CHADEMA na ndoto za kumuondoa Meya Arusha!

CHADEMA na ndoto za kumuondoa Meya Arusha!

Mtu ukiwa kimya muda mrefu ukrudi tunategemea uje na mambo mapya na yenye maana sasa wewe ulikimbia jukwaa umerudi kwa pumba hiyo?duh viongozi wa ccm majanga kama huyu naye ni katibu wa itikadi duu amakweli
 
Kujipa matumaini ni jambo zuri lakini kujipa matumaini ya uongo ni jambo la hovyo! Kwa idadi ya madiwani katika Jiji la Arusha na mgawanyo wake hakuna chama kinachoweza kufikisha 2/3 ya madiwani na kwa kuwa kanuni zinasema ili umwondoe Meya kwa kura ya kutokua na imani naye lazima upate 2/3 ya madiwani wote, basi Meya is there to stay!

Ushauri wangu ni kuwa waliochaguliwa wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi badala ya kuahangaika na ndoto za mchana!

Mie nililisema hili humu jamvini kuwa suala la uchaguzi wa meya ni gumu, watu mkabisha mpaka mapovu yakawatoka, cha msingi ni kuwatumikia wananchi , meya huyo wa Arusha atosha.
 
Kujipa matumaini ni jambo zuri lakini kujipa matumaini ya uongo ni jambo la hovyo! Kwa idadi ya madiwani katika Jiji la Arusha na mgawanyo wake hakuna chama kinachoweza kufikisha 2/3 ya madiwani na kwa kuwa kanuni zinasema ili umwondoe Meya kwa kura ya kutokua na imani naye lazima upate 2/3 ya madiwani wote, basi Meya is there to stay!

Ushauri wangu ni kuwa waliochaguliwa wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi badala ya kuahangaika na ndoto za mchana!
kinachopangwa na chadema lazima kitimie maana kinakuwa na baraka za Mungu kwa sababu ni kwa manufaa ya wananchi hakina hila ndani yake
 
...Uzuri wa Nape ana kahofu kidogo ka Mungu, tofauti na Mwigulu. Hili najua hatakujibu - tusubili.

Mkuu nakusapoti juu ya Nape kuwa na hofu ya Mungu, kwani amekuwa akienda shule ya jumapili, kifupi anayo maadili ya Mungu. Hofu yangu ni Mwigulu, nadhan ametoka kwenye familia ya wachuna ngozi na wauaji wa albino kwo amezoea kazi ya kuua watu... Nape mwambie Mwigulu kuwa Mungu hapendi tabia yake. Ageuke aone wapi alipojikwaa na Bwana wa Majeshi atamsamehe tu...
 
yuko wapi chriss lukos wapi wewe kiumbe uliyekejeli hapa jamvini jmosi kisha 4-0 ukakimbia jamvi iteni tena sombetini mpate 1-0 iwe 5-0 hahahaahahahahah umeya kweli mnaota
 
Last edited by a moderator:
kinachopangwa na chadema lazima kitimie maana kinakuwa na baraka za Mungu kwa sababu ni kwa manufaa ya wananchi hakina hila ndani yake

Acha kumshirikisha Mungu kwenye chama ambacho kinaua watu kwenye mikutano, chenye kupendelea dini moja na ukanda mmoja.

kanuni zipi zilifatwa hapo'nasikia mnahangaika na diwani wa Tlp mpate kura yake'Arusha mliacha nini nyie watu
 
Kwa kiwango fulani Nape nakutofautisha sana na Mwigulu. Wewe una utu kidogo na unakubali kutokubaliana ila tuu uko ndani ya kundi baya. Pamoja na yaliyosemwa yote ndani ya uzi huu ningekuomba uendelee kukaa mbali na huyo bwana madevu Mwigulu Nchemba, atakumaliza huyo. Yeye ni kama simba anayeweza kula mpaka watoto wake.
Out of topic unaonaje ukija na uzi wa kuelezea habari iliyo zagaa mjini kuwa Mwigulu kwa kutumiwa na mzee wa mvi walikutegeshea Juliana Shonza mkajivinjari mkirekodiwa na mkanda huo unatumika ili kukumaliza wewe? Tunaamini kuwa ni kweli kwa vile Mwigulu ametokea kuwa bingwa wa kuandaa mikanda ya video kwa manufaa ya kisiasa. Tuweke sawa mkuu.
 
Last edited by a moderator:
32Roberts
Kanuni za uchaguzi wa Meya ziko wazi, hachaguliwi kwa 2/3 isipokua kumwondoa unahitaji 2/3!
Jiangalieni sana magamba,CDM wako kazini muda huu,naomba nikwambie kitu kimoja,Timu ya CDM Arusha (Viongozi wote wa mkoa) wako makini kuliko unavyofikiria,na madiwani wa CCM wanaipenda CDM ndani ya mioyo yao,kuwa makini sana.
 
Acha kuwapotosha watu...
Si lazima chama chenyewe kiwe na 2/3 ya madiwani kama unavyosema. Kikanuni ikiwa 2/3 ya madiwani wote watapiga kura ya kutokuwa na imani na huyu "Meya" wa kichina basi anaondolewa. Na hili ndilo wananchi wanataka kuliona likitendeka.
Tusubiri kuona demokrasia ikichukua mkondo wake.
Kutokana na ubabe wenu wa kuwashinikiza, kuwanunua wajumbe na mbinu nyingine haramu wengi wa madiwani katika Jiji la Arusha hawamtaki "Meya" mlompandikiza cheo kinachomzidi akili!

Kujipa matumaini ni jambo zuri lakini kujipa matumaini ya uongo ni jambo la hovyo! Kwa idadi ya madiwani katika Jiji la Arusha na mgawanyo wake hakuna chama kinachoweza kufikisha 2/3 ya madiwani na kwa kuwa kanuni zinasema ili umwondoe Meya kwa kura ya kutokua na imani naye lazima upate 2/3 ya madiwani wote, basi Meya is there to stay!

Ushauri wangu ni kuwa waliochaguliwa wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi badala ya kuahangaika na ndoto za mchana!
 
Nape acha kuongea usichokiamini na kibaya zaidi unaonglea chini ya meza! Usikwepe mjadili kwanza kiongozi wako wa kampeni muliokamteua aende kule Arusha.Maana tunakuona mbabaishaji tu,Muda si mrefu uliopita umenukuliwa ukisema "HAUWEZI KUONGELEA YA UCHAGUZI WA ARUSHA KWA KUWA NI SWALA DOGO KWAKO" Sasa utusaidie wewe na Mwigulu nani anacheo kikubwa zaidi ya mwenzake? Lkn pia utuambie kama Mwigulu ni naibu katibu mkuu wa ccm mkoa wa Arusha au wilaya ya Arusha bila kumsahau Tayson utuambie anacheo gani?.Maana kwa mujibu wa ulopokaji wako umebainisha ya kuwa viongozi wenu wakitaifa tukianzia na wewe amukuwa na amuna muda wala nafasi ya kufuatilia na kuzungunzia suala la Uchaguzi wa Arusha,Sasa hao niliokuorodheshea ni baadhi tu ya walionekana wakitia kambi Arusha.Sasa watu wakizani ni miongoni mwa viongozi wenu wa kitaifa! Kumbe wewe mwenezi hauwatambui !?.Duuh hili ni balaa kubwaaa sasa
 
Acha kumshirikisha Mungu kwenye chama ambacho kinaua watu kwenye mikutano, chenye kupendelea dini moja na ukanda mmoja.

wananchi waliopigia kura Mbeya kuichagua chadema ni wa ukanda gani? na waliopigia kura kuichagua chadema kigoma vijijini ni wa ukanda wa wapi? na waliopiga kura kuchagua chadema Mwanza ni wa ukanda wa wapi? hoja zenu za hila ndizo zinazoipaisha chadema na kudidimiza ccm
 
Mnauwa wananchi wetu kwa ajili ya umea...nyie watu wa hovyo sana...lakini Alutha conti nua.
Kujipa matumaini ni jambo zuri lakini kujipa matumaini ya uongo ni jambo la hovyo! Kwa idadi ya madiwani katika Jiji la Arusha na mgawanyo wake hakuna chama kinachoweza kufikisha 2/3 ya madiwani na kwa kuwa kanuni zinasema ili umwondoe Meya kwa kura ya kutokua na imani naye lazima upate 2/3 ya madiwani wote, basi Meya is there to stay!

Ushauri wangu ni kuwa waliochaguliwa wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi badala ya kuahangaika na ndoto za mchana!
 
Kujipa matumaini ni jambo zuri lakini kujipa matumaini ya uongo ni jambo la hovyo! Kwa idadi ya madiwani katika Jiji la Arusha na mgawanyo wake hakuna chama kinachoweza kufikisha 2/3 ya madiwani na kwa kuwa kanuni zinasema ili umwondoe Meya kwa kura ya kutokua na imani naye lazima upate 2/3 ya madiwani wote, basi Meya is there to stay!

Ushauri wangu ni kuwa waliochaguliwa wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi badala ya kuahangaika na ndoto za mchana!

Mkuu
Kwa Arusha ninayoijua mimi Mbona uyo Meya atajiuzulu mwenyewe akimbie Arusha kabisa..!!
Ngoja uone
 
Meya wa Jiji la Arusha, Gaudance Lyimo (CCM), ametamba kuwa wanaofikiria kumng’oa kwenye kiti chake wanaota ndoto za alinacha kwa sababu lazima wazingatie kanuni za uendeshaji wa Mabaraza ya Madiwani.

Baada ya kushinda kata nne za Arusha kwenye uchaguzi mdogo juzi, Chadema ilitamba kuwa kazi inayofuata ni kumng’oa Meya kutokana na kuwa na viti vingi kwenye Baraza la Madiwani.

Lyimo aliliambia Mwananchi kuwa pamoja na Chadema kuwa wajumbe wengi kwenye Baraza la Madiwani, bado hawana ubavu wa kumtoa.

Alisema ili kumtoa katika nafasi hiyo wanahitaji kuwa na theluthi mbili ya wajumbe . Lyimo alisema maana yake ni kuwa ili ang’oke lazima Chadema waungane na madiwani wa CCM ndiyo watafanikisha azma hiyo.

“Sharti la kumng’oa madarakani Meya au Mwenyekiti wa halmashauri ni kupata theluthi mbili ya kura za wajumbe wote. Najiuliza wenzetu watafikiaje kiwango hicho hadi waanze kutamba kuning’oa madarakani,” alisema Lyimo.

Jiji la Arusha lina jumla ya wajumbe 32 kwenye Baraza la Madiwani ambapo ukimtoa Meya, wajumbe wanaostahili kupiga kura wanasalia 31 hivyo kufanya wenye nia ya kumng’oa kiongozi huyo kuhitaji zaidi ya kura 24 kutimiza lengo lao.

Baada ya kunyakua viti vyote vinne kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jumapili iliyopita, Chadema imefikisha wajumbe 15 kwenye baraza ikiwa ni madiwani 12 pamoja na wabunge watatu, wawili wa viti maalumu na mmoja wa jimbo.

Kwa upande wake, CCM kimebakia na wajumbe 14, ikiwa ni madiwani 11 na wabunge watatu wa viti maalumu, huku TLP ikiwa na wajumbe wawili ambao ni diwani mmoja wa kata na mwingine wa viti maalumu.

Kata ya Sombetini ambayo awali ilishikiliwa na CCM iko wazi baada ya aliyekuwa diwani wake, Alphonce Mawazo kujivua uanachama na kuhamia Chadema.

Kutokana na mchanganuo huo, Meya Lyimo alisema hana hofu ya kupoteza nafasi yake kwa sababu ili Chadema wafikie lengo hilo, ni lazima waungwe mkono na wajumbe kutoka CCM, jambo alilosema ni ndoto ya kutokea.

“Nakusisitizia ndugu yangu, mimi nipo na nitaendelea kuwepo hadi mwisho wa kipindi changu kwa uwezo na msaada wa Mwenyezi Mungu. Hakuna wa kuning’oa. Hata leo nilikuwa ofisini kutekeleza majukumu yangu ya kuongoza kikao cha kamati ya fedha,” alitamba Lyimo.

Meya huyo aliwataka madiwani kutoka Chadema kuacha kupoteza muda na nguvu nyingi kuweka mikakati ya kumng’oa madarakani, badala yake watumie muda na nguvu hizo kuwatumikia wananchi waliowaamini na kuwapigia kura kwenye uchaguzi.

Haha leo Meya wa kichina ndio anajua sharia na taratibu za uendeshaji wa mabaraza si alipachikwa bila quorum kufika ha ha jasho linamtoka wenzake wa CCm watambutua tuu hafai amesababisha fujo Arusha na kusababisha mauaji
 
Nape,
Matokeo ya 4-0 kwa CCM sio jambo la kawaida hata kidogo. Wala sio la kujifariji kwa kubaki na Meya. Hili ni pigo la pili zito sana kwa mji wa Arusha pekee likifuatia zile jitihada zenu za kumng'oa Godbless kushindikana kwa aibu.

Rudisheni CCM ya Mwalimu. Huu mji una historia ya pekee kwa TANU/CCM.
 
kumbe ccm kuna watu waliobaki wenye busara hihi? Mi ndo mara ya kwanza nimemkubali mwanaccm hongera ila nakushauri uwahame make watakupaka kinyesi!

inakufa taratibu??ccm imekufa siku nyingi!!!inapumulia mashine za polisi,uwt,tume ya uchaguzi na mahakama,mamluki ET AL!!!

Nilikuwa napita tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom