Freeman Mbowe: Tunaanzisha wiki ya Maandamano kwenye Makao Makuu yote ya Mikoa nchi nzima

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
127
420
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema chama hicho kitaingia kwenye awamu nyingine ya Maandamano yatakayofanyika kwenye makao makuu yote ya mikoa nchini, maarufu kama wiki ya Maandamano yatakayofanyika kuanzia Aprili 22-30, 2024.

Aidha, amewatangazia Diaspora kufanya maandamano makubwa kwenye miji mikubwa Duniani kupeleka Ujumbe duniani juu ya mambo yanayoendelea nchini.

Kamati kuu ya Chama hicho imepanga wiki hiyo ili kuwapa nafasi waumini wa dini zote kumaliza mfungo wao.
 
Hayo wafanyayo siyo maandamano ni matembezi tu maana hakuna watakachokipata kwa mdebwedo huo
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema chama hicho kitaingia kwenye awamu nyingine ya Maandamano yatakayofanyika kwenye makao makuu yote ya mikoa nchini, maarufu kama wiki ya Maandamano yatakayofanyika kuanzia Aprili 22-30, 2024...
Hilo ndio Azimio la Mtwara?😄
 
Niko interested kujua ni nini madai namba moja ya hayo maanadamano!
1. Uongozi thabiti kutokana na Katiba Bora( Mpya)
2. Uchaguzu huru utakaoleta viongozi waadilifu
3. Udhibiti wa Mali za Umma na mafisadi
4. Maboresho ktk mfumo Haki jinai
5. Hatua za Dharura kupunguza makali ya Gharama za maisha ikiwemo Mafuta, umeme. Petrol, chakula, usafiri
 
HAYO WAFANYAYO SIYO MAANDAMANO NI MATEMBEZI TU MAANA HAKUNA WATAKACHOKIPATA KWA MDEBWEDO HUO
Viongozi wanalipana posho za safari kutoka kwenye ruzuku ya chama kwenda kuongoza maandamano mikoani ni mradi wa kujikusanyia pesa za kugombea 2025 wao binafsi Ubunge kwa kisingizio cha maandamano.

Huo ni mradi wa viongozi
 
'Mbowe kaamua aje na mbinu za Raila, akilambishwa sukari kidogo anaweka mpira kwapani. Maandamano halisi ya kulikomboa taifa hili hayataanzishwa na wanasiasa, yataanzishwa na wananchi wenyewe siku upuuzi ukiwatoka kichwani
 
Back
Top Bottom