Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,499
- 113,605
Wanabodi,
Tunakwenda shule ili kufunzwa maarifa, sio kupata akili, akili kila mtu anazo na anazaliwa nazo, ila jinsi ya kuzitumia ndicho tunachopaswa kujifunza na kufundishwa.
Mimi najihesabu ni muelimishaji umma kupitia kipindi changu cha TV, "Kwa Maslahi ya Taifa" na makala zangu za magazeti na humu JF.
Nimeamua kuanzisha darasa la watu kujifunza kwa wengine, hivyo nitakuwa nakuletea makala hizi za Face 2 Face zikihusisha mahojiano na watu mbalimbali kuhusu mada mbalimbali kwa kuwatumia watu hao kufundisha wengine.
Mwalimu wetu kwenye darasa la leo, ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe
Kwanza msikilize na uniambie umeelewa nini ili hicho ulichoelewa wewe uwafundishe na wengine.
View: https://youtu.be/RPpcwlnNJ0A?si=KLISZZ3sCb243xzz
Kwa vile sisi binadamu ni tofauti na tuna uwezo wa uelewa tofauti tofauti, mimi nimejitolea nitakuwa nawafanyia a short summary recaps ili wengi zaidi wafaidike na darasa hili.
Zitto ametufundisha kitu kipya kwenye siasa zetu, badala ya zile politics of confrontations za mikutano, maandamano, mivutano, kupigishana kelele and sometimes kutukanana kwa issues za kisiasa kusababishwa kuvuja kwa machozi jasho na damu, ACT Wazalendo inafanya siasa za politics of engagement.
Zitto Kabwe amesema
" Kwa miaka zaidi ya 30 ya siasa zetu za vyama vingi siasa zetu zimekuwa ni siasa za confrontations, kuandamana, kununa, kususa na hatupati chochote!.
Ukifanya jambo lili lile kwa namna ile ile ukitegemea matokeo tofauti, hapa utakuwa unajidanganya"
"Tumeamua kufanya siasa za engagement ili kuwezesha mageuzi kufanyika. Hiki kinachofanyika hapa ni matokeo ya kazi yetu, tumefanya mkutano Dodoma, tumeshiriki kwenye kikosi kazi, tumetoa mapendekezo, leo tunajadili utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi, hili ni jambo kubwa.
Huu sio mkutano wa kupindisha pindisha mambo, ni mkutano wa kunyoosha mambo kuleta matokeo chanya tunayoyataka.
Ofisi ya Waziri Mkuu imeishatangaza kuna miswada mitatu inapelekwa Bungeni kwenye Bunge la October kujadiliwa
4. Muswada wa kuhuishwa tume ya Warioba na kukwamua mchakato wa katiba mpya uliokwama
5. Muswada wa mabadiliko madogo ya katiba ili mabadiliko hayo yapate nguvu ya katiba.
Sisi tunafanya siasa za Pragmatism on doing and getting what is possible"
My Take
Hizi ndio siasa za ukweli, kinyume cha utopian politics".
Paskali

- Muswada wa mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi kuunda Tume Huru ya Uchaguzi
- Muswada wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi
- Muswada wa mabadiliko ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa