Mzee Kifimbo
Senior Member
- Mar 25, 2007
- 153
- 3
Naomba makada wa Chadema tupeni mwanga juu ya habari ya mzee Halimoja ambaye ni kada wa Chadema.
=======
Na Mzee Yusuf Halimoja - Gazeti la Mtanzania
KAMA tujuavyo, baada ya Tanzania kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Watanzania walikuwa huru kuanzisha vyama vya siasa. Kati ya vyama vilivyoanzishwa ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alipata nafasi ya kuangalia sera za vyama mbalimbali. Hakuficha alichoona. Alisema afadhali CHADEMA ilikuwa na sera nzuri.
Baada ya kauli ile ya Baba wa Taifa, ambaye amefariki dunia akiwa bado anaendelea kuheshimiwa na umma wa Tanzania, wananchi walitarajia kuona CHADEMA ikitumia kauli ya Mwalimu kueneza mtandao wake nchi nzima. Lakini haikuwa hivyo. CHADEMA imeshindwa kutimiza matarajio ya wananchi. Kwa nini?
Hebu turudi nyuma. Tumesikia watu wakisema kuwa chama tawala, CCM, kina makundi yake. Wenyewe wameendelea kupinga vikali kauli hiyo. Wanadai kuwa hakuna makundi ndani ya CCM. Tuanzie hapo.
Sipati sababu ya CCM kukataa kuwa na makundi. Makundi ni jambo la kawaida katika sekta mbalimbali za maisha, ikiwa ni pamoja na ndani ya vyama vya siasa. Hayana ubaya. Ubaya unakuja wakati makundi hayo yanapotumiwa vibaya.
Kwa mfano, katika dini ya Kikristo kuna makundi yanayoitwa "madhehebu". Kwa mfano kuna Wakristo Wakatoliki, Waanglikana, Walutheri, Wapentekoste, na wengineo wengi tu. Makundi haya yakishirikiana katika shughuli mbalimbali hujenga. Lakini yakipoteza wakati kupambana yenyewe kwa yenyewe huharibu.
Kwa upande wa vyama vya siasa, tuna mfano hai kutoka Marekani. Ndani ya chama kimoja cha Democrat wagombea wawili, Barack Obama na Hillary Clinton, wanapambana wakiungwa mkono na makundi ndani ya chama hicho hicho kimoja.
Kwa jumla chama bila makundi si chama hai. Ni chama kilichokufa. Makundi ndani ya chama huleta ushindani unaokisaidia chama kuwa hai, kupata mawazo mapya yanayokipeleka chama mbele, na hata makundi hukisaidia chama kupata viongozi bora wanaotokana na ushindani.
Tukiiangalia CHADEMA hatuwezi kuficha ukweli kwamba nayo pia ina makundi yake. Ni mawili. Kundi la kwanza liko Makao Makuu ya chama. La pili liko mikoani.
Imedaiwa kwa haki kabisa kwamba kundi la kwanza la CHADEMA lililoko Makao Makuu ya chama ni kundi linaloundwa na viongozi wa Makao Makuu na watendaji wakuu wa chama hicho, wakiwamo wakurugenzi.
Inaonekana kuwa lengo kuu la kundi hili ni kulinda maslahi binafsi. Furaha kubwa ya kundi hili ni kuhakikisha kuwa ruzuku ya shilingi milioni 66 inayopata CHADEMA kila mwezi haifiki mikoani. Badala yake inatumiwa nao kwa mishahara na posho za safari za magari na helikopta zisizokwisha na zisizo na manufaa yoyote kwa chama.
Kuna habari kwamba baadhi ya wale walioko makao makuu wamenufaika na fedha za CHADEMA, kiasi cha kuanzisha miradi na biashara ambazo hawakuwa nazo kabla hawajajiunga na CHADEMA.
Kwa jumla kundi la kwanza la CHADEMA lililoko makao makuu linatuhumiwa kwa ubadhirifu, ufisadi, udikteta, matumizi mabaya ya fedha ikiwa ni pamoja na matumizi ya helikopta ambayo hayana tija yoyote katika ujenzi wa chama.
Juu ya yote, kundi hili linaaminiwa kuwa lina mawakala wa chama tawala ambao wamekaa pale kukomba tu fedha ya chama zinazowapeleka mikoani, huku wakiuacha Mkoa wa Dar es Salaam ukiwa hauna uhai wa chama kwa sababu safari ndani ya Dar es Salaam hazina posho. Kwa kifupi kundi la kwanza la CHADEMA lililoko makao makuu ni kundi la wababe wasio na uchungu wowote na chama na wanaoendesha chama kama vile ni kampuni yao binafsi. Kiongozi au mtendaji yeyote anayethubutu kupambana na maovu yanayoendelea kutendwa na kundi hili la kwanza anahatarisha nafasi yake. Atafukuzwa bila kupewa nafasi ya kujieleza, hata kama atakuwa ameitwa kwenye kikao hicho ili ajieleze. Hiyo ni demokrasia kwa staili ya Makao Makuu ya CHADEMA. Nani anabisha?
Kundi la pili la CHADEMA ni lile lililoko mikoani. Lengo kuu la kundi hili ni kuhakikisha kuwa lengo la chama cha upinzani la kushika madaraka ya utawala linatimia. Hili ni kundi lenye uchungu wa kweli na chama. Ni kundi linalotaka nguvu zote za chama zielekezwe kwenye kujenga chama ngazi zote.
Ni kundi linalotaka kujenga mtandao wa chama nchi nzima. Kundi hili linataka chama kiwe na ofisi mikoani kote na wilayani ili wanachama wapate mahali pa kukutana, kupata wanachama wapya, kufundishana sera za chama, na kubadilishana mawazo juu ya ujenzi wa chama utakaosaidia kuleta ushindi katika chaguzi mbalimbali. Kwa kifupi hili ni kundi linalotaka chama kiwe cha watu wote badala ya kugeuzwa kuwa kampuni ya watu binafsi.
Kundi hili la pili lililoko mikoani ambalo ndilo lenye uchungu na chama linapinga vikali matumizi ya helikopta wakati wa kampeni za uchaguzi, wakati wagombea ubunge na udiwani hawapewi hata shilingi moja ya kuwawezesha. Kundi hili pia linataka ruzuku ya chama isiishie kufujwa makao makuu, bali ifike mikoani ili kusaidia kufungua matawi na kuwafikia wananchi wa vijijini ambao hawana habari zozote za CHADEMA.
Lakini kundi hili la CHADEMA lililoko mikoani linapodai lifikishiwe ruzuku huambiwa na Katibu Mkuu wa chama kuwa mikoa na wilaya zinapata ruzuku kwa kupelekewa bendera na kadi za chama! Hapa mtu hakosi kujiuliza.
Bendera za chama zitatundikwa wapi na kadi za chama zitagawiwa wapi wakati chama hakina ofisi mikoani na wilayani? Na viongozi wa chama mikoani watakwendaje kufungua matawi kama ruzuku wanayopelekewa ni bendera na kadi tu za chama bila kupelekewa nauli na kodi za mapango?
Kwa kila hali, CHADEMA Makao Makuu imepoteza matarajio ya wanachama wake na wananchi kwa jumla. Kibaya zaidi Katibu Mkuu wa CHADEMA hajui matatizo ya mikoani. Hatembelei mikoa.
Wakati chama kikiendelea kuendeshwa vibaya makao makuu, kundi la CHADEMA lililoko mikoani lilikaa likisubiri saa ya ukombozi. Ikafika.
Ilitokea kwamba Desemba mwaka 2007, CHADEMA ilifanya uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa chama. Kundi la kwanza la CHADEMA lililoko makao makuu likamwandaa mgombea wake. Kundi la mikoani halikukutana kumwandaa mgombea.
Wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA ndio waliopewa jukumu la kumchagua makamu wa mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya chama. Kura zikapigwa. Mgombea aliyeandaliwa na makao makuu alipata kura 37, wakati mgombea ambaye makao makuu yalipambana naye, Zakayo Chacha Wangwe, alipata kura 56. Nguvu ya umma ilifanya kazi.
Huko nyuma viongozi wa CHADEMA walizoea kuhubiri kuwa nguvu ya umma inayotakiwa ni ya kuiondoa CCM madarakani. Hawakuona uwezekano wa kutumiwa nguvu ya umma kuleta mabadiliko na ushindani wa kweli ndani ya chama.
Lakini hapa wajumbe wa mikoani, kwa kumchagua Chacha Wangwe aliyekuwa ameandaliwa kushindwa, walikuwa wamefanya mapinduzi makubwa yaliyothibitisha kuwa nguvu ya umma, inaweza kutumika ndani ya chama kutimiza matakwa ya walio wengi.
Wajumbe wa Baraza Kuu waliomchagua Chacha Wangwe kihalali na kidemokrasia kuwa Makamu Mwenyekiti waliamini kuwa huo ulikuwa mwisho wa ushindani. Lakini sivyo ilivyotokea. Makao Makuu ya CHADEMA hawakukubali kushindwa.
Hivi leo Makao Makuu ya CHADEMA si tu kama Chacha Wangwe anatengwa na haungwi mkono katika mipango yake ya kukileta chama kwa watu. Ananyanyaswa pia. Kwa mfano aliendelea kunyimwa chumba cha ofisi makao makuu.
Akalazimika kujipatia kwa nguvu. Lakini Chacha Wangwe ambaye amedhamiria kukijenga chama si mtu wa kukata tamaa. Anaandaa mikutano na maandamano yanayofanikiwa kutokana na ushirikiano mkubwa anaopata kutoka viongozi wa mikoa na wilaya, huku watu wa makao makuu wakimwangalia kwa husuda. Katika kumharibia jina Chacha Wangwe Makao Makuu ya CHADEMA yanaeneza uzushi kwamba yeye ni wakala wa CCM. Lakini nani hajui kuwa yeye ndiye mpinzani wa kweli?
Kwa jumla kundi la CHADEMA lililoko makao makuu ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo na uhai wa CHADEMA. Ni kundi lisiloheshimu demokrasia. Makao Makuu CHADEMA kimebaki chama kinachotaka kiendelee kuitwa cha "kidemokrasia" huku kikiendeshwa kidikteta.
Kwa mfano hatua ya makao makuu kumtenga Chacha Wangwe aliyechaguliwa kihalali kuwa Makamu Mwenyekiti siyo ya kidemokrasia. Ni ya kidikteta. Vile vile hatua ya kufukuza watendaji wenye mtazamo tofauti bila kupewa nafasi ya kujieleza pia ni udikteta. Hivi sasa kuna uhasama mkubwa kati ya makao makuu na wanachama wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam wanaoshirikiana na Chacha Wangwe kukijenga chama Dar es Salaam. Kwa mfano mwanachama mmoja wa CHADEMA mkoani Dar es Salaam ametiwa ndani na mtendaji wa makao makuu bila kufanywa juhudi yo yote ya kumaliza masuala ya chama ndani ya chama.
Na huko Makao Makuu ya CHADEMA kinachoendelea ni juhudi za kumkwamisha Chacha Wangwe ili kazi yake isionekane, kusudi asipate nafasi ya kuchaguliwa tena kuwa kiongozi. CHADEMA itafanya makosa kumpoteza kiongozi safi asiyehusishwa na ubadhirifu wala ufisadi.
Chacha Wangwe ni mpambanaji hodari asiyetetereka na kila mwananchi mwenye mapenzi ya kweli na CHADEMA, hasiti kumuunga mkono. Kwa mfano mjini Dar es Salaam aliungwa mkono alipoitisha maandamano ya kupinga hatua ya wananchi wa Tabata Dampo kuondolewa kwenye makazi yao kwa nguvu ili kumpisha mwekezaji.
Na Chacha Wangwe ni mpiganiaji mkubwa wa haki za binadamu, ameamua kuendeleza mapambano ya kutetea ardhi ya wananchi.
Lazima aungwe mkono ama sivyo tutakuwa tunawandaa watoto wetu kwa vita dhidi ya wawekezaji ambao kwa kweli watageuka kuwa walowezi.
Tukirudi CHADEMA Makao Makuu tutaona kwamba yamekaa kulaumu CCM kwa udikteta, wakati CHADEMA inaendeshwa kidikteta. Wamekaa kulaumu serikali ya CCM kwa ubadhirifu na ufisadi kana kwamba CHADEMA hakuna wabadhirifu na mafisadi.
Lakini pia CHADEMA imeendelea kulaumiwa kwa ukabila. Ni ukabila wa CHADEMA uliosababisha kati ya wabunge sita wa viti maalumu watano watoke kabila moja. Pia ni ukabila uliosababisha karibu nusu ya wakurugenzi wote wa CHADEMA watoke kabila moja. Na hivi sasa kuna tetesi kuwa vigogo wa kabila moja wanamwandaa mtu wao ili achaguliwe kuwa Rais mwaka 2010. Watanzania wasifanye makosa kumpeleka Ikulu Rais atakayejaza watu wa kabila lake.
Hivi basi, ndivyo makao makuu ya CHADEMA yalivyoshindwa kutimiza matarajio ya wananchi. Lakini CHADEMA si makao makuu. CHADEMA ni wanachama na wananchi. Kwa hivyo wanachama wa CHADEMA mikoani wana jukumu kubwa la kusafisha CHADEMA Makao Makuu ili CHADEMA itimize matarajio ya wananchi.