CHADEMA na ndoto za kumuondoa Meya Arusha!

CHADEMA na ndoto za kumuondoa Meya Arusha!

Sihusiki na hisia zako, huu ndio ukweli Chama makini kingejadili kuwatumikia watu badala ya kupoteza siku nzima mnajadili jambo lisilowezekana
Mheshimiwa Nape nakupa Pole kwa yaliyowapata kule Arusha, lakini nikupe ushauri mdogo ambao nafikili ungeufanyia kazi ungeonekana ni muungwana na wala huna chuki binafsi ila ni siasa tu. Ushauri wenyewe ni kwamba uchaguzi umepita, kilichobaki ni kuangalia next year kwa nyie wa vyama vya siasa lakini mnatakiwa hata kama dhamira yako haikutumi jitahidi kuficha hilo kwa kuwapongeza walioshinda. Pia nikupongeze kwa kazi nzuri unayoifanya ya kuhakikisha kijana mwenzako Mwigulu anaendelea kuropoka huku wewe ukionekana kutumia japo busara kidogo kwa kuongelea walau mambo ya kitaifa kwama watu wahimize maendeleo. Nasema hivyo kwa sababu mpaka sasa hujaonesha kwa wazi nani hasa unamuunga mkono kati ya wanaotajwa tajwa kutaka kukalia pale magogoni. Mwenzako toka Singida ameshatangaza kwamba Rais ajaye ni Lowasa pale Mwanza wewe uko upande gani?
 
Tatizo lako nepi ni kusahau ya jana, wakati unasema hatoki Meya kumbuka meya huyo aliingiaje na kwa jinsi alivyoingia atatoka kwa style ile ile watu wa Arusha hatutanii na kwa hili wewe Nepi kaa kimya usikilize majibu.
 
Mkuu Mwita,
Hili ni hatari kwa vyama vyote. Ebu emagine bajeti ya mishahara ya wafanyakazi inakwamishwa kwa kura za chadema hapo unafikiri nani ataathirika? Itabidi waangalie sana vitu vya kupinga.

Mimi nafikiri mvutano huu ni jambo jema kwa Arusha. Ccm hawawezi tena kupeleka mipango yao mibovu maana itapigwa chini. Itabidi wakae chini na kuamua pamoja maeneo ya maana ambayo ndio yanaweza Kupita.


Jambo moja nililo na uhakika nalo ni kuwa meya wa ccm hatoweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa madiwani wa Chadema hawatomuunga mkono. Hata kama sheria na kanuni za uendeshaji wa mabaraza ya madiwani zitawabana Chadema katika kufikia azma yao ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani na meya wa jiji lakini ccm na nape watambue kuwa kwa mazingira yaliyopo meya huyo hawezi kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Wanachoweza kufanya madiwani wa Chadema ni kuhakikisha kuwa mipango yote ya meya wa kichina wa ccm haipitishwi na baraza lao na badala yake mipango na mikakati yao ndiyo inapitishwa na kutekelezwa kwakuwa katika maamuzi ya baraza utaratibu ni kupiga kura na uamuzi unafanywa kwa simple majority na hakuna mambo ya 2/3 ya kura za wajumbe.

Ni dhahiri kuwa katika hali kama hiyo nape na ccm yake wanajidanganya kudhani kuwa meya hatang'oka bila kufikiria kuwa atawezaje kufanya kazi zake ikiwa wajumbe wengi wa baraza la madiwani hawamuungi mkono.Kwa muda huu ambapo nape na chatanda wanajifaragua kuwa meya kuondolewa madarakani ni ndoto basi waacheni waendelee kujifaragua ila itakapofika wakati wa shughuli za mabaraza na meya kutaka kutekeleza majukumu yake ndipo wataijua Chadema.
 
[h=2] ALAT yasikitishwa viongozi wa mitaa kuong'olewa kienyeji
[/h] Ijumaa, Julai 27, 2012 06:03 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

JUMUIYA ya Serikali za Mitaa (ALAT) imesikitishwa na wimbi ya viongozi wa Serikali za Mitaa kung'olewa madarakani kwa tuhuma na vurugu bila kufuata taratibu na kanuni za kisheria.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa ALAT, Dk. Didas Ma------, ambaye ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, ametoa mifano ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliongolewa madarakani kufuatia tuhuma zilizotolewa na madiwani dhidi yao.

Alitaja mifano michache ya halmashauri zilizokumbwa na matatizo hayo kuwa ni Rungwe, Mbeya, Tabora, Kibondo, Kigoma, Shinyanga na Misungwi.

Alisema wenyeviti wa halmashauri hizi wameng'olewa kwa sababu ya tuhuma zilizoibuliwa na madiwani.

"Maeneo mengi kuondolewa kwa viongozi hawa, kuliambatana na vurugu," alisema Dk. Ma------.

Alisema ALAT imekemea vikali tabia ya kuwang'oa viongozi wa Serikali za Mitaa kwa njia ya vurugu na tuhuma na kuelezea vitendo hivyo kama ukiukwaji wa misingi ya utawala bora na kinyume cha sheria za Serikali za Mitaa na za nchi.

Alisema Sheria za Serikali za Mitaa Na. 7 na 8 za Mwaka 1982 pamoja na Taratibu za Kumuondoa Mwenyekiti wa Halmashauri za Mwaka 1995 (Taratibu za Kumwondoa Madarakani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Tangazo la Serikali Na. 263 la Tarehe 19/5/1995), na Taratibu za Kumwondoa Madarakani Mwenyekiti/Meya (Tangazo la Serikali Na. 264 la Tarehe 19/5/1995)-zote zinaweka utaratibu wa kufuata wa kuwandoa viongozi hao.

"Lakini cha kushangaza katika maeneo mengi, viongozi wa Serikali za Mitaa, wameng'olewa bila kufuata taratibu hizi za kisheria. Serikali zipo lakini zinakiukwa," alisema Dk. Ma------.

Aliwaasa viongozi madiwani na viongozi wengine wa Serikali za Mitaa kuheshimu taratibu na sheria katika kuwaondoa viongozi wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali.

Alisema kama sheria hazitaheshimiwa migogoro na vurugu zitaendelea na hivyo kuzifanya zishindwe kutoa huduma kwa wananchi na kushindwa kuchochea maendeleo katika maeneo husika.

Alisema Kamati ya Utendaji ya ALAT inatarajia kukutana kujadili matukio na wimbi la viongozi wa Serikali za Mitaa kung'olewa katika maeneo mbalimbali.

"Mbali na hilo, ALAT itachambua sheria za Serikali za Mitaa na zile za kuwaondoa madarakani viongozi, kwa lengo la kuziboresha na tuleta tija na ufanisi ili pale mwenyekiti au meya wanapata tuhuma waweze kuchukuliwa hatua na kuondoa migogoro na kujengo mshikamano na umoja katika halmashauri," alisema Dk. Ma------.
 
Tatizo ni dogo sana umechanganya uongo na ukweli pamoja ndo maana hauliki! Ni kweli kuwa mie muumini wa uimara wa upinzani kuisaidia CCM kufanya vizuri zaidi.Na imani hii siisemei chumbani naisema hadharani. Mengine ni hisia zako ambazo hazinihusu!
Mkuu achana na hao wachokonozi bwana, hawajui wanachokiongea. ....Du! ila lile vazi lako linalofanana na suti nyeusi ya Mbowe huwa nalipenda! Naona hata Mwigulu ameanza kukuiga ingawa yeye kashona la kijani.
 
Nape bana! Ulikuwa kimya, mara umeibuka kama kakakuona. Najua matokeo ya arusha umeyafurahia. Si unamjua mwanaume wa shoka anayetoka monduli? Naona uswahiba wenu utaimarika zaidi kuanzia sasa.
 
Ningejuaje kama usingesema, ungesemaje kama nisingesema? Ahsante kwa taarifa

Nape, kuna taarifa kuwa ulirekodiwa ukivunja amri ya .... na ukakamatwa ugoni. Je unawaeleza nini wadau wa JF juu ya jambo hili?
 
Sihusiki na hisia zako, huu ndio ukweli Chama makini kingejadili kuwatumikia watu badala ya kupoteza siku nzima mnajadili jambo lisilowezekana

OMG kumbe unawajua wahusika??? ila wewe hauhusiki na hizo hisia??? najua nafsi yako ina Mungu, mwisho wa siku utawataja kwa majina!!!


 
Nafikiri umejua kuwa nimesema ulikamatwa na mke wa mtu kwa fitina za mwigulu, na kwa kuwa nisingeweza kusema kama usingesema niseme, basi kwa kuwa nimesema hili basi utakuwa umepata cha kusema. Hivyo naomba useme juu ya tuhuma hizi za ugonile.
 
Hivi kati ya wale madiwani walofukuzwa na cdm wapo walogombea kupitia chama kingine tena? Kama ndio ni chama gani na walipata kura ngapi7?
 
Nape achana na hilo li-chama lenye siasa za maji taka.
 
Mbona una hofu sana wewe gamba?Subiri uone kama itakuwa ngumu kumwondoa huyo gamba mwenzako.Arusha imeshakombolewa.Acha kutoa mapovu bure.
Kujipa matumaini ni jambo zuri lakini kujipa matumaini ya uongo ni jambo la hovyo! Kwa idadi ya madiwani katika Jiji la Arusha na mgawanyo wake hakuna chama kinachoweza kufikisha 2/3 ya madiwani na kwa kuwa kanuni zinasema ili umwondoe Meya kwa kura ya kutokua na imani naye lazima upate 2/3 ya madiwani wote, basi Meya is there to stay!

Ushauri wangu ni kuwa waliochaguliwa wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi badala ya kuahangaika na ndoto za mchana!
 
Kujipa matumaini ni jambo zuri lakini kujipa matumaini ya uongo ni jambo la hovyo! Kwa idadi ya madiwani katika Jiji la Arusha na mgawanyo wake hakuna chama kinachoweza kufikisha 2/3 ya madiwani na kwa kuwa kanuni zinasema ili umwondoe Meya kwa kura ya kutokua na imani naye lazima upate 2/3 ya madiwani wote, basi Meya is there to stay!

Ushauri wangu ni kuwa waliochaguliwa wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi badala ya kuahangaika na ndoto za mchana!

Vipi kuhusu mafisadi papa mliotaka wajivumbe gamba ndani ya siku 90, bado hazijatimia, au mlimaanisha RA peke yake? Pambana na Lowassa kwanza kabla ya CDM. Vipi Mzee Makamba alishakurudishia kadi yako ya uanachama wa CCM na UVCCM alizokunyang'anya katika mkutano Iringa?
 
Tatizo ni dogo sana umechanganya uongo na ukweli pamoja ndo maana hauliki! Ni kweli kuwa mie muumini wa uimara wa upinzani kuisaidia CCM kufanya vizuri zaidi.Na imani hii siisemei chumbani naisema hadharani. Mengine ni hisia zako ambazo hazinihusu!

kwa hili utatufurahisha wengii na linaonyesha ukomavu wako, ila hii busara ungempa na ndugu yako mwigulu... Maana inaelekea mnapigana vita mbili tofautii kabisaa na mkiendelea hivi ipo siku wenye mrengo huu ndani ya CCM ambao una maslahi kwa nchi kulioko chama mtakuja nyukana makonde na wahafidhihina kama mwigulu wenye nia moja tuuu ua upinzani CCM itawale milele.. It time to do house cleaning, you should take care of them before they take care of you
 
Kumbe umeya ndiyo kihoro chenu, hadi mmediriki kuua raia wema kwa mabomu

siasa maji taka .... Rostam Aziz

Kumbe wewe ndiye Polisi uliyeona wakiua, wewe si Polisi punguani ambaye mpaka sasa hujawakamata wauaji uliowaona? Acha hizo!
 
Kujipa matumaini ni jambo zuri lakini kujipa matumaini ya uongo ni jambo la hovyo! Kwa idadi ya madiwani katika Jiji la Arusha na mgawanyo wake hakuna chama kinachoweza kufikisha 2/3 ya madiwani na kwa kuwa kanuni zinasema ili umwondoe Meya kwa kura ya kutokua na imani naye lazima upate 2/3 ya madiwani wote, basi Meya is there to stay!

Ushauri wangu ni kuwa waliochaguliwa wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi badala ya kuahangaika na ndoto za mchana!

Nape,
Ni jana au juzi umenukuliwa na vyombo vya habari nchini kuwa hukutaka kuongelea uchaguzi wa madiwani Arusha kwa kuwa si level yako. Uchaguzi wa madiwani kwako ni minor issue kwa kuwa kuna viongozi wa CCM mkoa wanaweza kulizungumzia hilo.

Sasa ni nini kilichokutekenya hadi kuja kuliongelea suala la kung'olewa "Meya wa kichina" ambaye pia mmoja wa madiwani mkoani Arusha wakati level ya udiwani ni ndogo sana kwako?? Au viongozi wa CCM mkoa wako likizo, imebidi u-step in kuziba hilo gap?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom