadhani waZanzibar wote ni CUF na CCM? Hebu soma huu mjadala hapa japo utapata akili http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=12645

Na nani kakwambia kama mimi nakerwa na CUF na 'udini' wao? Hilo la udini umesewa wewe, mi najua CUF si chama cha kidini

Asha
 
Matatizo yakitumiwa kama Stepping Stone siku zote hujenga badala ya kubomoa. Habari kwa jinsi ilivyoandikwa ina ukweli mwingi usio weza kupingwa.
Watu wenye mionyo ya ubinafsi na roho za kihayawani wapo kila mahali, watakosekana vipi Chadema?

Binafsi sioni tatizo la kutumia helkopta kusafiria lakini naona umuhimu wa ku priotize matumizi ya helkopta kulingana na safari.
Isiwe tu kwamba kila mara Mwenyekiti akitaka kwenda mikoani basi ni lazima apande hiyo machine.

Kuhusu kutumia ruzuku yote makao makuu na kuacha mikoa na wilaya na sehemu zote za nchi zikitapatapa, hilo nadhani ni kosa la kimiani mnyonya damu.
Chama siyo makao makuu, chama ni mtandao mzima wa utendaji nchini kote.
Kwa sabau Ruzuku inatolewa kufuata idadi ya wabunge ni vema kutoa fungu kubwa katika majimbo yaliyotoa wabunge na fungu jingine libaki HO na jingine liwekwe kuimarisha chama sehemu ambazo hazina wabunge.

Ukweli kwamba HO inatumia fedha karibu yote ya Ruzuku na wakati huo huo imeshindwa kabisa kutwaa hata kiti kimoja cha Ubunge katika majimbo ambayo yanaizunguka HO na lile ambalo ni la HO ni dalili moja kwamba kuna kundi la watu ambao Vision zao zinaishia kwenye mifuko yao ya kaptula na Account zao za Benki.

Njaa ni jambo la kujirudia rudia kwa kila kiumbe.
Ni vema kujenga mazingira ya kula leo kesho na siku zote kwa kila kiumbe kuliko kujenga mazingira ya kula leo na kuacha kesho ijishughulikie.

Uchunguzi uliomo ndani ya Taarifa hii nauunga mkono kwa dhati na bila kusita nawapa changamoto Chadema kuweka sawa mambo kuliko kuanza kuleta Mizengwe ya kukataa madai ambayo yana kila dalili ya ukweli.


here we go again Kifimbo . .Je mwenyekiti ndiye aliyekuwa na maamuzi pekee ya kuwateua hawa ama ni Chama ? Yaani akina Slaa wote walidiwa nguvu na Mbowe ? Kama kuna maeneo ambayo hayapokei upinzani na hayana watu wa kuweza kuchukua nafasi bado wakachukulie mtaani ?Watu wote hawa wana historia na Chama .Hebu muone Mdee na Zitto kwa mfano .
Lunyu,

Umegusa kabisa kiini cha malalamiko, kuwa kuna wahusika ambao wana nguvu sana kwenye Chadema kiasi cha kuwapatia vibarua wapenzi wao, watoto wao, shemeji zao n.k.

Msisimko ulioletwa na vijana kama Zitto na Mdee ni mkubwa na unahitaji kudumishwa kwani umewavuta watu wengi kuingia au kushabikia Chadema, hasa vijana. Hii ndio maana ni muhimu sana kwa CHADEMA kujiangalia upya na kuondoa haya makunyanzi ambayo yanaweza yakakigawa chama.


It is worth recalling what was said two months ago.
 
Wakubwa na wadogo... Amani iwe kwenu!!!!!!!!!

Haya tena CHADEMA ni chama cha udikteta na mafisadi walioko pale makao makuu kama alivyosema mzee Yusuf Halimoja.

Ninaweza kabisa kuzungumzia sababu za hoja hii kuvuma na kusambazwa kwa bidii kubwa. Lakini nitafanya hivyo nitakapojiridhisha kuwa wasomaji wangu hapa hawalijui jukumu la CHADEMA bungeni wala katika majukwaa ya siasa Tanzania. Kwa ajili ya ukweli huo mimi nitazungumzia tu ulazima wa akina RA, EL, JK na wengine wengi ambao wana uhakika wa kuendelea kutawala kwa kupitia CCM, kuajiri watu na kulipa fedha nyingi kwa mission ya kupandikiza migogoro ndani ya CHADEMA.

Historia ya Tanzania inaonyesha kuwa toka miaka ya 1980 tumekuwa tukiibiwa. Na kila miaka ilivyosonga licha ya nchi kuwa na wasomi wengi, vyombo vingi ya habari, wanasiasa wengi wajuzi; ndivyo pia na kasi na ukubwa wa kuibiwa kwa rasilimali za Tanzania ilivyoongezeka.

Hadi ilipofikia CHADEMA kwa msaada wa watanzania waliochoka kuvumilia wizi unaofanyiwa nchi yao na kutishika kuwa muda si mrefu nchi itabakia sega tupu, walitokeza hadharani na kuanza kuwavaa wazi wazi wezi wa rasilimali zetu. Iliwakilishwa Buzwagi, Ikafuata orodha ya Mafisadi, hatimaye ikawezekanishwa kashfa ya Richmonduli. Wakubwa wakajiuzulishwa, na mengine mengi yameendelea kujiri na yatakuja zaidi.
Ulitaka CHADEMA ifanye uchokozi gani zaidi ya huu. Mijitu ilizoea kula kwa kwenda mbele. Chini yao kuna watu wanasubiri wapukutishiwe makombo. Hawa ndo wanapiga kelele Oooh!!! CHADEMA ina ukabila, Eti CHADEMA inatumia vibaya fedha za ruzuku!!!!!! Na makelele mengine mengi tu!!

Hasira yao si ukabila ndani ya CHADEMA, wala si matumizi mabaya ya ruzuku.
Wanachokasirika ni jjinsi ambavyo wanavuliwa nguo na CHADEMA. wameamua kuajiri watu wa kukisambaratisha chama.

CHADEMA inapata shilingi ngapi jamani hadi tunaijadili namna hii??? Wao CHADEMA wanapewa 60,000,000/= tu kwa mwezi. Wenzao CCM wanapewa 2,000,000,000/= (shilingi bilioni mbili kwa mwezi) maana yake ni kuwa kila siku CCM inachukua 80,000,000/= kutoka katika hazina ya taifa. Kwa nini wanaochukizwa na matumizi mabaya ya ruzuku wasifuatilie hili??

Nilikuwa ninawasubiri watanzania wenye nia njema watokeze hadharani kuipongeza CHADEMA kwa kuweza kupambana na lichama kama CCM ambacho kinapata fedha nyingi kwa siku moja kuliko ambazo CHADEMA inapata kwa mwezi mzima. CHADEMA inaweza kuishikisha adabu CCM ambayo ina mabilionea wengi ambao wamevipata vijisenti vyao hivyo kwa kutumia mwavuli wa chama. CHADEMA inaibana na kuitisha CCM ambayo viongozi wake wengi wanatumia fedha za umma kukiimarisha chama. Sungura anapambana na tembo jukwaani na tembo ameridhika wazi kuwa kazidiwa. Sasa analazimika kutumia mbinu za ziada. Hiloo!!! kubwa zima hovyo*

Napeleka salamu kwa Mafisadi wanaojibidiisha sana kupandikiza migogoro CHADEMA, kwamba saa yenu ya kujitetea ni sasa. Lakini punde chaja kizazi ambacho hakitawapa ngau muda finyu wa kujitetea. Kizazi hiki hakitawapa nafasi mkidanganye na bakshishi. Hatakuwepo wa kununuliwa aanzishe migogoro CHADEMA. Na pengine aina ya siasa wakati huo haitakuwa ya vyama kama tuliyo nayo sasa.

Kama ninyi ni wevi mtaimbwa kila pahala kwa ushujaa wenu wa kuiba. Kama ninyi ni mafisadi na wala rushwa mtaimbwa hivyo hivyo kwa heshima ya uchafu wenu mlioifanyia nchi. Kutengeneza migogoro CHADEMA haitawajenga kwa muda mrefu.

Ninyi mliowekwa kuichachafya CHADEMA: tambueni mahitaji ya nchi yetu ya Tanzania. Tunahitaji wanamapinduzi wa kweli wanaoweza kupambana na ufisadi wa CCM. Tukiunyamazia tunawaacha watu wetu wengi hapa Tanzania wakiangamizwa na uharamia wa CCM. Pamoja na wajibu mliopewa na lamba lamba ambayo mmeahidiwa; hebu waacheni waliojitoa sadaka kutetea mustakabali wa masikini wazawa wa Tanzania waendelee kufanya hivyo. Oneni aibu kwa ajira mliyopewa.

Wanachama makini wa CHADEMA...... vita mbele, endeleeni kwa moto zaidi. Mamluki wanapopandikizwa kwenye chama washughulikiwe mapema kabla hawajajikita zaidi.
Karuzuku kadogo tunakopata tukatumie kwa makini kuwamaliza kabisa mafisadi.

Aluta kontinua
 
Jamani kuna mtu mwenye ile makala ya Mzee Mtei aliyoandika "CHADEMA ni nini, CHADEMA ni nani?" ambapo aliweka wazi historia ya kuanzishwa kwa CHADEMA na wakina nani alianzisha nao na katika maeneo gani? Iliwahi kuwekwa hapa JF na kati ya Zitto au Mnyika; hebu toeni link basi

Asha

...chama mbadala!!
 
Msubiri Philemon Michael aje...he gets so emotional niinvoke hii issue ya WAPUKI labda nitakutumia in PM
 
Back
Top Bottom