Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kufanya maandamano ya amani Nov 2, 2020 kupinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu

Hajjawahi kutokea Tanzania na yataendelea hadi kieleweke,wezi wameshikwa pabaya, wameingia nyumba sio.
 
Hahahhaha mkuu upo?
Naona mnachekelea baada ya kubaka uchaguzi.
Kma ulisoma law of diminishing returns then inapaswa uunge mkono maandamano ya kesho maana ndio yameshikilia hatma ya siasa zetu kwa miaka 20 ijayo.
Maandamano ya nini mkuu? Wananchi wameshamaliza kufanya uchaguzi.
 
Ndugu zangu Wana JF mimi ntakuwepo katika maandamano yaleo na ntakuwa ubungo bus terminal, naamini nawengine watakuwepo.

Haya nimaandamano ya amani yakudai demokrasia, baada ya demokrasia kupokwa katika sanduku lakura.

Najua wapo wengi watanibeza kwakuona tunachokipigania hakiwezekani lakini niwambie tu inawezekana kupata demokrasia yakweli tena katika wakati huu ambao wengi wanaogopa kumkabili jiwe .

Inawezekana nikafa kwa kupigwa lisasi na police ambao wanatumia siraha zilizonunuliwa kwa kodi zetu, lkn kamwe sintoogopa, maana demokrasia yakweli lazima izaliwe upya.

Siwezi kukubali nchi yangu igeuzwe kama Rwanda,Burundi au Uganda katika uminywaji wa demokrasia, hilo litatokea labda nikiwa gerezani au kaburini, hii ni nchi yetu sote wala si ya ccm peke yao.

" Naapaa, naaahidii ,nchi yangu Tanzaniaa, demokrasia yake ntailindaa mpaka kufaa", Naapa la naahidiii,nchi yangu Tanzaniaa, demokrasia yake ntailindaa mpaka kufaa". Ee Mungu naomba unisaidie.

Tukutane barabarani,saa mbili kamili asubuhi.
 
Yani nyie ndio makichaa kabisa em tulia uvae barakoa uko, mnatuhamasisha tuvuruge amani huku kwasababu hamtakuwepo hapa eeh, endelea kuota..
Wewe uko wapi ,mbona ip address yake inaonyesha huko hapa
 
TAARIFA MUHIMU SANA!!!

Watanzania tuishio nje ya nchi (TANZANIA DIASPORA) tumeanza kuandamana kupinga UCHAFUZI uliofanyika juzi hapo nyumbani Tanzania!

Hawa ni ndugu zetu kutoka Ulaya ya Kaskazini (Sweden , Norway na Denmark ) ambao tayari wameanza maandamano yao nje ya Ubalozi wetu uliopo Stockholm, Sweden...
Wewe utakuwa juha si bure. Unapinga kwani ulipiga kura? Acha uzembwete
 
Swali la kijinga sana hili. Umelirudiarudia siku nzima. Hivi hauna kingine cha kuuliza? Mamko angeweza kumzuia dikteta mwenye vifaru na mabunduki hayo? Muulize hapo mamko kama angeweza kuzuia uchaguzi uliotayarishwa na dikteta ambaye ana jeshi, TISS, polisi, NEC, Masajili, TCRA, Mamlaka ya Anga... Jibu atakalokupa mamko ndilo jibu hilo.
Mama yangu kaingiaje hapa, hebu jiulize mwenyewe kama una hata chembe ndogo tu ya busara.

Kama unajua "dikteta ana vifaru na mabunduki" haya maandamano unayohimiza hapa hawezi kuyatumia?

Ni lipi ni rahisi kutekelezwa: kufanya maandamano wakati 'dikteta' akishatangazwa kuwa mshindi, au kumvuruga akili na kuzuia njama zake za kuchafua uchaguzi?

Kama nilivyosema mwanzo, nilidhani najadili jambo muhimu la nchi yetu na mtu mwenye uelewa na utulivu wa akili, kumbe ni mmoja wa wapumbavu tu wanaojitokeza mara kwa mara hapa jamvini?

Sina muda wa kuendelea kupoteza na mtu wa aina yako.
 
Mamko ana jibu lake.
Na wewe unajihesabu kuwa upande wa upinzani?
Watu wa aina yako mnawaharibia sifa wapinzani wa kweli wanaofanya kila kitu kuleta mabadiliko ndani ya taifa hili.

Mnaifanya kazi yao kuwa ngumu sana, huku wakiumizwa nanyi huku pembeni mkishangilia.

Nakuacha uendelee na raha zako.
 
Hili anguko lilitegemewa hata wao wanajua. KUPINGA KILA JAMBO hata yale ya maendeleo halafu utegemee wapiga kura wakupe kura yao! Tukutane 2025 na mjipange vinginevyo hata zile siti chache za madiwani mtazikosa
 
Shida mnadhani siasa ni ajira. Huyo zitto au Lissu wana professions nje ya siasa so hawasaki life bali wanakula matunda ya taaluma zao hta nje ya siasa.

Kma mlidhani bila ubunge watakua kapuku kama ww then pole sana. Wenzio wana M.A za Warwick na Bucerius ndio uwaonee huruma?

Ndio yale mambo ya tajiri akiugua mnashangilia unadhani akiporomoka ww ndio utapanda!!

Typical black mentality
Sijui umetumia vigezo gani kuhitimisha kwamba mimi ni kapuku, na izo M.A za Warwick na Bucerius na vinginevyo aliyekuambia mtu anashiba pesa ni nani, bado mnataka posho za ubunge na mashangingi ya bure, pesa haitoshi usituone watoto wadogo.

Halafu ni Ameporomoka au wananchi wameamua kuchagua wawakilishi wengine, we sema tu black mentality unajikuta mzungu sana kama mpuuzi amstamdamry chiii, kaa kwa kutulia, rudi kitaa kumenoga.
 
Niko hapa buguruni shell nakunywa chai nawasubiri wadau! Tumejipanga tutathubutu na tunaweza! Tuliweza airport hatushindwi fanyeni chap chap

Safi sana, sisi tupo huku Ubungo... naona wapigania-haki wanazidi kumiminika tu.
 
Kumbusho:

Usibebe kitu chochote kinachoweza kutafsiriwa kuwa silaha, beba maji tu mengi ya kunywa na kunawa uso... ni maandamano ya amani.
 
Safi sana, sisi tupo huku Ubungo... naona wapigania-haki wanazidi kumiminika tu.
SAA mbili na dakika tano tunanyanyua mzigo safari inaanza, wengine tutakutana nao mbele kwa bwele! Msiache kubeba maji ya kunywa kama rejeta!
Nyerere asingeandamana Leo tusingemuita baba wa taifa
 
Vibaka na wanyang'anyi ndio hutumiaga huu mwanya. Na hao ndio watao andama. Watanzania sisi mpaka uamke ndio ule, uende ukaandamane utakula nini?
Usipojiongeza hayo maisha ya kuamka ndipo ujue utakula nini utakufa nayo.
 
Back
Top Bottom